- Wamarekani walijifunza one thing na mambo ya kukataza ishus muhimu kwa wananchi, kwamba wananchi watatfuta njia zingine hata kuvunja sheria kupata wanachokitaka, ukiwakataza viongozi wetu kutibiwa nje kwa hela za serikali wataenda kwa hela zao na ndipo tutakapoibiwa than never before!
Respect.
FMEs!
mzee sisemi wasitibiwa nje ya nchi na hata kwa gharama za serikali.. kwani naamini maisha ya mwanadamu ni lazima yaokolewe kwa gharama yoyote bila kujali kama ni mwanasiasa, maskini au tajiri. Hivyo, hatuwezi kuzuia watu wenye kutafuta tiba wasipate tiba kwa sababu hatutaki watumie fedha! La hasha.
Pointi yangu ni kuwa pasipokuweka utaratibu mzuri unaoeleweka na kukubalika tunajikuta tunatumia fedha nyingi kutengeneza na kuboresha uchumi wa nchi za watu wengine kwa mambo ambayo sisi wenyewe tunaweza kufanya.
Kwa mfano, tayari tuna utaratibu wa rufaa kuanzia hospitali za chini hadi mtu afike Muhimbili, Mbeya, Bugando na hata kwenye hospitali kadhaa teule nchini. Tayari tuna uwezo mkubwa wa vipimo vya magonja mbalimbali n.k
Haja yangu hasani kuwa kama taifa ni lazima tujenge uwezo wa ndani wa kukabiliana na magonjwa mbalimbali yanayoua watu wetu kwa wingi: Kwa mfano, mambo ya Kansa, shinikizo la damu, mshtuko, kiharusi n.k ni vitu ambavyo tunahitaji kuhakikisha tunavijengea uwezo wa ndani.
Unakumbuka yule mbunge mwaka jana ambaye alijisikia kizunguzungu Bungeni na watu wakakaa pembeni kumpepea? Au wale watoto waliokufa kwa kukosa hewa ambao walichukukuliwa nje (hakuna mtu aliyejaribu kuwapa CPR)! Sasa vitu kama hivi vinahitaji uwezo wa ndani.
Kama tungeweka utaratibu wa lazima kuwa checkups zote za kawaida zinafanyika nchini kwa mtindo wa rufaa kama ilivyo kwa wananchi wengine basi tutasaidia kutengeneza uwezo wa ndani. Pale inapofikia kuwa hali fulani kweli hatuna uwezo wa kuitibu au hatuwezi kujua kitu gani kinamsumbua mgonjwa basi ndipo tunatengeneza mtindo wa rufaa wa kwenda nje kama tunavyofanya sasa kwenye watu wenye matatizo ya moyo.
HIvi, tukijiuliza jiji la Dar, lina Trauma Center? Kwa nini kwa mfano watawala wetu wasijaribu kuwasiliana na Hospitali kama ya Chuo Kikuu cha Michigan (Ann Arbor) ambayo ni mojawapo ya leading Trauma Hospitals in US kuweza kuestablish a trauma unit angalau katika kila hospitali?
Je, tuna helikopta za dharura pale inapotokea ajali mahali ambapo tunajua barabara itachelewesha uokoaji? Nakumbuka ajali ya Akukweti pale Mbeya.. fikiria mtu amepata ajali Mbeya.. tunakimbia kumleta Dar halafu tunataka kumpeleka SA! Kwanini Mbeya hakuna Trauma Center? Nimedokeza kwa mfano kwenye suala la matetemeko ya ardhi kwamba linaweza kutoka na Rukwa ikapigwa vibaya sana.. hivi ukiangalia unaweza kuona ni watu wangapi wataumia (itakapotokea) kwa kukosa huduma ya haraka ya maumivu?
Lakini hii haitaondoa ulazima wa kumpeleka mtu nje ya nchi pale inapobidi kwa mfano ajali kubwa ambayo njia pekee ya kuokoa maisha ni kumpeleka nje n.k Kwa hiyo najaribu kuona ni jinsi gani tunaweza kuwalazimisha (siyo kuwaomba) watawala wetu kufikiria uboreshaji wa huduma ya afya nchini na njia pekee naamini ni wao wenyewe kuwa watumiaji wake!