Kwanini timu za zanzibar hazishiriki Kombe la Azam.?

Kwanini timu za zanzibar hazishiriki Kombe la Azam.?

Mwaka jana ktk ASFC YANGA alikutana na MWADUI ya Jamhuri Kihwelu (Asst. Coach Mwanamtwa Kihwelu)! YANGA alipenya kwa mbinde sana! Na mwadui waliamini Yanga inabebwa! Mwanamtwa Ktk malalamiko ya kwa referee, anasema referee alimjibu kuwa MNATAKA MSHINDE, MTAWEZA KUWAKILISHA NCHI HUKO DUNIANI?
Hahahah huyo Refa kavu sana. Ila ukiangalia kilochomkuta Mtibwa utasema Refa yupo sahihi.
 
Habari za jumapili wanajamvi.
Kama swali linavyo jieleza. Najua kuna taasisi zinazosimamia mchezo wa mpira wa miguu bara na visiwani, !
Je kwanini hawana wazo la kuzifanya timu za mpira wa miguu za zanzibar na za huku bara kukutana katika kombe la Taifa (Azam Cup) ambalo linazikutanisha timu kutoka mikoa yote ya Nchi yetu na Bingwa anashiriki katika mashindani ya kimataifa.
Kombe la shirikisho ambalo kwa msimu huu Tanzania iliwakirishwa na Mtibwa.
Tukiondoa siasa, na faida binafsi za viongozi nadhani mashindani hayo yangetoa fursa nzuri kwa wachezaji wa zanzibar kuonekana na kupata uzoefu bara!
Na nafasi ya kuonekana katika mashindano makubwa zaidi ya kimataifa.
Bila kusahau kuwa mashindano haya yangesaidia zaidi kuboresha. Uzalendo wetu kama Watanzania. Kombe la Mapinduzi linaweza kuwa na Mchango wa Uzalendo lakini Kombel la Taifa/ Azam Cup ingeweza kuwa na mchango mkubwa zaidi.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hujui kuwa Zanzibar ni nchi na ina utaratibu wake wa kupata timu za kushiriki CAF?
 
Mkuu tukiacha unafiki Zanzibar sio Nchi ni sehemu ya Nchi ya Tanzania ambapo Tanzania kama Nchi inawakilishwa na TFF.
Hizo mbwembwe nyingine za kisiasa zisizo na mbele wala nyuma ndiyo zinazowakwamisha vijana wetu leo na kesho. Ifike mahali watu wawe na akili na waache unafiki. Na ujuha.
Mkuu hujui kuwa Zanzibar ni nchi na ina utaratibu wake wa kupata timu za kushiriki CAF?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom