Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Kuna taarifa kuwa stesheni za SGR zitapewa majina ya marais wetu. Huu ni muendelezo wa karibu kila kitu cha maana kupewa jina la aliyekuwa Rais (hivi karibuni ni Rais aliyekuwa madarakani).
Tuna shule zinazoitwa Mkapa, Vitengo vya Hospitali vinavyoitwa Kikwete, stesheni za basi za Magufuli, Kiwanja cha ndege cha Nyerere, na sasa hivi tunajenga uwana wa michezo wa Samia Suluhu Hassan Arusha! Hivi ni wana siasa peke yao ndio walioifikisha nchi yetu hapa tulipo?
Kwa nini hizi stesheni hazikupewa majina kama Shaaban Robert (Dar es Salaam), Mbaraka Mwinshehe (Morogoro), Isike (Tabora) na mashujaa wetu wengine ambao tumewasahau! Ingekuwa nafasi nzuri yakuibua watu waliochangia historia yetu kutoka kila sehemu ambayo reli inapita. Kutumia majina ya wanasiasa kunageuza kitu ambacho watanzania wote tumechangia kuwa na sura ya kichama maana hamna mwanasiasa wa upinzani atapewa heshima kama hiyo.
Inabidi tubadilike na tuandike upya historia yetu kwa kutambua kuwa sio lazima uwe Rais ndio uthaminiwe na nchi yetu.
Amandla.
Pia, soma: Si kila jengo, eneo na barabara lazima ipewe jina la Mwanasiasa au Kiongozi. Kuna Wanamichezo na Wasanii wanaopaswa kuenziwa ili kulinda historia yetu