Kwanini tunaaminishwa Freemasons ni watu wabaya lakini kiongozi wake nchi nzima tunamuhusudu?

Kwanini tunaaminishwa Freemasons ni watu wabaya lakini kiongozi wake nchi nzima tunamuhusudu?

Ni heri anaefahamika ana roho au imani za kishetani kuliko kuwa na watu wanaojifanya kuwa wakarimu wanajali wanauchungu watu wa dini kumbe ni mashetani wakubwa..chande anaweza kuwa na roho nzuri sana kuliko raisi
 
Hakuna imani ya kweli inayokimbia maswali ndugu, "Ila tumeambiwa tu Maswali ya kipuuzi ujiepushe nayo.."
sasa umepigana na nani au hizo vita zinauhusiano gani na ufreemason kuwa mbaya au mzuri
Vita vya kiroho...vita vya imani kama unayopigana sasa hivi kwamba iweje kuwa huyu anasemwa hivi na yuko vile...Bila shaka una inner conflict au siyo? Basi sisi vita vyetu ni vya kiroho lakini matokeo huwa katika ulimwengu wa kimwili kama hivi nilivyoweka summary kuwa sasa hivi ushindi upo upande wetu sisi ambao tunaamini kinyume na wao...Is it clear!
 
Mbona kuna jambo hujajiuliza kama kuna jema kwanini waumini wake hawajitambuli shi kwenye jamii kama walivyo waislam na wakristo
 
Ni heri anaefahamika ana roho au imani za kishetani kuliko kuwa na watu wanaojifanya kuwa wakarimu wanajali wanauchungu watu wa dini kumbe ni mashetani wakubwa..chande anaweza kuwa na roho nzuri sana kuliko raisi
Kama huyo ni mbaya kwako basi ujue na wewe ni mbaya kwake...huo wema wako ni ubaya kwake kama ulivyo ubaya wake kuwa wema kwa mtu kama mimi...Duniani kuna roho mbili tu ya shetani na ya Mungu na kila mmoja ni mbaya kwa upande wa mwenzake...Jiulize una beba roho ipi?
 
Mbona kuna jambo hujajiuliza kama kuna jema kwanini waumini wake hawajitambuli shi kwenye jamii kama walivyo waislam na wakristo
Tangu lini wema ukawekwa gizani? Duniani kuna watu!
 
Napita tu make hawa watu wabaya sana
Usiwaogope hawana lolote zaidi ya hofu na mashaka ndicho wanachokuzidi...Umekombolewa na dunia yote imenyang'anywa kwao ila tu wana operate in structure na deceptions...

Ogopa mtu mwenye roho mtakatifu yeye awezaye kufufua kilichofishwa kwa jinsi yoyote ile...Let us put them to the place where they deserve!
 
Kuna tofauti kati ya mama na Mama?
hiki ni kiswahili na makubaliano ya wanalugha mkuu.
Hakuna tofauti kati ya mama na Mama, ila kuna tofauti kati ya Mungu na mungu au God na god.
sio mimi ni dunia ndio imekubaliana hivyo...
 
Wabongo kwa ushabiki hatujambo
Gold is available deep deep inside the the earth surface
 
Wanosema kuwa shirika la wajenzi huru ni wabaya walete ushahidi,

Wajinga tu ndo wanoamini maneno ya vivumishi kuwa Freemason ni wabaya
 
Hill no dhehebu kama mengine. Mvutakamba anavutia kwake. Freemason sio wabaya kwa jinsi tunavyoaminishwa. Wala hawajawahi kulazimisha mtu kua mfuasi wao. Binafsi nawapenda kwa jinsi ya utaratibu wao..wanakutana kwa mambo yao. Ambayo ni shughuli zao.wangekua wabaya naamini wangeshazuiliwa ku operate. Uwe makini na maneno ya wasiowapenda
 
nakupata, Ila Tanzania hatutambui Atheists, na ndio maana Wimbo wa Taifa Tunaimba Mungu Ibariki mkuu.
hivyo kipengele cha wapingwe wote kinakuwa hafifu hapo...
Kwani kuna watu wananyimwa haki flaniflani kwenye jamii mimi naona yoyote hata wewe unaweza kuanzisha Taasisi inayotambua Uwepo wa Mungu na ukafanya yako bila usumbufu...
Dah kumbe Atheists hawatambuliwi Tz ndo maana tunaimba Mungu ibariki... Asante kwa elimu mkuu
 
