Kwanini TAMISEMI wamechagua wanafunzi kujiunga NACTVET?

MCHEBETE

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2016
Posts
326
Reaction score
596
Mh waziri Tamisem Angela Kairuki, wiki hii ametangaza chaguzi/selection za vijana wa kidato cha nne kujiunga na kidato cha tano pamoja vyuo mbalimbali.

Miaka ya nyuma vijana wote waliokuwa wakijiunga na vyou vya ufundi pamoja na uwalimu serikali ilikuwa inacover gharama zote au baadhi. Leo hii unampangia mtoto kutoka huko wilaya ya Misenyi aje kusoma chuo cha mwl Nyerere Diploma ada zaidi ya laki 9.

Mzazi hata uwezo wa nauli kufikisha mtoto wake Dar hana, ada atapata. Nimeajribu kuwasiliana na Tamisemi nimeambiwa kuwa waandike barua kwa katibu tawala wa mkoa kumueleza changamoto hii.

Nadhani hizi chaguzi zingejikita kuangalia hasa mazingira wanakotoka vijana, kama kuna ukakasi na wazazi wanashindwa somesha vijana wao elimu ya juu, huku chini inakuaje.
 
Na Mimi nimeona changamoto ni Ada hapo labda serikali inge cover hizo gharama ,wazazi wengi ni maskin sanaa kusomesha vijana wao vyuo vya Kati ,njia rahc ni kijana aende A level ilii aje aombe mkopo asome chuo kikuu
 
Ada minimum =660,000
Utakutana na Direct cost = 200,000
Hostel /year = 600,000
Pesa ya kujikimu 8,000 per day
Books & stationery??
Mtoto wa Form4 unampeleka chuo mkoani akili bado haijakomaa.

TAMISEMI Sijui walikua wanawaza nini, hapo solution ni kumpeleka mtoto Private tu maana gharama za chuo ni kubwa bado ana Dip1 & Dip 2[emoji119][emoji119][emoji119]
 
Mh waziri Tamisem Angela Kairuki, wiki hii ametangaza chaguzi/selection za vijana wa kidato cha nne kujiunga na kidato cha tano pamoja vyuo mbalimbali.

Miaka ya nyuma vijana wote waliokuwa wakijiunga na vyou vya ufundi pamoja na uwalimu serikali ilikuwa inacover gharama zote au baadhi. Leo hii unampangia mtoto kutoka huko wilaya ya Misenyi aje kusoma chuo cha mwl Nyerere Diploma ada zaidi ya laki 9.

Mzazi hata uwezo wa nauli kufikisha mtoto wake Dar hana, ada atapata. Nimeajribu kuwasiliana na Tamisemi nimeambiwa kuwa waandike barua kwa katibu tawala wa mkoa kumueleza changamoto hii.

Nadhani hizi chaguzi zingejikita kuangalia hasa mazingira wanakotoka vijana, kama kuna ukakasi na wazazi wanashindwa somesha vijana wao elimu ya juu, huku chini inakuaje.
Acheni ulalamishi somesheni watoto wenu, mmewazaa wenyewe ni wajibu wenu kuwasomesha. Kila kitu ulalamishi wakati unakula tunda kuna mtu alikusaidia au ulimgawia hilo tunda. Starehe mle wenyewe halafu mnakuja kulalamikia gharama za kusomesha watoto wenu? Ujamaa haupo tena.
 
Ada minimum =660,000
Utakutana na Direct cost = 200,000
Hostel /year = 600,000
Pesa ya kujikimu 8,000 per day
Books & stationery??
Mtoto wa Form4 unampeleka chuo mkoani akili bado haijakomaa.

