Kwanini Tanzania hatuna misimamo ya wazi UN

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kura ya kuilaani Urusi kwa kitendo chake cha kuyaongezea majimbo ya Donesk, Luhansk, Kherson na Zaporizhia kwenye ramani ya nchi yao imepigwa kwenye Umoja wa Mataifa, huku Tanzania ikiamua kutochagua kulaani wala kupinga Urusi kulaaniwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kutochukua upande (Abstention) kwenye mambo yanayoihusu Urusi. Sisi kama taifa msimamo wetu ni upi?
 
Masikini huwa hana upande..hasa linapokuja suala la kuchagua kati ya mabosi wawili.

Nchi yetu inamefuata moja ya sera ya kipuuzi kuwahi kutokea dunia, hii inachangizwa na uonga, umasikini na ujinga wa viongozi wetu.

Hili litatutesa Maisha yote..NAM ni moja ya sera ya hovyo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kura ya kuilaani Urusi kwa kitendo chake cha kuyaongezea majimbo ya Donesk, Luhansk, Kherson na Zaporizhia kwenye ramani ya nchi yao imepigwa kwenye Umoja wa Mataifa, huku Tanzania ikiamua kutochagua kulaani wala kupinga Urusi kulaaniwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kutochukua upande (Abstention) kwenye mambo yanayoihusu Urusi. Sisi kama taifa msimamo wetu ni upi?
Nchi kama Tz sio lolote pale UN ipige kura wala isipige haiwezi kuathiri lolote katika maamuzi ya hao watu, bora tukae kimya mpaka pale tutakapo kua superpower kama wao.....
 
Hakuna siku nimeudhika kama leo,mambo yapo dhahili nchi moja inapora nchi nyingine kimabavu,eti bado tupo neutral,inaudhi sana.Kwa maana hiyo sisi kipindi cha idd amini tulikuwa tunalilia umoja wa afrika umkanye amini ilikuwa nini na sasa sisi tunafanya nini.anyways ngoja ninyamaze ila nimekwazika sana.Huu upande wa kuitwa NAM haufai,bure kabisa.
 
Sera ya Tanzania ya mambo ya nje ni kutofungamana na upande wowote na hii Sera ipo tangu enzi za Mwalimu, ulale pema kiongozi wetu tunapokwenda kuadhimisha kumbukumbu ya kifo chako bado nchi inakukumbuka kwa mazuri daima.

Wapiganapo tembo ziumiuzo ni nyasi. Kutokuwa na upande ni heri kwa nchi yetu kwa sababu bado in tegemezi kwa wote hivyo tunajiweka katika hatari ya kujitenga zaidi

Mwisho ,katika vita ya Ukraine na urusi hatuna maslahi yoyote yanayohatarisha amani na usalama kiasi cha kwamba tunatakiwa kuchagua upande tutakao kuwa salama
 
NAKAZIA
 
Usitukane mamba kabla hujavuka mto
Nchi yetu ni ombaomba haiwezi kuwa na rafiki au adui wa kudumu
Suala la kutochagua upande ni zaidi ya kuwa sisi ni ombaomba. Tena wenye nguvu ya kiuchumi (ambao tungeenda kwao kuwaomba omba) ndiyo wale ambao wangependa tuwe na msimamo dhidi ya Urusi. Sababu kwa nini hatupigi kura ya kulaani au kusupport ni kwamba vita yao haituhusu sisi.
 
Tunapaswa kujadili kama sera yetu ya mamba nje ni relevant kwa sasa au, hili ndo jambo la kujadili great thinkers.
 
Tujikite kwenye kuwasuluhisha basi
 
Kama huna hela huwezi kuwa jasiri na kama huna ujasiri huwezi kuwa na msimamo. It's that simple.
 
Kura ya kuilaani Urusi kwa kitendo chake cha kuyaongezea majimbo ya Donesk, Luhansk, Kherson na Zaporizhia kwenye ramani ya nchi yao imepigwa kwenye Umoja wa Mataifa, huku Tanzania ikiamua kutochagua kulaani wala kupinga Urusi kulaaniwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kutochukua upande (Abstention) kwenye mambo yanayoihusu Urusi. Sisi kama taifa msimamo wetu ni upi?
Kwani kura za awali za kukemea uvamizi walipiga wapi!!?? Unafahamu msimamo wa nchi yako tangu uhuru !!??
 
Kura ya kuilaani Urusi kwa kitendo chake cha kuyaongezea majimbo ya Donesk, Luhansk, Kherson na Zaporizhia kwenye ramani ya nchi yao imepigwa kwenye Umoja wa Mataifa, huku Tanzania ikiamua kutochagua kulaani wala kupinga Urusi kulaaniwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kutochukua upande (Abstention) kwenye mambo yanayoihusu Urusi. Sisi kama taifa msimamo wetu ni upi?

Hakuna masikini mwenye msimamo boss.
 
Tunajiita nchi isiyofungamana na upande wowote, ambapo kimsingi hilo jina limesababishwa na kuwa kwetu tegemezi kiuchumi, tunaishi kwa kuomba misaada na mikopo toka sehemu zote duniani.
 
Tuna serikali dhaifu isiyokuwa inaelekea wapi zaidi ni kuiba kodi za wananchi
 
Tanzania ni nchi huru na tuna viongozi wenye kufanya maamuzi sahihi Kwa nchi na wananchi wake,na si kufata kina Nani wataka nini ,na huu pia ni ujasiri wa kutoendeshwa au kuchaguliwa upande

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tunajiita nchi isiyofungamana na upande wowote, ambapo kimsingi hilo jina limesababishwa na kuwa kwetu tegemezi kiuchumi, tunaishi kwa kuomba misaada na mikopo toka sehemu zote duniani.
Mwendo wa kuembeza bakuri tu..kesho tupo Ukraine kesho kutwa tupo Urusi..[emoji28][emoji28] hatutaki kuwaudhi mabosi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom