Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda uwe umezaliwa mlemavu tu unasingizia ugali hapaNa ukiendelea kula ugali usiku halafu asubuhi unaamkia chai, supu au mtori chapati kiribatumbo hakitakuacha na mishavu yako itaendelea kuwa mikubwa kama unapuliza moto.
Nilifikiri watu wanakula baada ya kuwa na njaa.Kwa kawaida mwili wa binadamu unahitaji nishati ili uwe na nguvu ya kuendelea kuwa na nguvu haijalishi unafanya kazi au hufanyi, usipokula utajukuta katika hali mbaya.
Nishati ya mwili wa binadamu hutokana na vyakula anavyokula.
Binadamu hula hasubuhi ili kupata nguvu ya kumudu na kuhimili harakati za kimaisha za kuanzia hasubuhi hadi mida ya mchana haijalishi ni kazi ngumu au nyepesi utazifanya kwa huo muda so automatically mwili utakuonyesha ishara ya uhitaji wa chakula.
Unapofika mchana mwili utahitaji chakula ili kupata nishati na nguvu ya kufanya harakati za kibinadam hadi wakati wa jioni au usiku.
Tunakula usiku ili kurejesha nguvu tuliyoipoteza kwenye shuhuli au harakati tulizozifanya katikati ya mchana na usiku.
Kiasi cha chakula ndiyo kinaweza kutofautiana kulingana na kazi tunazozifanya, mtu wa ofisini huenda akawa anakula vyakula vyepesi ili kuilinda afya yake asiwe na mafuta mengi mwili au akapata uzito mkubwa, mtu anayefanya kazi ngumu hula vyakula vizito na chakula kingi kulingana na uhitaji wa mwili wake.
Kula ni kitu muhimu kwa binadamu ndy maana hata mtoto mdogo asiyefanya kazi yeyote ni lazma ale.
Anaongea too general.. hapohapo anasema chakuka cha jioni mwisho saa12.Inategemeana na kazi unayofanya, sijui ushauri wake huwa unamlenga nani hasa
Njaa ni indicator kuwa mwili unahitaji chakula tumbo liko empty ndy maana ya njaa, ukiipuzia utashangaa unaanza kukosa nguvu ni kama gari au piki piki mafuta yakipungua kwenye tank itatoa ishara ukiipuzia ishara chombo kitazima na Safari inaishia hapo hadi uweke mafuta tena.Nilifikiri watu wanakula baada ya kuwa na njaa.
Akilii kubwaAliwahi kuleta hoja kwamba watu wasinywe juisi ya matunda halisi, mfano machungwa.
Wengi sana tulicheka na kusema kwanini na wakati juisi ya matunda halisi ndio sahihi na ina vitamin original?
Baadaye alivyoeleza, wote tukabaki tunakubaliana naye....
Alieleza kwamba, ili kupata halisi walau inayojaa glasi moja, unapaswa kukamua machungwa si chini ya matano.... Sasa ukinywa glasi mbili asubuhi, mbili mchana na mbili jioni, jumla sita maana yake siku moja unakuwa umekula takribani machungwa 30 😁
Sasa baada ya mwezi si unakuwa unekula shamba zima? 😁 Na wakati mwili unahitaji nusu kipande tu cha chungwa!
yamkini upo sahihi watu wengi wanauelewa mdogo na ni walalamishi wasiopenda kuambiwa ukweli unaokwaza😂😂😂Elimu ya Janabi ni nyepesi sana, huenda wabongo wengi wana vichwa vizito tu.
Umeongea vizuri, mtu anayekaa ofisini asubuhi hadi jioni ni tofauti na mbeba zege au fundi ujenzi. Milo yao na content ya milo lazima itofautiane tu.Inategemea na shughuli zako
Janabi huwa anawalenga watu ambao wameajiriwa Kama yeye ambao hukaa ofisini bila kutoka jasho.
Binafsi Mimi wakati nafanya Kazi za kukaa ofisini tu .
Nilikuwa nakula mlo Kama huo anaoshauri janabi.
Ila nilipojaribu harakati za mizunguko ya hapa na pale unaondoka saa 11 na kurudi saa tano usiku
Lazima ule milo hadi minne.
Matumizi ya chakula yanategemea na ufanyaji wako wa Kazi .
Ni sawa na kuweka mafuta katika gari hauwezi mafuta ambayo hayatakufikisha destination.
Mkuu usitizame mwanga wa simu, t.v, l.e.d lights zozote atleast 1 hour kabla ya kulala.. kama ni comment ya to yeye na warembo wengne utazikuta tu ata udubu 😂😂Mwili wa binadam unatabia ya kuiga namna ulivyo zoweshwa.
Mimi nakula ugali na samaki/dagaa na mlenda/matembele kila asubuhi ya saa tatu, baada ya hapo nakuja kukutana na maziwa mtindi ifikapo saa nane mchana.
Inapo wadia saa kumi na mbili jioni nakula tena mlo kamili kama ni wali na asusa ama mchemsho wa ndizi na chochote, kisha saa tatu usiku nakunywa kikombe cha chai yenye hilki, tangawiz, karafuu na sukari kwambaaaali... ndipo nakuja kubarizi hapa Jf polepole hadi saa sita ndipo nalala...😊
NatapikaKitu cha kwanza asubuhi uamkapo ni maji kabla ya chochote kuingia mdomoni.