Kwanini TANESCO isivunjwe?

Kwanini TANESCO isivunjwe?

Moyo na roho yangu vinaniambia kuwa ukosefu wa umeme nchini ni wa kutengenezwa kwa ajili ya neema ya wakubwa. Kuna biashara iliyojificha nyuma ya ukosefu huu wa umeme!

Kuna matangazo ya majenereta nimeona leo kwenye TV. Umeme utarudi mpaka yaishe.
 
Hakuna namna hili Shirika la TANESCO litapata ufanisi bila kuligawanya na kuruhusu wazalishaji wengine wa Nishati ya Umeme kufanya hivyo.
 
Umeme unaozalishwa bongo ni mdogo wakati mahitaji yanazidi kuongezeka hili ndo tatizo. Hata waziri awe nani au bodi ngapi zivunjwe bila vyanzo vipya vya kufufua umeme changamoto ipo pale pale. Wanazunguka tu mbuyu hao wanasiHasa.
Kwa miaka mingi inafahamika kuwa tanzania Kuna maporomoko makubwa ya maji, Kuna upepo, Kuna joto la ardhi, Kuna jua na Kuna gesi na makaa ya mawe yanayoweza kutumika kuzalisha umeme wa kutosha na hata kuuza, lakini tuna watu wa hovyohovyo TU wasiokuwa na Nia njema kwa taifa na watanzania isipokuwa matumbo Yao na wapendwa wao TU.
 
Hakuna haja ya kuivunja TANESCO Ila Kuna haja ya nafasi za Watendaji wakuu wa TANESCO kutangazwa ili the best brains wa apply na kupewa kazi.

Hii teua tengua Ni Kama ku bet
 
Hakuna haja ya kuivunja TANESCO Ila Kuna haja ya nafasi za watendaji wakuu wa TANESCO kutangazwa ili the best brains wa apply na kupewa kazi.
Hii teua tengua Ni Kama ku bet, hujui Kama Ni maharage ya Mbeya au ya Manyara.
Vifo na hasara inayopatikana kwa kukatika umeme nchini ni kubwa sana kuliko mapolomoko ya Hanang. Umeme ukikatika kuna watu wanakufa wengi kwenye matibabu (theater, ICU, watoto njiti, mama kujifungulia gizaji, suction machines kushindwa kufanya kazi, matibabu kuahirishwa, mitandao ya matibabu kushindwa kufanyakazi, watu kupigwa visu gizani mitaani, magari kugongana barabarani taa hazifanyikazi, watu kukwama kwenye lift za majengo, watu kukosa hewa (ventilators), vibaka na wezi kuua watu majumbani kutokana na giza. Hasara ndio usiseme kabisa; vifaa vya majumbani vinaungua vingi sana, vyakula vinaharibika, joto vyumbani ni kali zana (heat stroke), uzalishaji unasimama viwanadani na wafanyabiashara wanaotegemea uwepo wa umeme kuanzia vinyozi, welding, juicers, cold chain, na watu kukosa chakula kutokana na kuburugika kwa kipato na mitaji kufa.

Haya yote yangesababisha kuona na kusikia TANESCO na serikali kububujikwa machozi umeme unapokatika, sio kama hivi tunavyowaona na kuwasikia. Ni kama vile hakuna kinachotokea kwa wananchi na taifa. mtu anasema bwawa linaweza kuzalisha umeme lakini labda February 2024 ndio tunaweza kujaribu kuwasha turbine moja tu kuzalisha umeme. Watu walitegemea kusikia kuwa kutokana na dharura ya kukatika umeme mtambo umewashwa kwa majaribio tangu November 2023.
 
