A
Anonymous
Guest
Taasisi za Serikali, hasa TANAPA, zinapaswa kuboresha uwajibikaji katika malipo ya watu wanaowafanyia kazi. Inasikitisha kuona mtu anafanya kazi na TANAPA kwa miaka 4–5, lakini anastaafu bila kulipwa deni lake hadi sasa.
Kinachoumiza zaidi ni kuona TANAPA ikiendelea kutumia fedha nyingi katika shughuli za promotion kwa kushirikisha comedians na wanamitandao, huku madeni ya watu waliowahi kutoa huduma kwa taasisi hiyo yakibaki bila kulipwa. Hata kama kiasi cha deni ni kidogo, bado ni haki ya mhusika kulipwa.
TANAPA inapaswa kuweka wazi kama tatizo ni bajeti, utekelezaji wa taratibu za malipo au changamoto nyingine. Pia, kuna madai kwamba baadhi ya malipo hupewa kipaumbele kwa upendeleo, huku wakati mwingine waombaji wakiambiwa nyaraka zao za malipo zimepotea.
Hili si suala la fedha pekee, bali ni suala la haki na heshima kwa watu wanaotoa huduma kwa taasisi za Serikali. Tunawaomba viongozi na wakuu wa vitengo kuhakikisha madeni ya watoa huduma yanalipwa kwa wakati na kwa haki, kabla ya taasisi kutumia fedha katika shughuli nyingine za kujitangaza.
TANAPA, badilikeni na hakikisheni watu wanaowafanyia kazi hawalazimiki kusubiri miaka mingi ili kupata malipo yao.