Kwanini tunapenda kutuma pesa (kwa njia ya simu) kuliko benki ambazo huwa na gharama nafuu?

Mi sipendi kabisa kutuma pesa kwa simu
Wezi sana mitandao
Kitu kizuri umeweka na kiasi,

Imagine unatoa elfu kumi wanakata 1000, ambayo ni 10% Hii si ni balaa kabisa na bado wadau wanakomaa huko huko
Mimi ukiona nimekutumia pesa kwenye simu ujue:
1. Gharama ya mimi kuja na kukupatia plus gharama ya muda ntakaotumia kuja ni kubwa kuliko gharama ya mimi kutuma na wewe kuitoa.
Au labda wewe huko uliko hakuna namna nyingine ya kupata huduma.
 
Nimejifunza kitu...sisi watu weusi hatuna hesabu za hela.
 
Bank na makampuni ya simu wanakosea kuweka Gharama Kubwa kutoka kwenye simu kwenda benki....wakiweka rate ndogo itavutia hata watu wa kipato cha chini kuweka PESA benki tena Mara kwa Mara, ndio itavutia watu kutumia Benki zaidi...mi niliacha kutumia simu kwenda bank baada ya kuona natumia pesa nyingi zaidi. ...yaan nikituma hata elfu 20,000 nakatwa 2400...
 

Benki na ATM zao hawaaminiki.
  • ATM hazijatapakaa kama mawakala kila sehemu kama unavyosema
  • Changamoto ya kutafuta usafiri kuzifikia hizo ATM zilipo ni kubwa
  • Kutotabirika kwa uwepo wa huduma kwenye ATM ni jambo jingine, unatoka mbali unafika ATM mbovu gharama kutafuta nyingine ni kubwa
  • Ni rahisi kushikana shati na wakala kama fedha haijaenda kuliko ATM
 
Kitu kizuri umeweka na kiasi,

Imagine unatoa elfu kumi wanakata 1000, ambayo ni 10% Hii si ni balaa kabisa na bado wadau wanakomaa huko huko
Hoyo 1000 ni sawa na nauli ya kwenda kuitafuta ATM ilipo
 
Hapa ndio jibu la mada lilipo. "Convenience"

Na si watu wengi wenye bank account. Kuna shughuli nilishafanya na watu 20 mikoani huko. Kati yao waliokuwa na account bank ni wawili tu lakini kila mmoja ana mzunguko wa pesa wa kuzidi sh. 300,000 kwa mwezi.
 
Nilishawahi kuhamisha pesa kutoka bank ile ilikuaga na rangi ya blue blue siku hizi wanajiita africanacity nilipigwa nikachakaa .
 
Mkuu Asante sana,nitakuwa makini haswa,hii mitandao inatuibia kijanja
 
Kwa Dar ni usumbufu ulioje kusafiri hadi benki au kwenye ATM.
Ila hata ughaibuni, kama kuna uwezekano wa kufanya malipo mitandaoni, hakuna anayesumbuka kwenda benki na gharama, iwe benki au mitandaoni ni bure kwa mlio ndani ya nchi moja, ya kimataifa unaweza kuchajiwa.
 
Wakati benki zipo watu tulikuwa tunatuma fedha kwa mabasi pesa inamfikia mtu mpk hapo kijijini

Ova
 
Yaani mara mtandao uko chini,
Mara hakuna salio,
Mara kadi imemezwa shida zote hizi za nn??
Mara foleni ukifika teller kafunga dirisha anaenda lunch...

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Niwe mkweli tu kwa sasa nimeacha kabisa kutuma pesa kutoka bank kwenda mpesa na kutoka mpesa kwenda bank hebu fikiria kutuma 1million kutoka bank kwenda mpesa ni 12k. na hapo mpesa hujaitoa. Wakati kutoa cash kwenye atm 400k max ni 1200 +vat jumla 1800, for 1m ni sh 5.2k,
 
Convenience kwa hapa Dar hujaniambia bado. Wakala wa banks wapo kila kona. Hivi unadhani kwanini banks ziliweka mawakala? Convenience
 
Bank bado zina utaratibu wa utoaji huduma wa karne 19 na hii ni karne ya 21. Accounts yako ukaifungulia dar alaf ikaja kufungwa na ukitaka kuifungua kama upo arusha itakuchukua muda mwingi hadi ije kuanza kutumika.
 
Convenience kwa hapa Dar hujaniambia bado. Wakala wa banks wapo kila kona. Hivi unadhani kwanini banks ziliweka mawakala? Convenience
Tozo za kutoa pesa kwa wakala wa benki sidhani kama zinatofautiana sana na hizi za makampuni ya simu. Wacha nilifuatilie hili kwanza.
 
Zina
Tozo za kutoa pesa kwa wakala wa benki sidhani kama zinatofautiana sana na hizi za makampuni ya simu. Wacha nilifuatilie hili kwanza.
Tofautiana sana. Tena sana. Kutoa laki 2 ni elfu 5 kwa simu. Wakati ATM au wakala wa bank haizidi elfu 2.
 
Kiongozi, Chukulia mazingira ya Dar, Jinsi ambavyo ATM ziko maeneo mengi tofauti tofauti, plus unaweza kutoa hela kwa mawakala wa huduma za kifedha kama fahari Huduma na Nmb wakala
Hivi ulishajiuliza ni waTZ wangapi wana bank akaunti na ni wangapi wana simu?

Hivi unajua waTZ wengi hawana hela ya kukaa kwenye bank akaunt? Wana hela kiasi tu na iko kwenye mzunguko daily

Pia kwa hicho hicho kidogo tunasaidiana shida zetu za hapa na pale. Mfano hela ya kula, hela ya vocha, nauli, hela ya bia n.k

Halafu mlichobugi zaidi nyie watu wa bank, kwa mawakala mmeweka chaji kubwa kuliko ndani. Tena hao Fahari huduma ndo sitaki hata kuwasikia. Yaan nyie badala muweke gharama kiduchu huku kwa mawakala ili tukimbilie huko, nyie mnatukomesha.

Na migharama yenu ya ajabu ajabu inafanya watu wachukie bank. Yaan hela zangu halafu eti kuangalia salio tu unanikata, nikitaka statement tu hata ya miamala 5 tu napo mnakata looh!!

Kwa wajanja benk zimebaki za kupokelea tu mshahara kisha natoa zote nahifadhi mahala au natumia mdogo mdogo kwenye simu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…