Kwanini tunakimbilia India kwa Tiba?

Waheshimiwa wabunge wangetusaidia sana kuhakikisha hizi hospitali zetu zinaboreshwa. Lakini inasemekana na wao wako entitled kutibiwa nje !!

that is exactly my point.. kwanza tuwakatalie hiyo "haki" waliyojipa halafu tuone watafanya nini wakiumwa.. haiwezekani hospitali ziwe mahali pa kupumzikia tu halafu hao wanatimkia SA, India, au kwingine huko.

Halafu katika wazimu wa fikra zao wanakaa na kutuambia wana mpango wa kujenga barabara za kwenda mbinguni!
 

Kwa hiyo ni halali? Ukihalalisha hivyo je wangapi wataweza maana hata serikali haina uwezo wa kuwapeleka watu wote huko India.

Mimi naona tatizo ni kua hatupo serious na mambo yetu wenyewe. Tupo pale tunacheka cheka tu na kina JK. Tunafisadiwa bado tunacheka cheka tu. Tunajua kabisa wabaya wetu ni wepi lakini bado kila mtu na zake. Madaktari, waalimu, watumishi serikalini, wanasiasa, nk hamna ayewajibika lakini bado tunaona CCM ndio jibu la tuendako.
 

MM,
Kila mtu ana vipaumbele vyake, kwa wakati wake.
Huduma za afya na elimu si vipaumbele kwa sasa. Tunaangalia namna tutakavyogharamia uchaguzi mkuu na kuongeza mabilioni mengine kwa wananchi! Ebo.



Kuna mwana JF mmoja aliniponda niliposema kwamba Mbunge Sigfrid Ng'itu alikuwa mzalendo kwa sababu "Aliugulia Muhimbili hadi mauti yalipomfika". Mheshimiwa huyu hakwenda "kutibiwa" nje!
Huenda alikuwa na sababu zake!
 

Sababu si vifaa maana Duniani hamna aliyeanza na mavifaa, ila ni taboo na siasa zetu mbovu mbovu ambazo tunafundishwa toka wadogo. N Korea wala hawana mavifaa hayo, hata India wala hawana mavifaa kama US.
 
Kuna mwana JF mmoja aliniponda niliposema kwamba Mbunge Sigfrid Ng'itu alikuwa mzalendo kwa sababu "Aliugulia Muhimbili hadi mauti yalipomfika". Mheshimiwa huyu hakwenda "kutibiwa" nje!
Huenda alikuwa na sababu zake!

IDIMI.. sidhani kukubali kuugulia bongo tu hivi hivi ni uzalendo; kwangu ni uzalendo kama angesema nia yake hiyo ya kutaka kutibiwa bongo kwa sababu hataki kutibiwa nje ya nchi. Watu wengi wanaugua na kufia bongo kwani ndiyo hali halisi. Lakini tukiwapiga marufuku hawa wanasiasa kupata "haki" ya kufanyiwa uchunguzi sijui mara mbili kwa mwaka huko majuu kwa gharama ya walipa kodi na kama wakiumwa watatibiwa mahali popote duniani.. labda wataanza kufikiria wafanye nini kuboresha sekta yetu ya afya badala ya kuwaachia wafadhili na wahisani.
 

Katika hili nani aanze kumfunga paka kengele?
 

Nakubaliana nawe MM, kinachotufanya tusiwaopige marufuku hawa vigogo kuangalia afya zao nje ya nchi ni nini hasa?
 
- Wamarekani walijifunza one thing na mambo ya kukataza ishus muhimu kwa wananchi, kwamba wananchi watatfuta njia zingine hata kuvunja sheria kupata wanachokitaka, ukiwakataza viongozi wetu kutibiwa nje kwa hela za serikali wataenda kwa hela zao na ndipo tutakapoibiwa than never before!

Respect.


FMEs!
 
Iko haja ya kuangalia upya tiba kwa viongozi wetu even check ups zifanyike hapahapa bongo ili waweze boresha sekta hii ya afya, pia tunao good doctors to do such things.
 
Sielewi unawezaje kumkataza mtu kwenda nje kwa matibabu, hii ni ndoto.
Cha muhimu ni kuongeza ubora wa Hospitali zetu ili mtu asiwe na haja ya kwenda nje.
 
We can buy Presidential Planes; we can buy the so presumed surveillance radar, but never a MRI CT Scan! Does the Gvt have a plan to strengthen Health Sector? Can’t we have even one hospital we can fully equip and make it our referral hospital instead of going to India?
 