Dear director rea project how to be pre qualified class one in tender documentary to bird all contractors rea? Because they don't know to identify the project strategy management in analysis to identify to present in intaview and question and answers to identify because the cerficate decolation is not results field work. How did they get it 12 months ago the same 365 days they should be to identify if a really electrical engineers around the world wide refer contract agreement written. As follow

1:Financial management and security fund and controller as follow
A. Value of money the running cost budget estimated is available 119.709.450 tsh refer annex 1 budget instructed in analysis as follow
  • Price per km construction line
  • Price to install customers connection
  • Price to install transformers
and pole dressing and installation
B: deducted retention 5% is available amount 5.985.472.5 tsh to reduce our value of money automatically
C: with tax holding 5% is available amount 5.985.472.5 tsh
D. Total deducted is available amount 11.970.945 tsh
E: remaining balance is available received to run the project and to provide all facility personal 95% sub contractors is available amount tsh 107.738.505 -:-dived 12 months Period of agreement the same total days 365 is available amount per month tsh 8.978.208 .75 dived 30 days is available amount per day 299.273.625 tsh how to run this amount and also results to deliver the job and to provide all facility personal 95% and how to recover vat on time? As follow in analysis to identify
  • Transportation cost budget daily each clew 100.000tsh
  • 16.733km scope of work mv line-:- 5 km per liter velocity waves daily at site to distribute our material and our staff is available total lite 3.3466 times 2 our destination daily comsupition is available total lite 6.6932 * times 3500 tsh price labor cost budget is available amount 23.426.2 daily at site
  • 35.03km scope of work lv line -:- dived 5km per liter velocity waves is available 7.006 lite times 2 our destination daily comsupition is available total lite 14.012 times 3500tsh price per liter is available daily cost at site 49.042 to distribute our material and our staff daily at site
*Transportation cost daily at site tsh 100.000 one clew
* Labor cost budget one clew in analysis as follow
20qty labor cost daily at site 200.000tsh
8qty climbing lineman at site 160.000tsh
1qty drive 20.000tsh
1qty foreman at site daily. 30.000tsh
Total amount one clew. 410.000tsh
How to run this amount 299.273.625tsh ? To provide all facility personal and to run
* Transportation cost to follow material warehouse each trip. 300.000tsh
100km from kibaigwa kogwa district to passed chamwino district to arrive dodoma town warehouse -:-dived 5km is available total lite 20 and go and return each trip 40lite times * 3500tsh is available amount 149.000
* Purchased safety gear PPE and insurance reqistation our staff estimated amount 7.000.000tsh
*Purchased working tools at site and damage tools estimated 11.000.000tsh
How to run this amount 299.273.625tsh to recover all facility personal 95% and also to run the project personal and also to deliver the job personal? How did they get it the value of money 119.709.450 to provide all facility and to run the project? Should be to identify the really electrical engineers which used formula the principal method to calculate mathematics and also results the number answers?

Planning material management and program to be pre qualified class one to identify in analysis as follow
A. 360km total from iringa to kibaigwa site -:-80 speed limit velocity waves is available total hours to arrive to deliver our wooden poles the same 4.5 hours each trip
B. 70qty each trip wooden poles 12mt size -:-16.733km scope of work ht line is available 4 trip total* times 70qty = 280qty is available
C 120qty -:-35.03km scope of work lv line is available 3 trip total*times 120qty each trip is available total 360pc wooden poles
D: 16
 
Hakuna umeme hata dar es salaam, viwanda, majumbani na kwenye biashara hakuna umeme, ni shida na hasara ya matrilion inapatikana: Mvua zinanyesha nchi nzima, mabwawa yamejaa na mafuriko kila kona ya nchi. Kwanini umeme hakuna?

Kipindi cha ukame mnasingizia mabwawa yamekauka na mabwawa yakijaa unasingizia miundombinu mibovu na hakuna anaeonekana kusikitishwa kwaajili ya nchi kukosa umeme. Kwa kipindi kirefu tunaambiwa kuwa maji yaliyoingia bwawa la nyerere yanamudu kuwasha mashine ya kufua umeme, baada ya hapo mvua zikaendelea kujaza mito na mabwawa hadi mafuriko kutokea, lakini unamsikia kiongozi anasema labda mwezi February 2024 ndio mashine ya kwanza inaweza kuwashwa ili kufua umeme, maneno na kauli ambayo haionyeshi kuwa kuna udharura wa upatikanaji wa umeme nchini. yaani hakuna userious wowote kwenye kauli wala muonekano wa msemaji, hovyo.

