Hili la kusema watu wengi hudhani kuwa benki ni kwa ajili ya watu fulani ni sahihi kabisa. Ndio maana watu wengi hawana account za bank. Lakini watu hao wengi wasio na bank accounts wana miliki simu na wanapokea na kutuma fedha kupitia accounts za simu.
Iko hivi, watu wengi hawana taarifa sahihi juu ya matumizi ya accounts za bank. Kuna rafiki zangu siku moja walikua wanang'ang'ania kuwa wataendelea kutumia CRDB kwa sababu ipo kila mahali...mimi nikawaambia sitaitumia sababu muda mwingi naishi Dar es Salaam. Je, ukienda mkoani? Nikawajibu, ni mara ngapi kwa mwaka naenda mikoani? Na nikienda hata robo mwaka haifiki narudi hapa hapa. Zaidi ntakaa week 2 tena za likizo. Kuna bank kuhamisha pesa toka bank kupeleka Tigo/voda ni bure ila kila mwisho wa mwezi unakatwa sh 250/- hata kama wamepandisha siku hizi, basi tuseme 500/- bado ni nafuu sana.
Lakini kwa nini utumie simu? Wakati kuna visa?
Kuna bank kutoa kwa visa unakatwa sh 3,000 bila kujali kiasi unachotoa. Wakati tigo kutoa laki 2 ni elfu 5. Kuna kipindi mzee alikua anaumwa kalazwa hospitali, na mimi ndio nilikua caretaker. Kuna gharama kule hospitali haziko kwenye bima, sasa ndugu na jamaa wakawa wanataka wanitumie pesa kwa simu, haki nakwambia niliwapa account yangu ya bank. Mtu akihoji niende kwa bank muda huu sijui bla bla namwambia nenda kwa wakala niwekee juat like unavyoenda kuweka tigopesa.
Ilisave sana gharama za kutolea pesa. Maana nikienda ATM navuta laki 2 mpaka 4 kwa buku wakati tigopesa ningetakiwa niwaachie elfu 10 hapo.
Cha msingi ni taarifa.