Juzi Taifa limepata msiba kwa kupotelewa na mkuu wa Freemason Tanzania kama sio EA mzee Chande. Mkuu wa Taasisi/Club/Dhehebu ambalo Mkuu wake anafahamika lakini waumini au members zake hatuwajui. Duniani kote kuanzia miaka ya 2000 mashambulizi misikitini,makanisani,kwa waganga, Wasanii wafuatiliaji wa mambo wamekuwa wakiishutumu Taasisi hii kama ni ya kichawi, hatari,haifai, Yenye nguvu isiyozuilika.

Sasa leo tunagundua kumbe kiongozi wa taasisi hii pingwa, ni Mtu mzuri, anamchango mkubwa kwenye jamii, hajawahi kukutwa hata na chembe ya shutuma, hata wanaomfahamu wakimuelezea kurasa hata 1000 hutachoka kumaliza wasifu mzito wa mtu huyu mashuhuri.


Wajuaji wa mambo mtusaidie, Tuchukue Freemason Ipi, Ile Inayopodwa mitaani,Mitandaoni,makanisani,Misikitini,waganga, Uswahilini hofu ya freemasonry ndio usiseme, Humu JF, au Hii ya Mzee Chande ambayo imewaunganisha wanasiasa wa upinzani, watawala na watawaliwa kumlilia. Hii ambayo viongozi wetu wote toka nyerere walikuwa wakimpenda na kuwa karibu na kiongozi wetu...

Ninaandika nikiwa na OMBWE la maharifa juu ya hii taasisi lakini ninauhakika wa Hofu(wenda ya kweli au ya kutengenezwa na wajanja wachache mitaani kwa manufaa yao) juu ya taasisi inayosadikiwa kuwa tata na ya siri iliyotapakaa Dunia nzima na inayosemekana ilianza miaka 1600BC kwa mujibu wa Uzi wa mkuu wetu wa JF Melo Freemasons Inside - Out: Who are they? How they operate? How to join them?

karibuni wadau mtutoe tongotongo sisi wa vijijini...

cc: Magazeti ya leo
20170408_045700.jpg

Kanumba ahusishwa na mambo ya freemasonry kutokana kupishana siku moja na mkuu wake katika kifo (Gazeti la UDaku)
20170408_045850.jpg

Mwananchi:Zitto amlilia kiongozi wa Free mason kuzikwa J4.
20170408_045909.jpg

Mtanzania, Siri kifo cha kiongozi wa freemason
na mengine mengi yakionyesha masikitiko yake juu ya kupotelewa na mtu huyu mashuhuri nchini.


Kwanza nafuta maneno yako ya kuwatamkia watu kwamba wanamhusudu freemason. Ni wewe tu na watu wenye mawazo ya kishetan i kama wew endio mnahusudu umpumbvu wa kishetnai huo.

Mimi na uzao wangu hatumo miongoni mwenu. Nchi zima kwako iishie kwenye maishay yako na uyaone wee mwenyewe. Upumbave hatutaki.

Koma kutujumulisha wote.
 
Kwanza nafuta maneno yako ya kuwatamkia watu kwamba wanamhusudu freemason. Ni wewe tu na watu wenye mawazo ya kishetan i kama wew endio mnahusudu umpumbvu wa kishetnai huo.

Mimi na uzao wangu hatumo miongoni mwenu. Nchi zima kwako iishie kwenye maishay yako na uyaone wee mwenyewe. Upumbave hatutaki.

Koma kutujumulisha wote.
Pouwa poa muwakilishi wa uzao... Ila ungethibitisha na ushetani wao ungesaidia wengi.
Punguza munkari jukwaa linahitaji reasoning zaidi ya indoctrination
 
Freemasoni ni wabaya

Mzee wetu tuliye mheshimu sana,

Hayati Alhaji Sheick Yahya Hussein

Enzi ya uhai wake kila Ijumaa katika televisheni ya Chaneli teni kipindi cha saa nne usiku alikuwa akieleza ubaya wa Freemasoni na hakuna aliyekuwa anambishia.