Shida ni nini, muundo wa tanesco, wafanyakazi wa tanesco, viongozi wa tanesco, wizara ya nishati au serikali nzima?
Tanesco ni jina tu la kutupia lawama. Tatizo la Tanesco linaanzia Ikulu, mengine mbwembwe tu
 
Shabiki anatoka na furaha uwanjani akirudi nyumbani anakuta giza totoro umeme hakuna. Kama shida ni nguzo imeanguka ni kwanini fedha iliyotumika kununua magoli ya Yanga na Simba isingepelekwa kwenye ununuzi wa nguzo za umeme ili umeme vuwepo na vijana waendelee kutafuta fedha ya kununua jezi na viingolio? Siasa kila Kona haitusaidii.
 
Umeme kukatika ni hujuma tu kipindi cha magufuli mbn haukatiki kwan alikuwa anautoa chato??na 2025 cjui wanalipi kwa wananchi wanaokosa umeme kila Kona ya nchi.
 
Mimi kwa upande wangu naona tatizo kubwa ni uwajibikaji kwa watendaji wa shirika lakini pia kutakuwa na swala la ten percent kwa baadhi ya watendaji sasa kwa hali hiyo bado wananchi tutateseka tu!
Nini kifanyike itabidi viongozi wawajibishwe lakini pia uzalendo kwa viongozi ikiwa shirika limemshinda mtu ajiuzulu hapo tutaona uzalendo na uwajibikaji wa kweli
 
Hakuna haja ya kuivunja TANESCO Ila Kuna haja ya nafasi za Watendaji wakuu wa TANESCO kutangazwa ili the best brains wa apply na kupewa kazi.

Hii teua tengua Ni Kama ku bet
Hata wakiapply nani atawashotilist na kuwachagua?
 
Mimi kwa upande wangu naona tatizo kubwa ni uwajibikaji kwa watendaji wa shirika lakini pia kutakuwa na swala la ten percent kwa baadhi ya watendaji sasa kwa hali hiyo bado wananchi tutateseka tu!
Nini kifanyike itabidi viongozi wawajibishwe lakini pia uzalendo kwa viongozi ikiwa shirika limemshinda mtu ajiuzulu hapo tutaona uzalendo na uwajibikaji wa kweli
Tatizo kubwa la tanesco na mashirika ya umma yote ni kwamba mishahara ya watumishi wao haitokani na mashirika wanamofanyakazi, watendaji wakuu lazima wawe makada, serikali inataka gawio na michango (maafa, mipira, nk) kutoka mashirika haya, na kuendeshwa kisiasa zaidi, yaani kikurakura. Tanesco Kuna maeneo inashindwa kukusanya madeni kwasababu za kisaisa.
 
Hata wakiapply nani atawashotilist na kuwachagua?
Ichaguliwe international human resources company from Denmark wafanye shortlisting, interview kwa uwazi.
Sasa kweli maharagwe na tanesco? It was just too huge for him.
 
Tatizo kubwa la tanesco na mashirika ya umma yote ni kwamba mishahara ya watumishi wao haitokani na mashirika wanamofanyakazi, watendaji wakuu lazima wawe makada, serikali inataka gawio na michango (maafa, mipira, nk) kutoka mashirika haya, na kuendeshwa kisiasa zaidi, yaani kikurakura. Tanesco Kuna maeneo inashindwa kukusanya madeni kwasababu za kisaisa.
Hapo kwenye makada upo sahihi kabisa

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Ukweli kukosekana kwa umeme ni mateso makali kule vijijini zinakotoka kura zetu. Baada ya umeme kusambazwa vijijini wanavijiji waliachana na mashine zao za dizeli za kusaga nafaka na kukumbatia machine za umeme, sasa hivi weeeee!! wanalala na njaa kwa kukosa huduma hiyo tena. Kila mtu amekasirika hata vijijini na kuna mtu wanamlalamikia kwa mateso hayo.
 
Back
Top Bottom