Kwanini Tanzania haizalishi wakimbizi wengi duniani?

Kwanini Tanzania haizalishi wakimbizi wengi duniani?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kuwa mkimbizi ni kutoka sehemu yako ya asili au unayoishi (comfort zone) kwenda kuishi sehemu nyingine (uncomfort zone) bila hiari yako; umelazima.

Kuna aina mbili kuu za ukimbizi; kutoka sehemu zao za asili kwenda sehemu nyingine ugenini ndani ya nchi, na kutoka sehemu zao za asili kwenda sehemu nyingine ugenini nje ya nchi.

Sababu za ukimbizi ni hizi hapa:

1. Mazingira: Ukame, mafuriko, matetemeko, vimbunga - Kwanini hatuyatoroki mazingira kwenda nchi nyingine?
2. Uchumi: Kuhamia sehemu/nchi kupata kipato zaidi - Kwanini wengi hatuendi nchi za nje kutafuta uchumi?
3. Siasa: Vita, sheria mbaya, utawala mbaya, sera mbaya - Kwanini sisi hatupigani kama nchi zinazotuzunguuka?
4. Uhalifu: Kuhamishwa na wahuni, watu wabaya, kutoroka kukwepa kosa/hukumu. - Hatuna uhaliu wa kutosha kutukimbiza kwanini?
5. Elimu: Kutafuta elimu - Kwanini vyuo vikuu vya nje vina watanzania wachache kuliko nchi nyingine?

Watanzania hawakimbii wengi kutoka sehemu/nchi yao ya asili kwenda sehemu/nchi nyingine kwa sababu yoyote ile kati ya hizi 4 nilizozitaja hapo juu.

Swali; ni nini kinasababisha watanzania hawako wengi sana nchi nyingine za Afrika na nje ya Afrika kama nchi nyingine?
 
Back
Top Bottom