Kwanini tarehe ya Pasaka hubadilika?

Mkuu kuna shida gani au kuna dhambi gani na neno "easter", inshu yako ni neno "easter au tukio linaloadhimishwa na kukumbukwa siku hiyo ya easter ?, shida au point yako hasa ni ipi kuhusu neno easter ?.

Kama ni ishu ya hilo neno easter kutokuwepo kabla ya mtaguso wa nicea. tatizo ni nini au dhambi yao hasa ni ipi fafanua?.

Afu nikuulize utamadunisho ni kosa au ni dhambi au Mungu alikataza utamadunisho ?.

Kuhusu mtaguso wa kwanza naecea 325 ni kwamba mtaguso ulikuwa na ajenda kama tatu, kupinga mafundisho ya ARIUS kuhusu umwana wa Mungu, kutunga kanuni fupi ya imani na ajenda ingine ilikuwa ni tarehe ya kuadhimisha pasaka (na sio kuanzisha pasaka).

Mtaguso uliamua utaratibu wa kupata tarehe ya kuadhimisha Pasaka kila mwaka (yaani kabla au baada kidogo ya ekwinoksi ya mwezi Machi). Tarehe hiyo iliwekwa kuwajibu wazushi fulani, wazushi waliojulikana kwa jina la Wakwatodesimani).

Sasa shida/tatizo lako wewe na huo mtaguso wa nicea ni ipi ?.
 
Point ipo hapo uliposema "kama ilivyokuwa desturi ya wayahudi". Hivyo ushiriki wa hao wanafunzi wa Yesu wenye uraia wa kiyahudi kwenye izo passover za kiyahudi na sherehe na tamaduni zao zingine zote ilikuwa ni kwa sababu mbili tu, mosi woga na hofu waliokuwanayo wanafunzi kuhusu habari za ufufuko wa yesu, pili kwa ajili ya wao kukamilisha tu taratibu na tamaduni za kiyahudi basi (matendo ya mitume sura 12 utaona ushiriki wao), maana iwapo wasingefanya ivyo au wangefanya tofauti na hizo taratibu za kiyahudi wangekabiliwa na adhabu kali sana, kumbuka Yesu hakuwa anatakiwa kabisa na wayahudi hata mpaka kumuua.

Umenukuu mistari michache tuu ila kupata dhima nzima na mantiki ya icho kitabu kasome kitabu chote utapata context halisi sana.

kiufupi, kwa sababu ya uzito na woga wa kuachana na pasaka walioizoea passover wafuasi wa yesu walikuwa njia panda na hivyo wakawa wanahuduria pasaka ya kiyahudi na wayahudi wote (rejea nukuu yako ya matendo 12: 3-5 hapo juu) lakini SIKU YA BWANA (hiyo ndio pasaka ndogo wakristo tunaita jumapili) ilipofika wakawa wanajikusanya peke yao kimaficho ili kusali, kusoma maandishi yao na kumega mkate (rejea matendo 20:7)

Nanukuu โ€œ7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. Paulo akaongea na watu, naye kwa kuwa alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliendelea kuongea mpaka usiku wa mananeโ€

Ndugu yangu, kitendo cha wafuasi wa yesu kusali huku na huko, kama kufanya passover, sabato na tamaduni zingine za kiyahudi na wayahudi na then jumapili wanafanya mambo yao peke yao, hakikuchkua muda mrefu kubainika.

Wakuu wa mayahudi walingโ€™amua kwamba kuna wayahudi wenye tabia za pande mbili. Wanajiunga na ibada za kiyahudi na kishapo siku ya pili yake wanasali peke yao huku wakimkiri kuwa yesu kristo ni Mwana wa Mungu na mkombozi wa Wanadamu. (Kosa kubwa sana hilo walikuwa wanafanya, kumbuka huyo Yesu hawataki na walimuua na kuzuia kabisa kabisa habari na mambo yake)

Ndipo walipotunga ombi la kumi na mbili na kulitia kati ya sala yao ya Maombi kumi na manne(tefillah), Sala iliyokuwa ikisaliwa na wayahudi wote kila pasaka na sabato katika mwendo wao wa ibada zao.

ombi la kumi na mbili halikuwa ombi bali sala ya kuwalaani Waasi wa dini wakiwamo ndani yake wale wanafunzi wa yesu na wakristo. ombi hilo lilisema โ€œkusiwe na tumaini kwa waasi wa dini na uungโ€™oe kwa haraka kwa waasi wenye kiburi, wanazareni (wayahudi wakristo, wakiwemp wale wanafunzi wa Yesu), na โ€˜minimโ€™ (Wayahudi wazushi) wafe mara moja, wafutwe kwenye kitabu cha uzima na wasiolozeshwe pamoja na wenye hakiโ€ mwisho wa ombi hili kama ilivo kawaida kwa kila ombi, Watu waliokusanyika kwenye ibada iliwapasa kuitikia โ€œUtukuzwe wewe, Bwana unayenyenyekesha kiburiโ€
 
Mathayo 26..
Sio Uthibitisho wa pasaka mpya ila..
Ni contract ya yesu kuwaasa Waendelee kufanya Pasaka kwa Ukumbusho wa yeye
Hapa unajichanganya mkuu, labda ufafanuzi unahutajika. Sababu kwa dhima na mantiki nzima ya sikukuu ya kiyahudi passover, ni kivipi ifanyike kwa ukumbusho wa Yesu ?.