Ndugu yangu nikuunge mkono...swala la priorities ni tatizo kubwa sana katika nchi hii.Ukiangalia suala hilo hilo la Elimu kwa mfano unaona kuwa serikali na kwa kushirikiana na wanancgi iliamua kujenga shule za sekondari katika kila kata sasa tatizo ni kuwa hizi shule si shule kwani haziko equipped katika namna yeyote ile...hazina maabara na vitu vya namna hiyo.Kwa nini tunapoamua kufanya kitu tusifanye kitu tukamaliza tukasema hapa kweli tumejenga shule na si vyumba vya madarasa...shule bila maabara,shule bila maktaba...ndo kitu gani?

Kwa upande wa hospitali ni hivyo hivyo...wanafikiri kuweka kituo cha afya au zahati sehemu inatosha....kituo kinakosa daktari,kituo kinakosa vitendea kazi kama vifaa mbalimbali yaani unashangaa.Halafu wakilala wakiamka ohhoo KILIMO KWANZA....what's the f**k....kwani kilimo kuwa agenda kubwa katika maendeleo ya hii nchi imeanza kupigiwa kelele leo?Si toka enzi za Mwalimu hili suala lipo lakini kadiri miaka inavyoenda vitendo vimeenda chini na yamebaki maneno tu kuwa KILIMO ndo uti wa mgongo wa hii nchi....UHUNI tu!

Halafu hivi karibuni nasikia wanataka kujenga barabara za kupita hewani....meeeen....tuache utani mimi nafikiri kwa kuwa tumeona hizi barabara kwenye television ila kama umewahi kutembelea nchi ya mabarabara kama hayo kwa kweli huwezi kuamini kama kwa commitment ya viongozi wa Tanzania tunaweza kupata barabara zenye viwango vya kimataifa kama hawa tunazoziona kwenye ma-TV....sioni kama hiko kitu kitatokea anytime soon!

Mwisho wa siku ni maneno tu....hii nchi tu bwana inashangaza sana....inatia uchungu mno!Sasa kama wanashindwa haya mambo madogo madogo ni lini watafikiria kufanya hospitali kubwa kama hiyo Apollo ya India wanayoifuata kila kukikichwa kwa magonjwa ya moyo?Unajua inabidi ifike mahali viongozi wetu wanapotembelea nje ya nchi wajifunze wenzao wanafanya nini....!
 
Siyo Watanzania tu wanaoenda huko. Bali hata Wamarekani, Waingereza, Wacanada na watu wa Mataifa mengine mbali mbali. Madaktari wa Kihindi wamegundua kuna biashara nzuri ya kutibu Wagonjwa. Wengine wamefunga virago toka nchi za Magaribi na kuamua kurudi kwao kufungua hospitali zenye usafi wa hali ya juu, huduma 1st class na bei poa kabisa ukilinganisha na nchi nyingi za Magharibi. Sasa wanavuna walichopanda, na niliwahi kuona CNN Wamarekani mbali mbali walioenda kutibiwa India wakihojiwa na wote walikuwa wanasifia sana huduma kule India na kubaki kuuliza kama India wanaweza kutoa huduma nzuri kiasi kile tena kwa bei poa kabisa kwanini na sisi hapa kwetu tushindwe kufanya hivyo?
 
Ndo maana hata wengine waliaanza ujasiriamali wa kuuza na kununua figo za binadamu
 
Kama wachangiaji wengi walivyo sema tatizo la Tanzania ni kukosa priorities za taifa. Niliwahi kusema kwa nini kila serikali inayoingia madarakani isiamue mfano, kusema ktk awamu yake ya kwanza ni kujenga hospitali ya kutibu magonjwa ya moyo na hilo likafanyika ktk miaka 5 ya kwanza.

Awamu ya pili ikawa ni kupeleka wanafunzi wa udaktari 2000 nje ya nchi kusoma n.k. Lakini leo utasikia maneno tu mara kilimo kwanza, mara kasi mpya n.k. vtote hivi ni porojo tu.
 

mzee sisemi wasitibiwa nje ya nchi na hata kwa gharama za serikali.. kwani naamini maisha ya mwanadamu ni lazima yaokolewe kwa gharama yoyote bila kujali kama ni mwanasiasa, maskini au tajiri. Hivyo, hatuwezi kuzuia watu wenye kutafuta tiba wasipate tiba kwa sababu hatutaki watumie fedha! La hasha.

Pointi yangu ni kuwa pasipokuweka utaratibu mzuri unaoeleweka na kukubalika tunajikuta tunatumia fedha nyingi kutengeneza na kuboresha uchumi wa nchi za watu wengine kwa mambo ambayo sisi wenyewe tunaweza kufanya.

Kwa mfano, tayari tuna utaratibu wa rufaa kuanzia hospitali za chini hadi mtu afike Muhimbili, Mbeya, Bugando na hata kwenye hospitali kadhaa teule nchini. Tayari tuna uwezo mkubwa wa vipimo vya magonja mbalimbali n.k

Haja yangu hasani kuwa kama taifa ni lazima tujenge uwezo wa ndani wa kukabiliana na magonjwa mbalimbali yanayoua watu wetu kwa wingi: Kwa mfano, mambo ya Kansa, shinikizo la damu, mshtuko, kiharusi n.k ni vitu ambavyo tunahitaji kuhakikisha tunavijengea uwezo wa ndani.

