Kwa wale wapenzi wa Soka la Tanzania watakumbuka jinsi Vilabu chini ya FAT vilivyokuwa vinacheza mechi za kujipima nguvu kwa timu au vilabu kutoka nje ya nchi kwa mialiko ya Chama cha Soka FAT. Sijui kwanini kwa sasa utaratibu huo chini ya TFF haupo na pia vilabu vyetu pia havifanyi hivyo au kwenda kucheza mechi za kujipima nguvu nje ya nchi mara kwa mara nchi za jirani tu kama Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia n.k.Mechi za kimataifa ni muhimu kuliko eti unacheza na Mikumi united au Rwanga united ya lindi.Viongozi wa TFF.na Vilabu badilikeni mpira ni Sayansi.