Kwanini tunakula asubuhi baada tu ya kuamka?

Mwili wa binadam unatabia ya kuiga namna ulivyo zoweshwa.
Mimi nakula ugali na samaki/dagaa na mlenda/matembele kila asubuhi ya saa tatu, baada ya hapo nakuja kukutana na maziwa mtindi ifikapo saa nane mchana.
Inapo wadia saa kumi na mbili jioni nakula tena mlo kamili kama ni wali na asusa ama mchemsho wa ndizi na chochote, kisha saa tatu usiku nakunywa kikombe cha chai yenye hilki, tangawiz, karafuu na sukari kwambaaaali... ndipo nakuja kubarizi hapa Jf polepole hadi saa sita ndipo nalala...😊
 
Na ukiendelea kula ugali usiku halafu asubuhi unaamkia chai, supu au mtori chapati kiribatumbo hakitakuacha na mishavu yako itaendelea kuwa mikubwa kama unapuliza moto.
Labda uwe umezaliwa mlemavu tu unasingizia ugali hapa
 
Kwa kawaida mwili wa binadamu unahitaji nishati ili uwe na nguvu ya kuendelea kuwa na nguvu haijalishi unafanya kazi au hufanyi, usipokula utajukuta katika hali mbaya.
Nishati ya mwili wa binadamu hutokana na vyakula anavyokula.

Binadamu hula hasubuhi ili kupata nguvu ya kumudu na kuhimili harakati za kimaisha za kuanzia hasubuhi hadi mida ya mchana haijalishi ni kazi ngumu au nyepesi utazifanya kwa huo muda so automatically mwili utakuonyesha ishara ya uhitaji wa chakula.

Unapofika mchana mwili utahitaji chakula ili kupata nishati na nguvu ya kufanya harakati za kibinadam hadi wakati wa jioni au usiku.

Tunakula usiku ili kurejesha nguvu tuliyoipoteza kwenye shuhuli au harakati tulizozifanya katikati ya mchana na usiku.

Kiasi cha chakula ndiyo kinaweza kutofautiana kulingana na kazi tunazozifanya, mtu wa ofisini huenda akawa anakula vyakula vyepesi ili kuilinda afya yake asiwe na mafuta mengi mwili au akapata uzito mkubwa, mtu anayefanya kazi ngumu hula vyakula vizito na chakula kingi kulingana na uhitaji wa mwili wake.

Kula ni kitu muhimu kwa binadamu ndy maana hata mtoto mdogo asiyefanya kazi yeyote ni lazma ale.
 
Nilifikiri watu wanakula baada ya kuwa na njaa.
 
Nilifikiri watu wanakula baada ya kuwa na njaa.
Njaa ni indicator kuwa mwili unahitaji chakula tumbo liko empty ndy maana ya njaa, ukiipuzia utashangaa unaanza kukosa nguvu ni kama gari au piki piki mafuta yakipungua kwenye tank itatoa ishara ukiipuzia ishara chombo kitazima na Safari inaishia hapo hadi uweke mafuta tena.
 
Akilii kubwa
 
Elimu ya Janabi ni nyepesi sana, huenda wabongo wengi wana vichwa vizito tu.
yamkini upo sahihi watu wengi wanauelewa mdogo na ni walalamishi wasiopenda kuambiwa ukweli unaokwaza😂😂😂

layman hawajui hata mchakato wa kula na vipi mwili unahitaji chakula na vipi unafanya kazi ila wapo mbele wanatetea ulaji hovyo wa mavyakula yasio ya muhimu kwenye mwili.

Kuna ongezeko kubwa la vijana chini ya miaka 35 wenye ugonjwa wa presha na kisukari ila huwezi yajua hayo mpaka uwende clinic za haya magonjwa.

Siku mojamoja watz tujijengee utaratibu wa kuenda mahospitali(GEREJI ZA BINADAMU) hasa clinic za haya magonjwa ya presha na kisukari au clinic ya FIGO( DIALYSIS) kujionea huko yanayoendelea yamkini ukitoka huko utakuwa mtu wa kuachana na mitindo mibovu ya kimaisha.

Kujifunza kwa kuona ni kuzuri zaidi ya masimulizi. Muhimbili wangeanzisha tour za watu kwenda kujifunza kama wanavyoenda kutembelea mbuga za wanyama huwenda elimu ya Janabi ingepewa kipaumbele na airtime ya kutosha katika stesheni zote za TV na RADIO nchi nzima🤝
 
Umeongea vizuri, mtu anayekaa ofisini asubuhi hadi jioni ni tofauti na mbeba zege au fundi ujenzi. Milo yao na content ya milo lazima itofautiane tu.
 
Mkuu usitizame mwanga wa simu, t.v, l.e.d lights zozote atleast 1 hour kabla ya kulala.. kama ni comment ya to yeye na warembo wengne utazikuta tu ata udubu 😂😂
 
Kuna sisi tuna piga rakaa moja au rakaa mbili kwa siku
 
Kula kadiri mwili wako unavyohitaji chakula, zingatia balance diet kama hufanyi kazi ngumu na kama unauwezo wa kupangilia mlo wako.

Kama unafanya kazi ngumu na huna pesa za kukuwezesha kupata completed balance diet, Kula kinachopatikana, kikubwa uzima mana hakuna binadamu anayeweza kuishi bila chakula.

Hayo mambo ya binadamu asile ni ukichaa huwezi ishi bila chakula we fuatilia wataalam wa bongo ukauke tumbo ufe na cancer ya utumbo tunaoyoijua kama vidonda vya tumbo.

Ukiona mtu anaumwa vidonda vya tumbo ujue ni mhanga wa kupata chakula ujue anaumwa ugonjwa wa njaa, we endekeza wataalam uchwara wa Tz wakuue.

Wengine wanakushauri unywe maji hasubuhi kabla ya chochote, jaribu uone unavyotapika, wanakuambia maji ni muhimu kunywa mengi, we kunywa uone kama hutopata tatizo la maji kuzidi mwilini damu kuwa nyepesi, kila kitu kinatakiwa kwa kiwango usizidishe, wataalam wetu wanakariri machapisho ya wataalam wa nje bila uchunguzi wa kina wanatuletea na sisi.

We ishi maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…