Alitueleza ibada zao wanavyotoa kafara za watu.
Alieleza alama wanazotumia.
Alieleza alama yao kuu ya bikali ilivyochorwa alama ya G katikati ikiwakilisha helufi ya kwanza ya mungu wao yaani god
Alieleza wanavyoficha matendo yao maovu huku wanajifanya kuonekana wazuri mbele za watu
Aliwataja pia watu mashuhuri duniani ambao ni wa imani hiyo wakiwemo badhi ya maraisi wastaafu wa Marekani

Ukibofya neno Freemasoni kwenye mtandao unakutana na ibada za kumwabudu shetani

Swali
Hayo mambo mazuri ya Freemasoni yapo wapi? au yameandikwa wapi? au yanahubiriwa wapi ?

Kwanini wenye imani hiyo wanaishia kukanusha tu wanavyosingiziwa na hawaelezi kwa uwazi hayo mazuri tuyasikie ?

Kwanini wenye imani hiyo wanajificha yaani hawawaelezi watu wawe huru kuingia kwenye ibada zao au mikutano yao bila masharti.

Kila kitu chao ni siri siri wanaogopa nini kuwa wazi na sisi tujifunze imani yao ?

Au ni kama zile biashara haramu ambazo hazitangazwi ikitaka kununua lazima uwe mwanachama, uapishwe kuficha siri ndo ununue.

Ivi kunahitajika elimu ya chekechea hapo kugundua kuwa hiyo ni biashara haramu ?

Bwana Yesu Kristo wa Nazareti alishatufundisha kitambo kwa kusema

"Mtu akiwasha taa huiweka juu ya kinara ili iangaze kote"

"Mtu akifanya matendo mema anayaweka hadharani ili kila mtu ajifunze na kisha kuyafuata kwa kuyatenda"

Ukiona mtu anasema amewasha taa yake na ameifunika ndani ya chungu ili mwanga wake usionekane.
Jiulize kuna nini hapo?

Mungu amempa binadamu zawadi moja kubwa sana ambayo inawezekana hata Malaika hawajapewa

UHURU WA KUCHAGUA MEMA NA MABAYA.

UHURU WA KUMTEGEMEA MUNGU ALIYETUUMBA AU SHETANI ALIYELAANIWA

Uko huru kufanya unachotaka kwani kwako wewe siyo kosa kufanya maamuzi yako.

Nilisikiliza hojaji moja ya familia moja inayomwabudu shetani.

Ilisema haitaki kuamrishwa na Mungu kabisa
Inataka kuwa Huru (kuwa Free)
Ikitaka kulewa inalewa, ikitaka kulaani inalaani
Ikiamua kulipiza kisasi inalipiza
Inataka kuufurahisha mwili unavyo iongiza nafsi kutenda bila mipaka

Kwetu sisi tunaye mtegemea Mungu aliyeumba Mbingu na Nchi na Bwana wetu Yesu Kristo,
tumejifunga kumfuata ili kutimiza mapenzi yake na siyo mapenzi yetu.

Mwili ukimtamani binti mrembo au mke wa mtu, nafsi inatukumbusha kuwa Mungu wetu hataki jambo hilo basi tunaizuia tamaa hiyo.

Hatuko huru kuchagua matakwa yetu
Tunachagua tuliyoagizwa tu, tukimkosea Mungu tunatubu mara moja ili atusamehe.

Lengo letu ni kumpendeza yeye tu na sio kuwa Free mason.
Hatutujui maana ya kuwa Free

Because we are not
Free to choose
(msisitizo)

But they are Free to choose
(msisitizo wa kizungu)

Samahanini niliye wakwaza ni Imani yangu tu hiyo.















.
 
Mbona kuna jambo hujajiuliza kama kuna jema kwanini waumini wake hawajitambuli shi kwenye jamii kama walivyo waislam na wakristo
Kuna interview ilifanywa pale msiban (video iko humu jf) kuwa chande kazikwa kwa imani ya kihindu
 
Back
Top Bottom