Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Katika zama za kidigitali, taarifa si tu chanzo cha maarifa ama elimu bali pia ni nguvu ya kijamii na kisiasa. Haki ya kupata na kulinda taarifa binafsi imekuwa moja ya mihimili ya demokrasia na utawala bora.
Hata hivyo, mijadala ya sasa kuhusu Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini Tanzania imefungua ukurasa mpya wa maswali: Je, taasisi hii kweli inalinda masilahi ya wananchi au inatumika kama chombo cha kulinda watawala? Inalinda masilahi ya watanzania au viongozi wachache?
Kujiuzulu kwa Maxence Melo, Mkurugenzi wa Jamii Forums na mmoja wa wajumbe waliokuwa tegemeo katika Tume hii, kumeweka wazi kwamba mambo si shwari hata kidogo. Melo amekuwa mstari wa mbele na ni sauti inayotambulika kwa kupigania haki za kidigitali na uhuru wa kupata taarifa.
Hatua yake ya kujitoa kwenye Bodi inatafsiriwa na wengi kama ishara ya kukata tamaa kwa sababu ya mfumo uliojengeka ndani ya Tume hiyo. Inaonekana ni wazi kuwa hata wajumbe wa Bodi hii wanapitia mengi sana, kutokana na imani zako kuhusu Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Changamoto ya Uteuzi wa Viongozi
Kwa sasa, wajumbe wa Bodi wanateuliwa na mamlaka za juu serikalini. Hii inazua mgongano wa moja kwa moja: unatarajia vipi chombo kilichoundwa na watawala kiwe huru kuwakosoa hao hao watawala? Hali hii inasababisha Tume kuonekana dhaifu na kukosa ujasiri wa kusimama upande wa wananchi.
Watanzania wanahitaji mfumo mpya wa kupata wajumbe wa Tume hii. Badala ya uteuzi wa kisiasa, tunapaswa kuangalia mchakato wa kidemokrasia unaohusisha kura za wananchi au angalau mchakato shirikishi unaojumuisha vyama vya kiraia, wanahabari na asasi huru. Kwa kufanya hivyo, uhalali wa Bodi utakuwa si wa kisiasa, bali ni nguvu kutoka kwa wananchi wenyewe.
Masilahi ya wananchi Dhidi ya Masilahi ya Wachache
Lengo kuu la Tume ni kulinda taarifa binafsi na kuwezesha wananchi kufurahia haki zao za kidigitali. Lakini kinachoonekana sasa ni Tume kutumika kama ngao ya kuziba mianya ya taarifa zinazohusu serikali na viongozi wake.
Wakati taarifa za umma zinapaswa kuwa wazi kwa manufaa ya kila mmoja, mara nyingi zinageuzwa siri kwa kisingizio cha “usalama” au “faragha ya taifa.”
Picha ya kiongozi fulani ikichapishwa na kiongozi mwenye mtandaoni haina tatizo ila picha hiyo hiyo ikichapishwa kwenye ukurasa wa Godlisten Malisa ni kosa la kisheria, ni sawa na kusema moja kujumlisha moja ni mbili ila ukifanya wewe hesabu jibu ni tofauti, moja kumjulisha moja ni kumi na moja.
Kimsingi, upatikanaji wa taarifa ni chachu ya uwajibikaji. Wananchi wanapojua maamuzi yanayochukuliwa, fedha zinazotumika na mikataba inayosainiwa, ndipo wanaweza kuwawajibisha viongozi wao. Bodi inayokwepa jukumu hili inakosa maana kabsa.
Kuvunja Bodi ya sasa na kuunda upya kwa mfumo huru ni hatua isiyoepukika hata kidogo. Mageuzi hayo yanapaswa kujumuisha:
1. Uchaguzi huru wa wajumbe kupitia wananchi. Waziri wa Habari na Naibu wake wasihusike kabsa, kuepusha migongano ya kimaslahi, hawa ni wateule wa Rais.
2. Uwazi wa maamuzi ya Tume ili wananchi waone inavyofanya kazi.
3. Uwajibikaji wa moja kwa moja kwa umma, badala ya kuwasilisha taarifa kwa Rais au mawaziri pekee, taarifa iwe inakwenda kwa wananchi ambao wanaweza kukosoa.
4. Kipaumbele cha umma, kuhakikisha taarifa za masilahi ya taifa zinapatikana kwa urahisi bila urasimu usio na msingi.
Kujiuzulu kwa Melo ni kengele ya tahadhari, si tukio la kupuuzia kama ambavyo watu waliopo kwenye mfumo wanafikiria. Ni ujumbe kwamba mfumo uliopo haupo sawa, mfumo wa kibabe tena wa kibeberu. Tanzania inahitaji Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo haitumikii Rais, Waziri Mkuu, au Waziri wa Habari, bali wananchi wa Tanzania, vizazi na vizazi.
Kwa kuunda Tume huru, tunalinda si tu taarifa binafsi bali pia misingi ya uwazi, demokrasia, na mustakabali wa taifa. Bila mageuzi haya, Tume itabaki kivuli cha taasisi iliyokusudiwa kuwa nguzo ya haki na uwajibikaji.