TAMISEMI Sijui walikua wanawaza nini, hapo solution ni kumpeleka mtoto Private tu maana gharama za chuo ni kubwa bado ana Dip1 & Dip 2[emoji119][emoji119][emoji119]
uwongo mwingine uonage aibu, kulala 600,000/ chuo gani hicho wakati hata chuo kikuuu hakuna hiyo gharama
 
Akili inakomaa akiwa na umri gani?
 
uwongo mwingine uonage aibu, kulala 600,000/ chuo gani hicho wakati hata chuo kikuuu hakuna hiyo gharama

Umekariri sio kila chuo kina hostel zinatosheleza, mtoto aliyepangiwa pale Nyerere Memorial Kigamboni hakuna hostel pale itabd umtafutie histel za mitaani. Kwa semester wanacharge 300k
 
Muache aende chuo mtoto, akale upepo wa ferry. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tatizo naijua familia yake,yaani huyu alikuwa aende form five akomae aje akutane na kisanga cha Heslb huko mbele,
lakini uwezo wa mzazi kucover ada za diploma hawezi kabisa
 
Akili haijakomaa?Karne ya 21 kijana mwenye zaidi ya ,18+,unasema akili haijakomaa?watu tumesoma kutoka vijijini miaka ya 2000 tukaletwa udsm dar na tukasurvive,
Ishu hapa ni Ada na umaskini wa Wazazi,enzi hizo nimemaliza form4,nikapata nafasi college,mzazi alilipa ya kuanzia TU!nusu muhura,walipojua nimefika Dar college,sikutumiwa pesa tena,ilibidi Ile pesa ya kwendea field,niwe naitumia kulipia Ada,baada ya kuingia second year,ikabidi niwe natafuta na kazi za ufundi kitaa ili kusongesha maisha,Sina gheto,kukaa kwa ndugu shida,kipindi Cha likizo,tukawa tunaomba tubak hostel,ila msosi kujitegemea,mlo Mmoja kama mfungwa,
Wanaume tutafute pesa ili watoto wasome vzr,wengine tumefika hapa tulipo kwa miujiza,machozi,jasho na damu
 
unakuta mtoto kapangiwa Accountants TIA diploma miaka 3,hizi garama si kila mzazi anaweza afford.
kipindi cha nyuma colleges Serikali ina cover ,ikijua vijana ni wadogo watakaa hostel na accomodation nyingine.
ili kupunguza mzigo kwa wazazi
 
Kwa lugha nyingine serikali inawaambia wapelekeni watoto Private schools, wapiwapangia watoto wote shule , Private schools watapata wapi kodi za kulipa TRA?
 
Kabisa mkuu.ila saiv serikali hawa sponsor tena mzgo unabaki kwa mzazi.
unakuta mtoto kapangiwa Accountants TIA diploma miaka 3,hizi garama si kila mzazi anaweza afford.
kipindi cha nyuma colleges Serikali ina cover ,ikijua vijana ni wadogo watakaa hostel na accomodation nyingine.
ili kupunguza mzigo kwa wazazi
unakuta mtoto kapangiwa Accountants TIA diploma miaka 3,hizi garama si kila mzazi anaweza afford.
kipindi cha nyuma colleges Serikali ina cover ,ikijua vijana ni wadogo watakaa hostel na accomodation nyingine.
ili kupunguza mzigo kwa wazazi
 
Acheni ulalamishi somesheni watoto wenu, mmewazaa wenyewe ni wajibu wenu kuwasomesha. Kila kitu ulalamishi wakati unakula tunda kuna mtu alikusaidia au ulimgawia hilo tunda. Starehe mle wenyewe halafu mnakuja kulalamikia gharama za kusomesha watoto wenu? Ujamaa haupo tena.
umekurupuka sana mzee ,yaani kama sio Mtanzania,hapa tunaongea kuhusu huko tulikotoka,na jamii iliotuzunguka.
nimeleta uzi nafahamu mazingira ya umasikini wa hyo kijana.Nafuu yake kwenye elimu ilikuwakwenda kidato cha 5 na 6 ili chuo apate mkopo,na sio kumpeleka hivi vyou vinavyohitaji ada kutoka mfukoni kwa mzazi
 
Kimsingi hapa kuna bomu la ugumu wa maisha ya wazazi linaenda kuwalipukia vijana wao ,zamani vyuo kama hivii ukipangiwa watu walikuwa wanasoma Bure au Kwa ruzuku ya serikali ,lakn sahv wameweka mpaka ada kabisa ya chuo husika mtoto anapokwenda na Kwa kweli najua asilimia kubwa ya wazazi watapa taabu sanaa kupeleka vijana wao hivyo vyuo vya Kati

Serikali ingewapa tu mkopo wa Moja Kwa Moja hawa wote waliopangiwa vyuo
 
Back
Top Bottom