Kwanini Tanzania haiwezekani kutokea machafuko wala mapinduzi ya kijeshi

Udini hauruhusiwi kwenye mfumo wa kuendesha serikali
 
Mapinduzi au machafuko ni kitu kibaya sana ila mafisadi na pengo aliye nacho na asiyekuwa nacho inadhoofisha umoja wetu. Hali itakuja kuwa mbaya. Tunahitaji uongozi wa kukemea.
 
Credit kwa Ai
 
..hujui historia.

..Nyerere alipinduliwa 1964 akarejeshwa na Waingereza.

..Sultan Jamshid alipinduliwa Zanzibar mwaka 1964.

..hii habari kwamba hakujawahi kutokea mapinduzi au uasi unaitoa wapi.
Mapinduzi hayakutokea 1964, lilikuwa jaribio. Kasome tena historia.
 
Haiwezekani kwa sababu tuna amani...
 
Watz sio aggressive

ni tofauti na Kenya Nigeria na huko kwingineko hawa watu ni watata balaa, hawa ukizingua kinawaka muda wowote

Jamii nyingi ya watz ni watu waraimu sana

Wengi hawataki matata au kusumbuana na mtu

Kuna wakati uwa najiuliza sana hivi ni kweli huu uhuru tuliupambania wenyewe kama tunavyosimuliwa au mkoloni aliamua tu kujiondokea mwenyewe au kizazi kile na hiki cha sasa ni DNA tofauti?
 
Mbona kwenye mambo mengine wako aggressive
Ile kumkamata kibaka kumpiga moto au kumshindilia msumari kichwani mpk hapo wabongo ni makatili
Nchi hii tusiombe kinuke maana kuja kutulia itakuwa shuguli pevu

Ova
 
Naona unajipa matumaini na kujitoa woga.
 
Huenda ni kweli,, mapinduzi au uasi kijeshi ikawa vigumu sana.

Kwangu nina sababu mbili tatu

1: Kwa sasa hakuna siasa za upinzani vyuoni na mashuleni ambako vijana wasomi wangeamshwa, wangechochewa kujua na kudai haki zao kwa nguvu, kama miaka ya 2000 hadi 2010.

2: Idara ya ulinzi na usalama iko makini kupita maelezo kunusa taarifa na hatari inayoweza kuwapata viongozi ama serikali.

3: Hatuna historia au uzoefu wa "kuliamsha" zali kwa mapambano ya kudai haki kwa halaiki labda vikundi ambavyo kuvidhibiti ni rahisi kama Kibiti, Mkuranga, nk
 
Sababu kubwa ziko

Ya kwanza Tanzania haina ukabila nchi zenye ukabila mapinduzi na vita za wenyewe kwa wenyewe rahisi mno

Pili hatuna udini tunaheshimiana na dini sio kigezo cha kutugawa tofauti na nchi Zingine

Tatu waasi hupenda maeneo yenye madini kuyakalia ku finance vita vyao vya uasi sisi maeneo yenye madini tumewapa wawekezaji wakubwa toka nchi zenye zana hatari za kivita kama makampuni makubwa ya ulaya na marekani nk

Nne sisi tuna lugha moja Kiswahili sio vilugha

Tano kuoana na kuolewa na makabika tofauti kumesaidia kujenga mshikamano tofauti na nchi zingine wakomalia kuoa na kuoana kwenye vikabila vyao tu

Sita ajira Jeshini hazina ukabila

Makabila yote wako jeshini na waba vyeo kuanzia chini hadi juu hakuna kabila miliki jeshi au ambalo.laweza tamba kuwa wao ndio wamiliki jeshi
 
Haiwezekani kwa sababu tuna amani...
Amani hapana.
Waliokosa ada vyuoni na shuleni hawana amani.

Waliopotelewa na ndugu au kuuwawa hawana amani.

Waliofiwa na ndugu zao kwa kukosekana huduma na tiba za kiafya
hawana amani.

Waliokosa ajira hawana amani.

Waliobomolewa au kuhamishwa au kufungwa kisiasa hawana amani.

Nakubaliana kuwa Watanzania tumerithi kuridhika, hofu, na unyonge.

Ila bado vita na mapinduzi huenda madhara yake ni makubwa kuliko tulivyo sasa.
 
Omar Al Bashir wa Sudan naye aliunganisha jeshi na serikali lkn unajua kilichompata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…