Kwanini timu nyingi Ulaya zinatumia mfumo wa 3-4-3

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kwa siku za karibuni nimeshuhudia vilabu vingi barani Ulaya vikitumia mfumo wa 3-4-3. Makocha wengine wameuboresha na kuwa 3-5-2. Mfumo huu wa 3-4-3 yaani kuwa na Mabeki watatu, Viungo wanne na Washambuliaji watatu. Je mfumo huu unambeba yupi kati ya anayeshambulia au anayejilinda? Ni kwanini mfumo huu kwasasa unapendwa na makocha wengi?
 
Unazuia timu inayoanza kupanga masambulizi kuanzia nyuma. Mfano Man City na Chelsea
Ingawa City walishinda, lakini zilikua jitihada binafsi zaidi za De Bruiyne
 
Ngoja atakuja apa mourinho kulifafanua hili punde tu....
 
Hivi morinyo anatumia mfumo upi na man utd yake?
 
Kuna Genius mmoja kauonesha ulimwengu kuwa huu mfumo bado unafaa tena kwa ligi ngumu na yenye ushindani kama ya Uingereza
Baada ya Kuutumia na Kufanikiwa wengi wamemuiga na umeonekana kuwasaidia kwa kiasi fulani.....

Nadhani anafahamika...

Van Gaal.
 
Nadhani timu nyingi
zinatumia 4-2-3-1 . Hilo la 3-4-3 nadhani ni suala la wakati kuna muda dunia ilitawaliwa na 4-4-2 ikaja pia 4-3-3
 
Van gaal aliutumia mfumo wa 3 4 3 mechi tatu tu za mwanzo baada ya hapo akaukimbia...au kama una ushahidi wa Alivyofanikiwa kuutumia huu mfumo unaweza kuutoa...
Ukielezea mfano wa mechi moja uliomsaidia alipoutumia

Martinez aliutumia akiwa Swansea mpaka wakaitwa Barcelona ya England kwa soka safi walilokua wanacheza.
 
3-4-3 ni mfumo wa kupaki basi zaidi.

Unakuwa na mabeki kama watano ambao wanaziba nafasi za adui katika kupanga mashambulizi.

Ila pia ni mfumo wa hovyo sana, mebeki watatu wa kati kuna muda huwa wanategeana, rejea Man Utd alivyocheza na Chelsea juzi, angalia Morata alivyoruka free header huku mabeki wa Man Utd wakishindwa kujua nani akabe, nani acheze huru!

Mimi bad0 naukubali mfumo wa 4-2-3-1, yaani wachezaji sita wanakaba, wachezaji sita wanashambulia.
 
Inaruhusu mpira kuchezwa sana kati na pia kusaidia kupunguza mashambulizi ya mshambuliaji mwenye uwezo binafsi inaweza fanya marekebisho kama kiungo kakosea kuondoa shambulizi
 
Wenger ndo amekuja huo mfumo wa 3-4-3 tangu ligi ianze japo siku ya Man City alibadilisha, siupendi huo mfumo hasa akicheza Metsaker pale nyuma, nyuma kunakuwa wazi sana mnaweza kupigwa migoli mingi sana
 
Kuna Genius mmoja kauonesha ulimwengu kuwa huu mfumo bado unafaa tena kwa ligi ngumu na yenye ushindani kama ya Uingereza
Baada ya Kuutumia na Kufanikiwa wengi wamemuiga na umeonekana kuwasaidia kwa kiasi fulani.....

Nadhani anafahamika...
Conte.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…