Mtafiti77
JF-Expert Member
- Oct 31, 2011
- 1,877
- 2,314
Wana Jf habari,
Hivi karibuni nimekuwa nikilinganisha bei za maezeko/mabati kati ya nchi mbili tajwa nikabaki na maswali mengi nikaona niwashirikishe huenda mkanisaidia. Ipo hivi, baada ya kutamani mabati yale "matamu matamu" kama yale life style ya gauge 26, hapa kwetu kipisi kimoja kinacheza kwenye tsh. 20,000-23,000, wakati kipisi kama hiki kwa China kinacheza kama tsh.8,000. Ukipiga mahesabu, pamoja na usafiri mpaka unakuja kuezeka hapa Tz, unakuta bei inakaribia nusu au kuzidi kidogo nusu ya gharama za Tanzania. Swali langu ni, huu ni muendelezo wa China kuuza bidhaa duni ama ndiyo kusema sisi gharama za uzalishaji zipo juu kiasi cha kusababisha haya? Je, mlionunua bati kwa kuagiza moja kwa moja Uchina mnasemaje kuhusu ubora kwa kulinganisha pande hizi mbili?
Muhimu
Hapa ninazungumzia wale waliogiza toka viwanda rasmi kule China, siyo haya yasiyojulikana mtengenezaji hapa Bongo au haya ya viwanda fulani vya kichinachina vya hapa Tz vilivyojaza soko hivi siku za karibuni karibuni.
Ninaomba kuwashirikisha