KERO Kwanini TAMISEMI wanatumia muda mrefu kutoa mrejesho wa majibu ya Uhamisho?

KERO Kwanini TAMISEMI wanatumia muda mrefu kutoa mrejesho wa majibu ya Uhamisho?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari JamiiForums,

Kuna changamoto ya ucheleweshaji wa maombi ya uhamisho kwa watumishi wa umma walio chini ya TAMISEMI.

Niliwasilisha maombi yangu kupitia mfumo tangu mwezi Januari 2026, lakini hadi sasa bado yanaonesha kuwa yapo TAMISEMI bila hatua yoyote kuchukuliwa. Pia hakuna mrejesho wowote unaotolewa kupitia mfumo huo.

Ni vyema utaratibu ukawekwa ambapo, kama ilivyo kwa maombi yanayokataliwa, hata yale yanayokubaliwa mtumishi apewe taarifa na mrejesho kuhusu hatua iliyofikiwa na mahali ambapo maombi yake yamefika.

Mfumo unapaswa kuonesha kila hatua ya mchakato ili kusaidia watumishi kufuatilia maombi yao na kuepuka kusubiri kwa muda mrefu bila majibu. Hali hii pia huathiri morali ya kazi kwa kuwa baadhi ya watumishi huendelea kufanya kazi huku wakiwa na mawazo kuhusu hatima ya uhamisho wao.
 
Back
Top Bottom