Unakumbuka yule mbunge mwaka jana ambaye alijisikia kizunguzungu Bungeni na watu wakakaa pembeni kumpepea? Au wale watoto waliokufa kwa kukosa hewa ambao walichukukuliwa nje (hakuna mtu aliyejaribu kuwapa CPR)! Sasa vitu kama hivi vinahitaji uwezo wa ndani.

Kama tungeweka utaratibu wa lazima kuwa checkups zote za kawaida zinafanyika nchini kwa mtindo wa rufaa kama ilivyo kwa wananchi wengine basi tutasaidia kutengeneza uwezo wa ndani. Pale inapofikia kuwa hali fulani kweli hatuna uwezo wa kuitibu au hatuwezi kujua kitu gani kinamsumbua mgonjwa basi ndipo tunatengeneza mtindo wa rufaa wa kwenda nje kama tunavyofanya sasa kwenye watu wenye matatizo ya moyo.

HIvi, tukijiuliza jiji la Dar, lina Trauma Center? Kwa nini kwa mfano watawala wetu wasijaribu kuwasiliana na Hospitali kama ya Chuo Kikuu cha Michigan (Ann Arbor) ambayo ni mojawapo ya leading Trauma Hospitals in US kuweza kuestablish a trauma unit angalau katika kila hospitali?

Je, tuna helikopta za dharura pale inapotokea ajali mahali ambapo tunajua barabara itachelewesha uokoaji? Nakumbuka ajali ya Akukweti pale Mbeya.. fikiria mtu amepata ajali Mbeya.. tunakimbia kumleta Dar halafu tunataka kumpeleka SA! Kwanini Mbeya hakuna Trauma Center? Nimedokeza kwa mfano kwenye suala la matetemeko ya ardhi kwamba linaweza kutoka na Rukwa ikapigwa vibaya sana.. hivi ukiangalia unaweza kuona ni watu wangapi wataumia (itakapotokea) kwa kukosa huduma ya haraka ya maumivu?

Lakini hii haitaondoa ulazima wa kumpeleka mtu nje ya nchi pale inapobidi kwa mfano ajali kubwa ambayo njia pekee ya kuokoa maisha ni kumpeleka nje n.k Kwa hiyo najaribu kuona ni jinsi gani tunaweza kuwalazimisha (siyo kuwaomba) watawala wetu kufikiria uboreshaji wa huduma ya afya nchini na njia pekee naamini ni wao wenyewe kuwa watumiaji wake!
 
Imeishapatikana hiyo short-cut kwa wenye uwezo na vyeo vya kuwawezesha kwenda kutibiwa nje itabidi ifanywe kazi ya ziada ya kuikumbusha Serikali kuharakisha utekelezaji kujengwa kwa hospitali za Rufaa za ziada, ununuzi wa vifaa vya kisasa vya tiba na mafunzo kwa watakaohusika kutumia vifaa hivyo, na kuweka utaratibu mzuri wa tiba bora ndani ya nchi kwa manufaa ya wananchi wote.

Ni muda mrefu sasa tangu nimeanza kusikia kwamba kuna mpango wa kutaka kujenga hospitali kubwa hapa nchini kwa kushirikiana na hospitali ya Apollo, India. Nasikia wazo hilo lilitolewa na uongozi wa hospitali za Apollo baada ya kuona Serikali yetu inapeleka wagonjwa wengi India. Wakashauri kwamba ili kupunguza gharama hizo wako tayari kuisaidia Serikali yetu kujenga hospitali ya aina hiyo na Apollo watatoa wataalamu kuja kuanzisha matibabu na wakati huo huo kuwafunza madaktari hapa kwetu kutumia vyombo ambavyo watakuwa hawajui namna ya kuvitumia. Labda mpango huo ungetekelezwa idadi ya watu 'kukimbilia' India ingepungua.
 
This is an industry in itself, according to some newspaper reports.
 

mpango huo upo kwa muda mrefu lakini pia ni dili ndio sababu ya kumkwamisha Dr. Masau na taasisi yake ya moyo. Nadhani kiwanja kimeshapitakana na mipango imeshaanza. Lakini lazima kwanza watafute mahali pa kula.
 


Wamarekani wanakwenda kule kwa ajili ya unafuu siyo kuwa hawana huduma hiyo kwao. watanzania wanakwenda kule kwa sababu huduma hiyo hakuna hapa Tanzania. Kama ingekuwapo ni wazi kuwa ingekuwa nafuu zaidi ya huko India.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…