Kwanini tunapenda kuigana?

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Unamkaribisha mtu ndani kwako anaanza tv nzuri umenunua wapi na mimi nikainunue kochi zuri na mimi lazima nilinunue, mwingine utasikia nguo hii nzuri umenunua wapi na mimi niinunue. Hii pia iko kwenye magari ndio maana utaona ikiingia brevis kila mtu brevis, ikija crown kila mtu crown sasa hivi vanguard si wanawake si wanaume kila kona vanguard.

Tatizo nini ushamba, hatuna taste au hatuna ubunifu au uvivu wa kufikiri?
 
fashion znatuua sana
 
Dah...mimi sioni tatizo lolote hata kama wote tuna vitu vya aina moja (brand)....Ila siwezi nunua Vanguard tu kwasababu RRONDO amenunua wakati najua kabisa yeye ni ofisa wakati mimi ni mkulima ...nitanunua Kishen.....Cha msingi...Je tunanunua vitu kuwaonesha watu wengine? AU Tunanunua vitu kujiweka tofauti na wengine? AU Tunanunua vitu kukidhi mahitaji yetu?🙂
 
Labda hujaelewa, soma vizuri. Kuna,watu hawanunui kitu mpaka waone mtu mwingine kanunua. Ndio hao akikuona hata na viatu anataka umuelekeze duka akavinunue.

Pia tunaweza kununua vitu kuwaonesha watu,au kujiweka tofauti au kukidhi mahitaji. Yote yanawezekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…