Kwanini Tanzania hatutengenezi magari?

Ni kweli kabisa mkuu, tatizo letu hua tunakosa uthubutu katika kuwekeza. kama raisi kathubutu kutumia trilioni mbili kasoro kwenye kipande cha Dar Moro nadhani pia itakua vyema kama taifa tukaingia ubia na kampuni yeyote tukaanza uzalishaji mkubwa.
Tunaweza kuanzisha kiwanda cha magari ya 650cc baadaye tukaja kwenye magari makubwa zaidi. Kinachotakiwa ni commitment tu. kama ni mtaji hisa tutanunua hata kama hisa moja itakua ni 50,000 tutajichanga hivyohivyo.
 
Gari mpya 0 km ni watu wachache sana wanaweza mudu.Hapa mbeya sijaona gari zaidi ya 10 new models za watu binafsi.
kuna watu wengi wanaendesha 0 km, ila siwezi kuwataja sababu ni kinyume na maadili kutoa taarifa binafsi za watu. lakini tukiamua tunaweza kutengeneza gari ndogo classic kwa bei ya milioni 30.
 
Inawezekana kabisa na focus iwe kwa mauzo ya ndani ya nchi tu kwa kuanzia na badae target kuipeleka East Africa kulingana na ubora wa magari husika.
 
Jiulize ni nani anatakiwa kujenga hicho kiwanda,na yeye anapata ushirikiano upi?
 
Mpk tuwe na kundi kubwa la middle incone earners ndipo tutaweza kupata wananchi wengi watakao afford hizo gari tunazozitengeneza.
 
Nyumbu hujaziona gari zao tanzania tunatengeneza magari

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyumbu uwezo wao ni mdogo mkuu, angalia TATA walizindua kiwanda cha kuassemble nagari yao sijui ni nini kimezuia...wakati huohuo Rwanda inaassemble gari za Volkswagen.
How comes nchi ndogo kama Rwanda wanaassemble gari za kampuni kubwa kama Volkswagen lakini sisi tunashindwa kukomaa ata na TATA ambaye gari zake ni cheap.
 
Agizeni kutoka Rwanda Mkuu, Tanzania shida ni CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…