Kwanini tarehe ya Pasaka hubadilika?

Mkuu Kwani Nini Maana ya Iddi?
Iddi maana yake ni Siku kuu!..

Iddi maaana yake ni sikukuu
Idd alfitr ni Sikukuu ya Kufungulia baada ya kufunga ni kama Surah ilivyosema..

maana ya Iddi katika biblia..


HOSEA 12:9


Kwenye Quran hapo Imeandikwa baada ya Kuamaliza Kufunga washerekee Baada ya Kumtukuza Allah kwa Kuwavusha salama..

Ngoja nikupe Elimu kuhusu Vita ya Badr..

Vita vya Badri. - Vilikuwa ndio vita vya kwanza vya jihad vilivyopiganwa siku ya Ijumaa mwezi 17 Ramadhani, mwaka wa 2 A.H (624 A.D) katika bonde la Badri...

Wakati Suratul Al Baqara imeshuka 622 AD in Medina mwaka ule ule wa siku za Hijria..

Sasa agizo lililotoka Mwaka 622 unasemaje kuwa Limetokana na Shughuli iliyofanyika Mwaka 624??

Huwa si Relay kwenye Mitandao huwa narekay kwenye Kusoma na Kujua Ukweli..
Mitandao kila mmoja anauwezo wa kuandika atakacho
 
Big up sana
 
Mimi nimeshindwa kusoma hii story yako, umeandika mengi mno. nipigie simu nikufundishe jinsi ya kuandika story, hii umeandika kama Biblia.
Kama umeshindwa tu kusoma hii wewe tena ndio umfundishe kuandika?
 
Kwenye andiko uliloweka hakukua na neno sherehe, bali kumtukuza Mungu. Sasa kumtukuza Mungu ni jambo la kila siku, haimaanishi kusherehekea.

Mimi nimerejea mitandaoni maana kwenye quran haipo, sawq tu ilivyo pasaka. Kwa hiyo unapouliza chanzo cha Easter ni sawa na kuuliza chanzo cha idd el fitr..

All in all, hakuna madhara kwa watu wanaoamini jambo fulani kufanya jambo lao hata kama limepotoshwa. Kinachosikifisha ni mtu asiyehusika na jambo hilo kuona ukengeufu wa jambo na kujaribu kuliboresha ilhali kikiboreka pia halimfaidishi chochote. Mfano, Pasaka (easter) ikionekana ni sherehe ya kipagani, mleta mada anapata faida gani?
 
Sasa sisi waafrika mbn tunawaingilia mambo yao ?
Hao Wayahudi walitutangulia tu kuzijua kanuni za Asili zinazoendesha ulimwengu( Natural law ) , halafu wakajitangaza kuwa wao ni wa juu , nguvu ya duniani.
Ila Mwezi ni mfano ambao huwa unasimama kueleza Roho .
Sira 43:7 inasema "Kutoka Kwa Mwezi ni dalili ya sikukuu" . Lakini pia hata katika Astrology Mwezi huwa unasimama kuwakilisha Roho .
Sasa Kuna watu Roho zao zimepewa mission ya kutekeleza kanuni ya Asili ( natural law ) duniani na Mungu ndo hao akina Yesu Kristo .
 
Tarehe 14 ya mwezi wa Nissani Mkuu kalenda ya kiyahudi..

Ushahidi kuhusu Council of Naecea Tafuta Decree zote za Council of Naecea soma Decree ya Pili..
View attachment 2950561

View attachment 2950560
Unaelewa maana ya kubadili kweli ?.

Hiyo mbona ilikuwepo. (Na ilianza Tangu ufufuko wa Yesu, kutukomboa toka katika utumwa wa dhambi). Kama ni kubadili aliyebadili ni kristo mwenyewe na akasisitiza kabisa "fanyeni ivi kwa ukumbusho wangu".

Kumbuka hapa mimi sizungumzii passover ya kumbukumbu ya utumwani misri.

Kilichofanyika kwenye huo mtaguso wa nicea ni kuseti tarehe za pasaka ili kuondoa mikanganyiko ya tarehe ziliokuwepo sababu ya mikanganyiko ya calender ili pasaka isherhekewe sawa duniani kote.

..Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, ni Pasaka ya BWANA. Na siku ya kumi na tano ya mwezi huohuo ni
sikukuu ya BWANA, ndiyo siku ya mikate isiyotiwa chachu. (Walawi 23:5)..”.

