Kwanini timu zetu zinakuwa mbovu ugenini?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Sababu zipi timu zetu za Afrika zinakuwa nyanya (5-0, 5-0, 2-0, n.k) ugenini na kuwa imara (3-0, 2-0, 1-0, nk) nyumbani tofauti na Ulaya ambako timu inapindua matokeo hata ugenini. Hii ni dalili tosha kuwa timu zetu zinafanya hujuma (uchawi, kuwekewa madawa kwenye vyakula/maji, kupuliziwa dawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, n.k) timu ngeni zinapocheza nyumbani ili kuzidhoofisha ngeni.

CAF lazima zifanye uchunguzi wa kina kuhusu jambo hili. Hata Azam na Yanga kukataa kuingia vyumba vya kubadilishia nguo uwanjani ni sehemu ya hofu hiyo. ova
 
Subiri ya j.mosi utaedit uzi wako, wakongo wanapindua meza ya matokeo.

Barafu la moto
 
Mchezo huo walikuwa nao waarabu peke yao, siku hizi hata timu nyingine inaonekana kuwa wameuiga kiasi kwamba wanautumia hata kwenye ligi zao za nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…