Kwanini Toyota wanapanga kusitisha kuzalisha V8

Kwanini Toyota wanapanga kusitisha kuzalisha V8

V6 za kisasa zenye turbo 1 au zaidi zina horsepower na torque kubwa kuliko V8 za zamani kama hiyo ambayo Toyota wamekua wakiitumia kwa miaka mingi kwenye gari zao za bei mbaya.

Jambo lingine ni sheria za kulinda mazingira huko nchi zilizoendelea zinawabana wazilishaji wa magari kutumia clean technology. Kila kampuni imewekewa limit ya hewa ukaa ambayo magari yake yanatakiwa kuzalisha.

Let's say Toyota imeuza gari ngapi ulaya au Marekani,hizo kwa mwaka zinazalisha hewa ukaa kiasi gani? Kama ikizidi limit waliowekewa basi wanapigwa fine nzito, ndio maana RAV4 za Uingereza ni hybrid ili kupunguza greenhouse gas wakati za SA ni non hybrid.

Hybrid ni necessity sio kwamba wanapenda kutengeneza, Mazda mwaka jana ulaya wamepigwa fine karibia Euro my 150 kwa uchafuzi wa hewa coz walikua hawana hybrids kwenye models zao kusaidia kupunguza uzalishaji wa greenhouse gas.

Toyota na car makers wengine future ni hybrids au pure electric,hizi engine kubwa v8,v10 na v12 zinaenda kuzikwa rasmi ndani ya miaka 15 ijayo.
 
Mi huwa nayaona takataka tu. I adore Mercedes Benz G Class
au kwa sababu nimeona magari mengi na kudrive mazuri pia yaani niache kufikiri Cayenne,bmw X 6 4.0d au hayo Mercedes GL Class nifikiri viieiti hapana sina mapenzi ya kuiga mkumbo kuna mnyama mwingine biography ukiendesha utadhani upo ndani sitting room gari imetulia mnooo...
 
Hapa naomba mnisaidie kuelewa... Je, V8 ni aina ya gari au ni aina ya engine? Siku zote mimi nimekuwa nikijua kuwa V8 ni aina ya engine (eight cylinders) na zipo kwenye seeies mpaka V12 (kwenye supercars). Mwenye utaalamu atupe darasa tafadhali

V8 ni engine !!, hii imetokana na V configuration, Toyota walianza kutumia hii configuration toka Miaka mingi nyuma kwa engine za 1 and 2 Uz sema hizi zilikuwa ni petrol zilikuwa very heavy kwenye ulaji wa mafuta ,

Mwaka 2009 ndo Ikaja 1vd ambayo ni diesel version ya v8 kutoka Toyota , hii ndo imekuwa maarufu kutokana na kuwa na power combined with fuel efficient.

Yap zipo Hadi v12 kwenye super cars , na v20 kwa engine za meli ,
 
mbona magari ya fahari yapo mengi tu?!?, watanunua hata ford za kimarekani. Hata hivyo naamini toyota watakuja na toleo jipya expensive zaidi na africa itahamia huko
Mkuu toyota hawawezi kuacha kuazalisha gari ya gharama na inayotesa soko la Australia na Afrika kirahisi tu hivi.

Wanachofanya nu kwamba wanakuja na 300 series ambayo inakuwa announced mwezi wa 6 mwaka huu
 
Back
Top Bottom