Habari za Wakati huu wana na ndugu wa Jamii Forums
Nimekuja kwenu tena nikiwa nahitaji kujua jambo hili
8-12-2016 kampuni ya Tigo Tanzania ilitangaza rasmi kuwasilisha Muhtasari na maombi ya awali CMSA pamoja na DSE ili hisa zake ziweze kuorodheshwa na watu waanze kununua na kuuza
Cha kushangaza mpaka leo hii, Tigo Tanzania si miongoni mwa makampuni yaliyo Kwenye orodha ya DSE
Naomba kujua ni kwanini. Je bado taratibu hazijakamilika? Wameamua kuachana na huo mpango? Au sababu hasa ni nini
Mwenye kujua anijuze tafadhali
Nawasilisha,