viongozi wetu wanatutisha sana kuhusu kenya wanatuambia tutakua soko la kenya lakini hawatutishi kuhusu uchina, ki takwimu mwaka jana tuliuza bidhaa kenya zaidi ya walivyouza kwetu kwa takribani 2%, ingawa bidhaa tulizouza pia zingine zilitoka china ila ukifuatilia china wametuuzia bidhaa zaidi kwa asilimia 98% kwa akili za kawaida utagundua sisi ni sehemu ya godown la china , lakini viongozi hawaonyeshi kutaka kuleta kauwiano wa biashara kati yetu na china, je tuogope kenya anavyokuja kwetu zaidi ya nchina?
Kenya sio tunaiogopa, bali ni ukweli unaotokana na hali halisi. Kuna tofauti kubwa ya ukaribu au mtazamo wa muda mrefu wa kiushirikiano baina yetu na Kenya,na baina yetu na China.
Kenya ni nchi iliyomo katika jumuiya Afrika mashariki. Mtazamo wa kiushirikiano wamuda mrefu ni kuungana kwa jumuiya hiyo na kuwa kama nchi moja. Hili ni jambo kubwa sana na makini na ni lazima liangaliwe kwa pande zote, si tu kuwa wao wametuzidi kibiashara na elimu bali vile vile political stability.
Ni muhimu tuelewe kuwa tukishaungana ndio tumeungana kurudi nyuma si rahisi. Mfano ni Zanzibar, nchi ambayo kwa kipindi cha miaka 40 inmekuwa na manunguniko hayo hayo, lakini kuugeuza mchezo ni ndoto ya mwendawazimu.
Kwa upande mwingine China ni nchi iliyo mbali kijiografia na tunamikataba nayo ya muda(Fixed period) katika maswala mbali mbali, ambayo pale tusiporidhika wakatiwowote tunaweza kujitoa. Na hii ndio tofauti kubwa ambayo watanzania tunawajibika kuielewa.
Hapa nimeeleza kifupi tu, lakini ni muhimu kuelewa kuwa Mchina kupata uraia wa Tanzania kisheria ni process ndefu. Of course kama hatuzungumzii rushwa iliyoiandama nchi yetu, lakini tukiungana na Kenya watakuwa na haki kama watanzania. Hii ni pamoja na ardhi ambayo Wakenya walishaiuza kwa Waingereza na matajiri wao. Hivyo wanauhaba mkubwa wa Adrhi leo hii.
Hayo yote lazima yawekwe sawa kabla hatujaungana. Kwa hiyo hatuwaogopi, bali tunayaweka mambo sawa. Haraka haraka haina baraka.