Kwanini tuiogope Kenya zaidi ya China?

Kwanini tuiogope Kenya zaidi ya China?

Godwine

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2010
Posts
1,371
Reaction score
283
viongozi wetu wanatutisha sana kuhusu kenya wanatuambia tutakua soko la kenya lakini hawatutishi kuhusu uchina, ki takwimu mwaka jana tuliuza bidhaa kenya zaidi ya walivyouza kwetu kwa takribani 2%, ingawa bidhaa tulizouza pia zingine zilitoka china ila ukifuatilia china wametuuzia bidhaa zaidi kwa asilimia 98% kwa akili za kawaida utagundua sisi ni sehemu ya godown la china , lakini viongozi hawaonyeshi kutaka kuleta kauwiano wa biashara kati yetu na china, je tuogope kenya anavyokuja kwetu zaidi ya nchina?
 
hahahha china ndo kimeo Ila si unajua tulifunga nao ndo kazi kuwamwaga!!
 
kenya hawana jipya zaidi ya majambazi na immoral soceity, uchu wao wote ni kuja uku kufanya kazi kwani jeshi la unemployed pipo ni kubwa so they want some space to breath, china wanatupa loan mbalimbali za maendelo, kenya watatupa nini? technology gani watayotupa tujisikie tumeendelea? china wana product za high tech at reasonable price, siwalaumu china hata kidogo kwa bidhaa wanazoleta, kwa mfano mtanzania wa kima cha chini anaelipwa 120000 kwa mwezi aache kuangalia african cup of nation or world cup or news kwa sababu hana plasma tv inayouzwa 1.5million? kwa nini asinunue fake tv ya china ya 90000 akaona mpira? kwa iyo hadi azeeke bila kuenjoy burudani ya mpira kwa sababu hana tv! au vijana wa kisasa asivae nguo yenye jina la designer kwa sababu hawezi kununua woolworth? kila mtu atajikuna anapofikia, kama wewe unataka quality product, its simple go to dealer! kila kitu nchini kina dealer.
 
Labda mnawaogopa kama nao wanavyowaogopa wasomali! Kwi kwi kwi!

I nkai kwei kwei.
 
viongozi wetu wanatutisha sana kuhusu kenya wanatuambia tutakua soko la kenya lakini hawatutishi kuhusu uchina, ki takwimu mwaka jana tuliuza bidhaa kenya zaidi ya walivyouza kwetu kwa takribani 2%, ingawa bidhaa tulizouza pia zingine zilitoka china ila ukifuatilia china wametuuzia bidhaa zaidi kwa asilimia 98% kwa akili za kawaida utagundua sisi ni sehemu ya godown la china , lakini viongozi hawaonyeshi kutaka kuleta kauwiano wa biashara kati yetu na china, je tuogope kenya anavyokuja kwetu zaidi ya nchina?
Kenya sio tunaiogopa, bali ni ukweli unaotokana na hali halisi. Kuna tofauti kubwa ya ukaribu au mtazamo wa muda mrefu wa kiushirikiano baina yetu na Kenya,na baina yetu na China.

Kenya ni nchi iliyomo katika jumuiya Afrika mashariki. Mtazamo wa kiushirikiano wamuda mrefu ni kuungana kwa jumuiya hiyo na kuwa kama nchi moja. Hili ni jambo kubwa sana na makini na ni lazima liangaliwe kwa pande zote, si tu kuwa wao wametuzidi kibiashara na elimu bali vile vile political stability.

Ni muhimu tuelewe kuwa tukishaungana ndio tumeungana kurudi nyuma si rahisi. Mfano ni Zanzibar, nchi ambayo kwa kipindi cha miaka 40 inmekuwa na manunguniko hayo hayo, lakini kuugeuza mchezo ni ndoto ya mwendawazimu.

Kwa upande mwingine China ni nchi iliyo mbali kijiografia na tunamikataba nayo ya muda(Fixed period) katika maswala mbali mbali, ambayo pale tusiporidhika wakatiwowote tunaweza kujitoa. Na hii ndio tofauti kubwa ambayo watanzania tunawajibika kuielewa.

Hapa nimeeleza kifupi tu, lakini ni muhimu kuelewa kuwa Mchina kupata uraia wa Tanzania kisheria ni process ndefu. Of course kama hatuzungumzii rushwa iliyoiandama nchi yetu, lakini tukiungana na Kenya watakuwa na haki kama watanzania. Hii ni pamoja na ardhi ambayo Wakenya walishaiuza kwa Waingereza na matajiri wao. Hivyo wanauhaba mkubwa wa Adrhi leo hii.

Hayo yote lazima yawekwe sawa kabla hatujaungana. Kwa hiyo hatuwaogopi, bali tunayaweka mambo sawa. Haraka haraka haina baraka.
 
Wakenya noooo....bora wachina...hatutaki kuchinjana chinjana kuhamie bongo. Kimsingi arrogance ya wakenya mimi inanitia kichefuchefu. Sitabadili msimamo...nilishaonja machungu ya wakenya.
 
viongozi wetu wanatutisha sana kuhusu kenya wanatuambia tutakua soko la kenya lakini hawatutishi kuhusu uchina, ki takwimu mwaka jana tuliuza bidhaa kenya zaidi ya walivyouza kwetu kwa takribani 2%, ingawa bidhaa tulizouza pia zingine zilitoka china ila ukifuatilia china wametuuzia bidhaa zaidi kwa asilimia 98% kwa akili za kawaida utagundua sisi ni sehemu ya godown la china , lakini viongozi hawaonyeshi kutaka kuleta kauwiano wa biashara kati yetu na china, je tuogope kenya anavyokuja kwetu zaidi ya nchina?

Hakuna anayewaogopa nyang'au, tulimtoa nduli itakuwa hawa vibaraka. Usitie shaka tunakula nao sahani moja hadi watakapowaambia mabwana zao sijui ankal etc wameshindwa. Sisi ni taifa kubwa angalia historia, tuna marafiki wengi tu lakini sio Kenya.
 
Dr Lwaitama aliwahi kusema kwa mujibu wa utafiti Tanzania ina watu wenye fikra makini kuliko nchi zote za Afrika. Nawaomba na nawasihi sana ndugu zangu tujiamini na tutashinda mapambano yoyote yatakayokuja mbele yetu.
 
Back
Top Bottom