Pamoja na mambo mengine, Kikubwa kwenye pasaover ilikuwa ni ukumbusho wa kutolewa misri utumwani, sasa unaposema yesu aliwaagiza wanafunzi waendelee kufanya hiyohiyo pasaover ya kiyahudi ila kwa ukumbusho wake HOW ?, kukumbuka nini ?.
 
Wanafunzi wa Yesu karibu wote wamekufa wakiwa wanafanya pasaka ya Mikate isiyochachwa wewe niambie ni mwanafunzi gani ambaye alifanya pasaka tofauti na hiyo nyakati hizo
View attachment 2950736
Hiyo matendo 12:2-5 ulioinukuu hapo haisemi na wala haina ushahidi kuwa hao wanafunzi walikufa wakiwa wanafanya sikukuu ya mikate isiotiwa chache.

Kilichoandikwa hapo ni kuwa huo ukamataji na uwekwaji gerezani wa wanafunzi ulifanyika siku ya mikate isiotiwa chachu (na sio wakiwa wanafanya pasaka au kuadhimisha hiyo sikukuu ya mikate isiotiwa chachu), Soma vizuri kwa utulivu.
 
Wekaya kifooo
 
Mtaguso wa Nicea ndo umeharibu sana Dini ya Kikristu..kwahyo Mtaguso huo naulaaani sana Maisha yote..
Nipe kosa alilofanya arius..
Bila kuegemea upande wowote
 
Wayahudi wanafanya mpaka Leo wao wanakumbuka Nini???
 
Wayahudi wanafanya mpaka Leo wao wanakumbuka Nini???
Wanakumbuka
Mosi, Kukumbuka kitendo cha kuondolewa kutoka utumwani Misri.

pili, kumbukumbu ya kuwa ni alama kwamba Mungu aliliteua taifa la Isreli kuwa mali yake.

Kadiri ya kitabu cha hesabu sura ya 28: 16-17. na Kumb 16: 1-8. โ€œUtunze mwezi wa Abibu,ukamfanyie Pasaka Bwana ,Mungu wako nawe umchinjie pasaka Bwana Mungu wako katika kundi la kondoo na la Ngโ€™ombe , mahali atakapo chagua Bwana apakalishe jina lake. Usimle pamoja na mikate isiyotiwa chachu nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka katika nchi ya Misri kwa haraka ili upate kukumbuka."

Na mpaka leo wanamsubiri masiha/mkombozi kadiri ya agano la kale, na vitabu vyao vitakatifu biblia yao ni vitabu agano la kale tu basi.

Sasa unaposhikilia Yesu aliagiza waendelee kufanya pasaka ileile ya kiyahudi kwa ukumbusho wake inaleta ukakasi kidogo mkuu.
 
Kitu ambacho Nafurahi Ni kuwa Uko Well Informed kuhusu Dini!..

Nimewahi kuwa Judaism..
Na pia kuwa Muslim na pia kuwa xtian..
Na unaonekana unajua vingi..

Kuhusu Accusation ya wayahudi...

Nina Maswali machache kidogo..
Unamfahamu Joseph Smith??
Unafahamu kuhusu Mormonism?

Je Unawakubali Wamormon?
KAma ndiyo, kwanini?
Kama hapana kwanini?
Unakubali Biblia ya Wamormon?

vipi unamkubali Mtume muhaamedi?
kwanini?
unaikubali na kuiamini Quran?
kwanini?

Ukijibu hayo maswali kuna Follow up Questions
 
Mtaguso wa Nicea ndo umeharibu sana Dini ya Kikristu..kwahyo Mtaguso huo naulaaani sana Maisha yote..
Nipe kosa alilofanya arius..
Bila kuegemea upande wowote
Mkuu zilikuwa ni ishu za Umungu wa Yesu. Na ndio sababu yake zikakaziwa baadhi ya doctrine zihusuzo umungu na ubinadamu wa Yesu kwenye huo mtaguso wa nicea. Mambo mengine yanaumiza sana kichwa mkuu๐Ÿ˜. Cha msingi tusali na kutenda mema tuingie mbinguni, kweli zingine tutazikuta hukohuko mbele ya safari๐Ÿ˜๐Ÿ˜€
 
Na hichi ndo nilikuwa natka tudiscuss lakini Wengi hawawezi kuongelea swala hilo bila Kutake side..
Ni swala linaloumiza kichwa mkuu kama utakuwa unalinda Side unayoamini ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Na hichi ndo nilikuwa natka tudiscuss lakini Wengi hawawezi kuongelea swala hilo bila Kutake side..
Ni swala linaloumiza kichwa mkuu kama utakuwa unalinda Side unayoamini ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
Sio kulinda side mkuu, mimi ni RC niliepitia seminari kidogo sana, mbona mara nyingi tu huwa nakiri huku RC pia tunakasoro zetu kadhaa , ila suala la utatu mtakatifu kujadilika kiakili zetu izi na kutaka ulielewe kwa facts 100% bila tongotongo zozote hasa kwa kutumia bible as the only source ni gumu sana mzee.
 
Vizuri sana hapo umenena Vizuri!
Mseminary! na kiukweli you ade well informed!
mimi nilipitia theolojia and ex-Pastor..
 
pasaka ni suala la wayahudi kutoka utumwani misri au ni suala la ukatoliki?
hii ya sasa ni ya wakatolik na ndo wanaiita EASTER
hii hapa ni tofauti kwa jinsi inavyosherehekewa na ile ya wayahudi, jinsi walivyoelekezwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