Hivyo Pasaka ni tarehe 15 ya mwezi wa Kwanza. Lakini Biblia pia inautaja mwezi wa kwanza kwa jina la Nisan (Esta 3:7, Nehemia 2:1).

Yesu alisulubiwa mwaka ambao Ijumaa iliitangulia sikukuu ya Pasaka kwa siku moja (Yohana 18: 28, Marko 15:42-43). Hivyo tarehe ya Yesu kusulubiwa ni Ijumaa, Nisan
14. Siku moja kabla ya Nisan 15. Siku moja kabla ya Mwezi-Mkubwa.

Baada ya Yesu, Wakristo wengi Pasaka waliiadhimisha Jumapili, lakini utata ulijitokeza kuhusu tarehe ya kuiweka hiyo Jumapili ya Pasaka. Ilifika wakati jimbo moja la Wakristo linaadhimisha siku tofauti na jingine na kwa njia wanayoijua wao.

Utata huu uliondolewa kule Nicaea mwaka 325 ambapo Kanisa Katoliki lilipoamua kuwa, tarehe ya Pasaka iwe moja tu duniani kote, yaani iwe ni Jumapili inayokuja baada ya Mwezi-Mkubwa (Full Moon) yaani baada ya Machi 21 (Equinox).

Baada ya uamuzi huu, wataalamu walipania kuunda chati maalum zenye tarehe za Mwezi-Mkubwa zitazokasaidia kuitambua tarehe ya Pasaka kwa mwaka wowote.

Na formula za kukokotoa tarehe za pasaka ni nyingi tu, na moja ya formula ni hii hapa.

(1) : a=MWAKA mod 19;
(2) : b=MWAKA \ 100;
(3) : c=MWAKA mod 100;
(4) : d=b \ 4;
(5) : e=b mod 4;
(6) : f=c \ 4;
(7) : g=c mod 4;
(8) : h=(b + 8)\25;
(9) : i=(b – h + 1)\3;
(10) : j=(19xa + b – d – i + 15) mod 30;
(11) : k=(32 + 2xe + 2xf – j – g) mod 7;
(12) : m=(a + 11xj + 22xk) \ 451;
(13) : n=j + k – 7xm + 114;
(14) : Tarehe=(n mod 31) + 1
(15) : Mwezi =n\31;

Penye neno MWAKA, andika mwaka unaotafutak ujua tarehe yake ya Pasaka.

Panapotokea alama (\) ni kugawanya ambako hata kama jibu litaleta desimali, basi hiyo desimali unatakiwa kuachana nayo ili jibu libaki namban zima.

Penye alama (x) hiyo ni ya kuzidisha.
 
Ok Sasa Mkuu Nisikilize hapa chini nikuchambulie Hilo andiko Vizuri..

nilikupa Andiko la Al-Baqarah 185

شَهْرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِىٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلْقُرْءَانُ هُدًۭى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٍۢ مِّنَ ٱلْهُدَىٰ وَٱلْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ ٱلشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍۢ فَعِدَّةٌۭ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ بِكُمُ ٱلْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ ٱلْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا۟ ٱلْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا۟ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Inatamkwa Hivi..

Shahru ramadhana allathee onzila feehi alquranu hudan lilnnasi wabayyinatin mina alhuda waalfurqani faman shahida minkumu alshshahra falyasumhu waman kana mareedan aw AAala safarin faAAiddatun min ayyamin okhara yureedu Allahu bikumu alyusra wala yureedu bikumu alAAusra walitukmiloo aliiddata walitukabbiroo Allaha AAala ma hadakum walaAAallakum tashkuroona

Sasa mkuu hilo ni neno "وَلِتُكْمِلُوا۟ ٱلْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا۟ ٱللَّهَ"

Neno Al-Iddata (Iddi) unajua maana yake??
Maana imesema baada ya kufunga itakuwa Al Iddata (Iddi)..

Imeamriwa kwa aya Hiyo baada ga kufunga Itakuwa ni Al iddata yaani Sherehe ya iddi na kumtukuza Mungu..


Nilikuwekea Aya kwa Kiarabu mwanzoni nikaamini utasoma Herufi na utaona Neno Al Iddata..

Wengi wanashindwa kutafasiri hizi Lugha Kiarabu na Kiebrania..
 
Nilitaka kumjibu hivyo mkuu Ila kwa kuwa umejibu sawa!
Yesu kama wayahudi wengine wote, ilimpasa kufuata mila na desturi za kiyahudi alizozikuta tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake, na ndio maana nae pia alibatizwa kama wayahudi wengine tu.

