Kwanini timu nyingi Ulaya zinatumia mfumo wa 3-4-3

Kwanini timu nyingi Ulaya zinatumia mfumo wa 3-4-3

Me napendaga christmas tree.. Upo vzur huu mfumo.... 4 - 3 - 2 - 1
 
Katika elimu ya ukocha wa Mpira yapo mambo mengi likiwemo la mfumo.
Mifumo mingi huzingatia lengo kuu aidha kujilinda (defensive) Au kushambulia (attacking)
Sasa mfumo uliotaja una faida zifuatazo
1. Ulinzi madhubuti kwa sababu ya ukuta uliopitiliza Kati na kwa sababu wachezaji wa Kati kuwa na uwezo wa kurudi nyuma.
2.Ushambuliaji madhubuti, hii ni kwakuwa eneo la kati linakuwa na wachezaji wengi na ni rahisi kwa mpira kufika eneo la ushambuliaji.
3. Umiliki wa Mpira, kuna uwezekano mkubwa wa kumiliki Mpira (ball possession)

Hasara zake
1. Mfumo huu unahitaji team work. Lazima Uwe na wachezaji wenye uwezo wa kucheza kama team.
2.Kama team pinzani itacheza counter attack ni rahisi kufungwa kwa kuwa wachezaji wa kati watakuwa mbele wanashambulia. Hii itaacha mabeki watatu ambao nao pia watakua wamesogea mbele.

Timu zinazocheza mfumo huu huwa hazina mfungaji maalum.
 
3-4-3 inawabana wapinzani hasa mnapokuwa mnabuild up attack. Hii huwa inageuka kuwa 5-3-2 mnaponza kushambuliwa. Wewe angalia Chelsea. Wakianza kushambuliwa tu, akina Moses/Zapacosta na Alonso fasta wanarudi kuweka ukuta wa back 5. Fabregas au Hazard nae hurudi kati fasta. Ndo walichowafanyia Man Utd juzi kati hapa
c4eae227-a820-4bc5-8fdd-eac95bcc450c.jpg
 
Pep gardiola akiona mifumo ya namna hyo ndio anafurahi sana coz anaamini atapata point kutoka kwa mpinzani wake Mara nyingi pep hutumia mfumo 4-1-4-1 kama akiwa anacheza na timu ngumu kama Chelsea na man u
 
Wadau wa EPL mfumo huu mnauona wa ajabu sana. Huu umetumika sana italian serie A baba la baba BIANCONERI JUVENTUS. Ila inabidi mabeki wako watatu wawe visiki vya maana alafu wote wawe na asili ya namba 4 na 5. Sharti lingine viungo wako wa pembeni inabidi washuke mara kwa mara kuja kuziba nafasi za kushoto na kulia. Ni mfumo flani kama basketball vile, Huwezi kutegea ukidhani nafasi yako ww ni winga tu, au kiungo tu. Kiufupi 3-5-2 huwezi kutumia mfumo huu ukiwa na mabeki wa kati tia maji tia maji.
 
Pep gardiola akiona mifumo ya namna hyo ndio anafurahi sana coz anaamini atapata point kutoka kwa mpinzani wake Mara nyingi pep hutumia mfumo 4-1-4-1 kama akiwa anacheza na timu ngumu kama Chelsea na man u
Kuna nyakati pia na yeye hutumia 3-4-3
 
Antonie Conte alibadili baada ya vipigo msimu uliopita,aliutumia mpaka kuchukua ubingwa.Ndio makocha wengine wakaamua kuanza kuutumia huo mfumo.Ni mfumo mzuri ila wing zako mbili za kushoto na kulia inabidi wawe na mapafu kweli.Maana inabidi wakabe huku wakishambulia pia.Angalia kwa chelsea jinsi Moses na Alonzo wanavyocheza.
 
Msimuu huu anapigwa tu mfumo bora kwa sasa ni 4-1-4-1 wa pep gardiola.
 
Barca na Madrid wanatumia 433. Mfumo unatoa soka safi sana. Ila inabidi uwe na mafullbacks wenye spidi na creative. Ukipata na inverted wingers hakuna timu itakusumbua.
 
3-4-3

Wakidefence wanakuwa 7

Wakishambulia wanakuwa 7

So morinyoooo akikutana na Chelsea huwa anaona kama wapo 14 [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Siku anacheza na Liverpool alikuja na na 6-3-1 akaambulia draw. Mechi iliyofuata akawa direct, akachapwa. Siku anacheza na Chelsea akaedit kidogo akaja na 5-5-0. 😀
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom