Nilkuwa India karibuni kwa matibabu, self paid!!!
Afya ya mtu si mahali pa pata potea if you are serious with your health.Kama una fanya kazi basi unafanya hivyo kwa vile you are healthy.
Sekta ya afya nchini imezorota sana na si siri katika miaka 20 iliyopita.
Madaktari wanaingia mgomo, wahudumu vilevile.
Nenda Mwanyanyamala at your own risk!!
Katika siku ya leo ambapo unaweza katwa kichwa badala ya operation ya mguu is a serious problem.Tena very serious kwa Hospitali kuu nchini, MNH, Muhimbili Medical Centre.
Mgonjwa wa akili anaua wagonjwa wenziwe wodini!
Madaktari na matibabu karibu wote hawalipwi vizuri na wana miradi yao ya pembeni, concentration kazini hakuna.Daktari atafanya operation akifikiria ukata uliopo nyumbani.
Katika scenario hii mkuu MKJJ ukijipeleka Muhimbili ukiwa na kauwezo ka kujilipia , then you are not serious with your health.
Najua vizuri kuwa kupelekwa katika hospitali zetu kwa wakati mwingine ni jambo ambalo haliepukiki lakini nawahurumia sana wazalendo wenzangu.
Tufanye taratibu ku-subotage matibabu katika hizo hospitali huko nje ya nchi (kokote kule) ya wale wote wanaochota (maana hakuna kulipiwa, we can't afford it now) fedha za Taifa wakienda huko nje ya nchi. Kila sehemu huko nje ambako mlalahoi atakuwepo, kwa mfano kwenda kumtembelea na kumkashifu (kama wanavyokashifika wagonjwa wetu nchini kimatibabu) huko huko aidha kwa maandamano au individually.
Na demand ni lazima iwe wazi kwamba "NI LAZIMA ARUDISHWE AKATIBIWE MWANANYAMALA, MUHIMBILI AU BUGANDO, kama sio Peramiho au Lindi, as simple as that.
Ipi ni jinai zaidi baina ya hii na ufisadi???? Kama ni hii, basi I drop my case, lakini ufisadi ndio kichwa cha matatizo yote, umasikini, kurudi nyuma kimaendeleo, chuki na vijiko baina ya watu, nk, kwa kifupi ni uvundo. Kama atakatwa kichwa badala ya mguu, akipigwa sindano kwenye tundu ya haja kubwa badala ya takoni, shauri yake, nyumbani. Any life is sacred, we all deserve proper healthcare and the means we have are for all, not some.
Na katu hayatotokea hayo, na wanajua hivyo. Badala yake ulazima wa kuyashughulikia maslahi ya madaktari, wahudumu, na wengineo katika sekta ya afya nchini watayapa kipau inavyostahili badala ya "ufisadi" ambayo itasaidia kuboresha mapenzi, hamasa na ufanisi wa kazi zao katika kuwahudumia kwa awali kabisa wao wenyewe viongozi na kwa mapana na marefu ni kwa sisi sote wananchi. Hii kwa mtazamo mrefu itasaidia maendeleo ya sekta husika, kwa maana kama ni gunea pigs katika medical experimentations, basi sote ni guinea pigs, isitoshe ni yupi guinea pig mzuri kwa medical experimental research, fisadi aliyeshiba au mlalaho mwenye njaa???
Ni haramu kumfanyia hivyo aliyejigharimia mwenyewe bila ya pesa za ufisadi kwa maana utajiri ni kitu kitakatifu na ni dhamana na mtihani wa yule aliyemchagua Mwenyezi Mungu kumpa, autumie vizuri umuokoe na moto na autumia vibaya umsukumize motoni. Tajiri bora katika hili ata hand-pick na kuongozana na wagonjwa walalahoi wenye matatizo sawa angalau wawili au watatu, hii ndio kufuzu mtihani wa kupewa utajiri, utaendelea kufanya hivi mpaka moyo huzoea kiasi cha kutoweza kutulia bila ya kufanya hivyo na huku utajiri ukiongezeka, maana mtoaji ni Mwenyezi Mungu (SW). Lakini mafisadi viburi are worst of cteatures, filthy.
Natoa hoja.