Kwanini Tanzania hatuna Senate bali tuna National Assembly pekee yake?

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Nimeona Kenya wana mabunge mawili, National assembly na Senate?

Kwanini Tanzania hatuna hii senate? Je, majukumu ya senate kwa Tanzania yanafanywa na nani?

Kuuliza sio ujinga.
 
Nimeona kenya wana mabunge mawili, National assembly na Senate?

Kwanini tanzania hatuna hii senate? Je majukumu ya senate kwa Tanzania yanafanywa na nani?

Kuuliza sio ujinga
kuuliza kwa namna hii ni ujinga na hata niseme ni upuuzi.Unadhani kila kinachofanywa kenya ni lazima kifanywe na Tanzania ? Kuna siku utauliza kwa nini Tanzania hatuna Ruto.
Watu kama nyinyi mkiambiwa mkiona kama vipi mhamie Burundi mnaona mmetukanwa,
 
Mbona tena matusi.
 
Nimeona kenya wana mabunge mawili, National assembly na Senate?

Kwanini tanzania hatuna hii senate? Je majukumu ya senate kwa Tanzania yanafanywa na nani?

Kuuliza sio ujinga
usione wakenya wanalalamika sana ile nchi inapigwa mbaya mbovu kwa mifumo mibovu ya kutengeneza payroll kubwa ambayo haina msingi wowote hasa swali lako lingejenga hoja ya kwanini mabunge mawili kwa kenya? ufahamu mfumo mzima wa county kenya wanaoutumia governors na seneta ....ya kwetu ni mazito sana mpaka uende uliza ya watu au shida ni nini?
 
Nimeona kenya wana mabunge mawili, National assembly na Senate?

Kwanini tanzania hatuna hii senate? Je majukumu ya senate kwa Tanzania yanafanywa na nani?

Kuuliza sio ujinga
Swali fikirishi ili uitwe kibogoyo unatakiwa uwe na sifa zipi, kama ni mjasiliamali nitakupa zawadi ya namna ya kufanya vizuri kwenye biashara yako
 
Senate ipo kwaajili ya kusimamia Counties na mawaziri. Kwa mfano husimamia impeachment ya magavana Mawaziri hufika mbele ya seneti kujibu maswali mbali mbali.
 
Wakati mwingine watanzania akili zetu hazieleweki, kila siku mnalalamika humu gharama za kuendesha hilo bunge na Serikali, wengine mmefika mbali kwamba wakuu wa wilaya wafutwe na nafasi ya Makamu wa Rais iondolewe ili wananchi wapate nafuu leo hii unakuja na hoja ya seneti, hivi Kenya imewaloga? Ni lazima kila wanachofanya wao na Tanzania tufanye? Acheni shobo na hao wakenya au hamieni huko
 
Jiulize kwanini Kenya hawana Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa wilaya.

Simple tu wana senate kwasababu ya mfumo wa Majimbo, kama ilivyo USA na sehemu nyingi zenye mfumo wa majimbo.

Pia Soma Kidogo Hapa Ufungue akili yako.

Tofauti kuu kati ya Bunge la Seneti na Bunge la Kawaida (ambalo mara nyingi hurejelea Bunge la Wawakilishi au Bunge la Taifa) inatokana na muundo wa mabunge ya nchi zinazofuata mfumo wa mabunge mawili (bicameral system). Hapa kuna tofauti za msingi:

1. Muundo:
- Bunge la Seneti: Linaundwa na maseneta au wawakilishi wa majimbo/maeneo, mara nyingi likiwa na idadi ndogo ya wajumbe ikilinganishwa na Bunge la Kawaida.
- Bunge la Kawaida: Linajumuisha wawakilishi wa wananchi moja kwa moja kutoka maeneo mbalimbali ya uchaguzi, na lina idadi kubwa ya wajumbe.

2. Majukumu:
- Bunge la Seneti: Kazi yake kuu ni kuwakilisha maslahi ya majimbo au maeneo maalum ndani ya nchi. Pia linahusika na masuala ya kikatiba, mabadiliko ya sheria, na wakati mwingine kuchambua sheria zinazohusu ugatuzi wa madaraka au ushirikiano kati ya serikali kuu na zile za mitaa.
- Bunge la Kawaida: Linashughulikia masuala yote ya kitaifa, ikiwemo kupitisha bajeti, kutunga sheria za kitaifa, na kuangalia utendaji wa serikali kuu.

3. Uwakilishi:
- Bunge la Seneti: Maseneta wanawakilisha majimbo, maeneo au wilaya, si tu idadi ya watu. Hii inamaanisha kila jimbo au eneo linapata mwakilishi mmoja au wachache, bila kujali ukubwa wake wa watu.
- Bunge la Kawaida: Wajumbe wa Bunge la Kawaida wanachaguliwa moja kwa moja na wananchi kutoka maeneo ya uchaguzi, ambayo yanatokana na idadi ya watu.

4. Mchakato wa Sheria:
- Bunge la Seneti: Kwa kawaida linatoa mapitio ya pili ya sheria, yaani, baada ya kupitishwa na Bunge la Kawaida, sheria nyingi hupitiwa tena na Seneti kabla ya kuidhinishwa kikamilifu.
- Bunge la Kawaida: Linaanza na kuandaa miswada ya sheria na hujadili kwa kina kabla ya kuipitisha ili ipelekwe Seneti (ikiwa ni sehemu ya mfumo wa mabunge mawili).

5. Nguvu
- Bunge la Seneti: Mara nyingi huwa na nguvu ndogo kisheria ikilinganishwa na Bunge la Kawaida, ingawa inaweza kuwa na nguvu zaidi katika masuala ya kikatiba au ugatuzi.
- Bunge la Kawaida: Lina nguvu kubwa zaidi, hasa katika masuala ya bajeti na utendaji wa serikali.

Kwa kifupi, Bunge la Seneti linazingatia zaidi uwakilishi wa majimbo au maeneo, wakati Bunge la Kawaida linaangalia maslahi ya wananchi moja kwa moja kupitia wawakilishi waliochaguliwa.
 
mifumo yetu sawa na burundiii ...tuko vizurii
 
Thanks kwa maelezo mazuri
 
Nimeona Kenya wana mabunge mawili, National assembly na Senate?

Kwanini Tanzania hatuna hii senate? Je majukumu ya senate kwa Tanzania yanafanywa na nani?

Kuuliza sio ujinga
Nchi zote zenye Senate ni mbwembwe tu. Uingereza wana "House of Lords" ambayo msingi wake ni kudumisha utamaduni wao wa Kikabaila na ndio maana kuingia humo ni kwa kurithi.
 
Back
Top Bottom