Kwanini Tanzania tuliamua kumtumia twiga mnyama legelege kwenye nembo ya taifa?

Hoja fikirishi. Ni kama ina karibia ukweli.

Lakini Twiga japo anaonekana mrembomrembo miongoni mwa wanyama mwitu sio mlegevu kama alivyoelezwa.

Simba humudu wanyama wengi kweli, lakini kwa Twiga hammudu kirahisi.

Zipo video Simba anauwawa na Twiga. Mateke miguu ya nyuma na mbele huyatumia vizuri sana.

Ule urefu wake huonekana kama mlemavu akikimbia, lakini ndio mbio zenyewe.

Haonekani kuwa mnyama mbabe lakini nae pia anajua kujihami.

Tukiacha hayo ya Twiga. Ni kweli waTanzaia yafaa tujitafakari, tujipange kurukia ngazi ya juu ya maendeleo na ustawi.

Ulegelege, kutojali, kupuizia, kuridhika kwa vitu vidogo, kufikiria zaidi ya leo tu, uoga nk ni vitu tunavyo sana.

Tubadilike sasa.
 
Tanzania siyo legelege kama unvyoona wewe labda wewe mtoa mada ndiyo legelege
 
Haaaaahaaa
 
Tanzania siyo legelege kama unvyoona wewe labda wewe mtoa mada ndiyo legelege
Tanzania ni imara kwenye nini? Kama ni michezo, Tanzania ni mdebwedo ile mbaya, kama ndio kwenye akili, Watanzania wanaamini maji yanaweza kugeuza risasi iwe maji, sasa wamekuja na mpya, wanaamini eti maji yanayoitwa maji ya upako yanawez kutatua shida zako zote ikiwa ni pamoja na kukupa hela za miujiza
 
Tulizingua sana. Tumekaa kitwigatwiga tu. Nashauri tunapochagua ndege wa taifa tusikosee tena. Sagittarius Serpentarius atatufaa.
 
Mkuu hoja yako ina ukweli kwa asilimia kubwa sana

Tuna safari ndefu km taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…