Kwanini tofauti ya bei ya mabati kati ya China na Tz ni kubwa hivi?

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,877
Reaction score
2,314
Wana Jf habari,

Hivi karibuni nimekuwa nikilinganisha bei za maezeko/mabati kati ya nchi mbili tajwa nikabaki na maswali mengi nikaona niwashirikishe huenda mkanisaidia. Ipo hivi, baada ya kutamani mabati yale "matamu matamu" kama yale life style ya gauge 26, hapa kwetu kipisi kimoja kinacheza kwenye tsh. 20,000-23,000, wakati kipisi kama hiki kwa China kinacheza kama tsh.8,000. Ukipiga mahesabu, pamoja na usafiri mpaka unakuja kuezeka hapa Tz, unakuta bei inakaribia nusu au kuzidi kidogo nusu ya gharama za Tanzania. Swali langu ni, huu ni muendelezo wa China kuuza bidhaa duni ama ndiyo kusema sisi gharama za uzalishaji zipo juu kiasi cha kusababisha haya? Je, mlionunua bati kwa kuagiza moja kwa moja Uchina mnasemaje kuhusu ubora kwa kulinganisha pande hizi mbili?

Muhimu
Hapa ninazungumzia wale waliogiza toka viwanda rasmi kule China, siyo haya yasiyojulikana mtengenezaji hapa Bongo au haya ya viwanda fulani vya kichinachina vya hapa Tz vilivyojaza soko hivi siku za karibuni karibuni.

Ninaomba kuwashirikisha
 
Vipi kuhusu kodi??? Katika hesabu zako umejumlisha gharama za kumlipa TRA mzigo ukifika??? Usikute gharama kwa ujumla kuanzia gharama halisi ya bidhaa + usafiri + kodi ni sawa na kununua nyumbani na bado cha nyumbani kikawa bora zaidi.

NOTE: Wanasema ukiagiza bidhaa toka nje ya nchi na bidhaa hizo hizo zinazopatikana kwa kuzalishwa nchini basi jiandae kwa kodi kubwa. Sijawahi agiza mabati nje ya nchi ila hiyo nimekutana nayo kwenye kitu tofauti na mabati. Wapo waliowahi agiza mabati nje ya nchi hapa jukwaani watatuletea ushahidi.
 
Mkuu kwa Upande wa China siyo mabati pekee yanayouzwa kwa bei ya mkate. Bidhaa karbia zote zikiwemo za Umeme, vifaa vya Magari, Nguo nk. Tatizo ni Ubora wa bidhaa hizo na Kikokotoleo cha TRA
 
Majibu mbona rahisi sana kiongozi? Hapo ni sawa na kuuliza mbona korosho tanzania bei ni rahisi sana kuliko china? China wana vieanda vingi vya mabati na malighafi za kutosha kutengeneza mabati kwa wingi, tz hatuna viwanda vingi vya mabati
 


Nimelifanyia kazi mkuu. Mpaka ninakuja hapa, ujue nimeshapambana sana na fumbo hili.Nilipozidiwa nikaja hapa jamvini kupanua mawazo. Yani kwa saizi na aina ya mabati niliyodokeza wakati nachokoza mada, ukichukua vipisi kati ya 800 hadi 900, basi mabati pekee inacheza milioni nane za tz na usafiri na kodi haizidi milioni 2. Hata ukisema labda usafiri na kodi ni milioni 4, jumla utapata milioni 12, tayari unashika mabati yako. Huo moto kauguse kwa bati kama hizohizo za Kitanzania uone moto wake.
 
Mkuu kwa Upande wa China siyo mabati pekee yanayouzwa kwa bei ya mkate. Bidhaa karbia zote zikiwemo za Umeme, vifaa vya Magari, Nguo nk. Tatizo ni Ubora wa bidhaa hizo na Kikokotoleo cha TRA


Mimi pia naliona hili, sema nikaona si vema kujiridhisha peke yangu. Ninamashaka hapohapo kwenye ubora. Sasa kwa kuwa si mtaalamu, ninashindwa kuthibitisha mpka ninunue na kuumia, dah!
 
Majibu mbona rahisi sana kiongozi? Hapo ni sawa na kuuliza mbona korosho tanzania bei ni rahisi sana kuliko china? China wana vieanda vingi vya mabati na malighafi za kutosha kutengeneza mabati kwa wingi, tz hatuna viwanda vingi vya mabati


Asante. Ni baada ya kuona tofauti ni kubwa kibei kupita maelezo. Mana kama kweli bati hizo za china zina ubora, kwanini tunaumia na bati ghali za nyumbani? Maana hata ile maana ya kukuza vya nyumbani haipo tena, bali ni kumuumiza mwananchi. Bei inakata karibu nusu ujue.Mimi ninadhani ubora ni mdogo
 
Majibu mbona rahisi sana kiongozi? Hapo ni sawa na kuuliza mbona korosho tanzania bei ni rahisi sana kuliko china? China wana vieanda vingi vya mabati na malighafi za kutosha kutengeneza mabati kwa wingi, tz hatuna viwanda vingi vya mabati
kiukweli tz sijaona kiwanda cha 'kutengeneza' mabati, vingi hufanya 'coating' na 'roll forming/corrugation',

'coil' yenyewe(bati lenyewe hasa) hua yanatoka Japan/China
 
niko hapa kutaka kujua mengi zaidi, mi ni mwagizaji mzuri wa vitu toka china ila sijawahi agiza bati swala la ubora wa bidhaa ni uwe unafahamu bidhaa husika ili uweze kutofautisha na unayotaka kununua nje, pia kuangalia maoni ya wengine uone wanazungumziaje hiyo bidhaa
 
alaf , sunshare wote hao, wana import 'coils' kutoka uchinani/japan,
hali mbaya kwa ivi 'viwanda bubu' ambavyo huchukua 'bad coils' zilizokua sorted out na akina alaf,

Nakupata hapo
 
Bahati mb
Kabla ya kushangaa bati la China ,shangaa kwanza Zanzibar sukari kilo moja 1500 hapa dar sukari hiyo hiyo 2600

Sent using Jamii Forums mobile app

Bahati mbaya hii haijibu swali, inaimarisha swali la msingi labda. Kwa kifupi vigezo ni vingi, mfano, movie ya sukari kwa Zenji uliona wazalishaji wa Zenji walikatazwa kuuza bara.Sijui kama washaruhusiwa.
 
Mkuu kuna ishu ya ubora sijui km uneifikiria?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
material au malighafi upatikanaji wake ni mkubwa kuliko hapa,ndo maana hawa watu binafsi wanaounda mabati siku hizi material wanaagiza toka china
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…