Swali je aliendelea kufanya hiyo pasaover ya kiyahudi baada ya kifo na ufufuko wake ? Kama hakuemdelea kufanya ivyo kwanini ? Na vipi kuhusu wanafunzi wake baada ya yesu kupaa mbinguni waliendela kusherekea izo passover za kiyahudi kukumbuka kukombolewa toka utumwani misri ? Kama jibu ni hapana kwanini ?
 
Naomba uthibitisho mkuu!
Nipo Uthibitisho huo!
Kwani, alitwaa mkate akashukuru, akaumega, akawapa wafuasi wake, akisema, huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho wanu. Na hivi hivi baada ya kula akakiitwaa kikombe akisema, kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo kwaukumbusho wangu. (1Kor.11:23-25) pia rej.Mt.26:26-28;Mk.14:22-25;Lk.22:19-20.

(rejea kol 2:16-17)
Nanukuu
“16Kwa hiyo mtu asiwahukumu ninyi kuhusu vyakula au vinywaji, au kuhusu kuadhimisha sikukuu za dini, au Sikukuu za Mwandamo wa mwezi au Siku ya Sabato. 17Hizi zilikuwa kivuli cha mambo ambayo yangekuja, lakini ile iliyo halisi imo ndani ya Kristo.”
 
Umemaliza kila kitu Mkuu
 
Hii elimu umenipa Mkuu
 
Mkuu Nimependa Sana Majibu yako!
Nimefurahi Kuona Ulivyo well Informed Kuhusu Pasaka Kwakweli Ni faraja sana..

Sasa Tuanze na Council of Naecea..

Neno Easter halikuwahi kuwepo hapo kabla ya kikao Hicho kama Tamaduni ya Kikristo..(Christian Tradition)

Neno Easter limetokana na

Je Pasaka ilifutika baada ya kifo cha Yesu???
Hapana..

Bado pasaka iliendelea kutunzwa na Kuheshimiwa na Waisrael na hata Wanafunzi wa Yesu..

Matendo ya Mitume 12:3-5

"Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa.

Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu."

So Pasaka ilianza kubadilka kuwa Ni Mlengo wa Kifo cha Yesu kwenye Karne ya 2 Yaanj miaka ya 300s na hasa kwemye Council of naecea..

Mimi ni mwenyeji sana wa Kusoma vitabu vya Churches Father akiwemo Easebian (Mwanahistoria wa Dini na Churche father) na hata churches father wengine ila hakuna hata mahali Moja walipowahi kuandika Uwepo wa Paska kabla ya Kikao..

Labda kama utanionyesha..
 
Jibu la swali hilo ni ndiyo mkuu..
Na unataka yesu aendelee Kufanya pasaka wakati alifariki tarehe 15 Nissan siku ya Pasaka?
Kwahiyo alikaa miaka zaidi ya mmoja baada ya kufufuka??
Kama unazungumzia Wanafunzi wake, Yes walie delea Kudumisha Pasaka Kama ilivyokuwa Desturi ya wayahudi..
Soma matendo..
 
Mathayo 26..
Sio Uthibitisho wa pasaka mpya ila..
Ni contract ya yesu kuwaasa Waendelee kufanya Pasaka kwa Ukumbusho wa yeye..

Kumbuka Wanafunzi wa yesu sio wote walikuwa Wayahudi hivyo Mila zingine zilikuwa kwao ni ngeni na aliwafundisha Yeye..

Kuna wengine walikuwa wakananayo hivyo swala la Pasaka kwao likuwa jipya na ndo maana hata..
Maelekezo ya kuandaa Pasaka aliwatuma watu wakaandae na sio wanafunzi wake..
Kwahyi baada ya kufundishwa jinsi ya kuandaa na kufanya ndyo wanapewa maagizo ya kuendelea kufanya..

Je waliendelea kufanya au walifanya vinginevyo...
Ndyo waliendelea kufanya Pasaka hiyo na Hawakuihalifu
 
Kwa bahati nzuri waliendelea kuumega mkate kila wakutanapo, wakimkumbuka yeye na siyo kwenye pasaka moja tu.
 
Kwa bahati nzuri waliendelea kuumega mkate kila wakutanapo, wakimkumbuka yeye na siyo kwenye pasaka moja tu.
Wanafunzi wa Yesu karibu wote wamekufa wakiwa wanafanya pasaka ya Mikate isiyochachwa wewe niambie ni mwanafunzi gani ambaye alifanya pasaka tofauti na hiyo nyakati hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…