Wakuu mimi si mtaalamu sana wa sheria lakini najaribu kujiuliza maswali machache.
1. Kwanini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Kupitia mkurugenzi wake) inajaribu kujibu na kukanusha tuhuma kwa mgombea fulani. Si ilipaswa yeye mwenyewe au waenezi wa chama kama akina polelepole wafanye hiyo kazi?.
2. Je, Mkurugenzi anavosema mgombea A anapotosha umma na kuwadhihaki wengine, je hiyo kauli yake kuwa kuna watu watapeleka madini nje kwake haoni kama ni tuhuma pia.
Na hii imesemwa na mgombea anaye mtetea, haoni kama ni kitu kilekile anachokataza upande wa pili?
3. Anavosema watanzania wanataka A,B,C, hawataki E,F,G ni lini alikaa na watanzania wakamwambia hayo. Je anaweza kuthibitisha hayo mahakamani.
4. Je, uvunjaji wa taratibu unaofanywa na baadhi ya wagombea ubunge, mfano anayetoka nje ya jimbo lake kumnadi mgombea urais wa chama chake (kazi iliyopaswa kuwa ya mgombea mwenza) hayo haoni kama ni ukiukwaji wa taratibu?
Nawasilisha