Kwanini tunasema hii ni awamu ya sita na si ya tano?

BISECKO

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
640
Reaction score
713
Kuna moja ya thread jukwaa hili, imeandikwa humu ikiwa na hoja ya kwamba awamu ya Sasa serikali ya Mama Samia ni ya awamu ya tano yaani muendelezo wa mtangulizi wake.

Yafuatayo ni maelezo mafupi juu yakijibu hoja hiyo.

Ni vyema kutofautisha kati ya awamu na muhula ili usipate mkanganyiko;

1. Kuingia kwa serikali na Rais mpya madarakani ni awamu nyingine.

2. Awamu moja ina mihula miwili.

3. Ukomo wa awamu ya utawala unaenda sambamba na ukomo wa muhula.

Kwa mantiki hiyo, Rais anaweza akatawala kwa muhula mmoja awamu fulani ama mihula miwili, akishindwa kuendelea na muhula mwingine kwa sababu za kikatiba na serikali mpya ikaingia madarakani, basi itahesabika awamu nyingine.

Awamu ni ile ile tu kama Rais ni yule yule.

Ukomo wa muhula/mihula wa utawala ni mwisho wa awamu ya utawala na mwanzo wa awamu nyingine.

Yatosha kusema, ukomo wa muhula wa utawala wa Magufuli ndiyo mwisho wa awamu ya tano na mwanzo wa awamu ya sita ya Mama Samia.
 
Mbona inajulikana. Kwani siku zote ulikuwa wapi? Basi nakwambia. Hii ni awamu ya sita. Awamu huenda na mtu na siyo vipindi vya uchaguzi. Nadhani umeelewa hapo mwanangu na hoja hii mod anaweza kuiondosha.
 
usipate tabu:

1) Wanaolilia kuwa hii ni awamu ya tano wengi wao hawaamini kama jpm katutoka,hawaamini kama kuna yupo atakayekuwa bora zaidi ya jpm,hawaamini kama mama anaweza kuongoza nchi ya watu 60m+ bila ya kutumia mabavu,wasiojulikana au taskforce.
wanataka waendelee kumficha mama ndani ya kivuli cha awamu ya tano ili waendelee kujifariji.

2) Kundi la pili yumo mama na wengine wote wanaoamini nchi bila magu inaenda,tena vizuri zaidi,
 
Tujipe rejea kwa kinachoendelea Zanzibar hii ni awamu ya 8 ili tuweze kuwa na mantiki kutokana na msingi huo, kwanini hii inakuwa awamu ya 6 kwa Tanzania.

Wafuatao ni marais wa Zanzibar na kila mmoja amekuwa akitambulishwa kwa awamu yake

1. 1962-72 Sheikh Abeid Karume
2. 1972-84 Aboud Jumbe
3. 1984-85 Ali Hassan Mwinyi (Mzee Mwinyi alimalizia muda wa Aboud Jumbe ila ilikuwa ni awamu ya 3 bila kufanyika uchaguzi)
4. 1985-90 Abdul Wakil
5. 1990-2000 Salim Amour
6. 2000-10 Amani Karume
7. 2010-20 Dr. Shein
8. 2020 - Dr. Hussein Mwinyi

kwa msingi huo huo kwa kuwa mwendazake hayupo na kaingia madam President HE Samia Suluhu Hassan, hii inakuwa awamu ya 6.
 
Ingewezakua awamu ya tano kama Marehemu alopita angefariki ikiwa ni chini ya miaka mitatu kabla ya awamu hii kuisha
 
...
1. Kuingia kwa serikali na Rais mpya madarakani ni awamu nyingine.

2. Awamu moja ina mihula miwili.

3. Ukomo wa awamu ya utawala unaenda sambamba na ukomo wa muhula.

Kwa mantiki hiyo, Rais anaweza akatawala kwa muhula mmoja awamu fulani ama mihula miwili, akishindwa kuendelea na muhula mwingine kwa sababu za kikatiba na serikali mpya ikaingia madarakani, basi itahesabika awamu nyingine.

Awamu ni ile ile tu kama Rais ni yule yule.

Ukomo wa muhula/mihula wa utawala ni mwisho wa awamu ya utawala na mwanzo wa awamu nyingine.

Yatosha kusema, ukomo wa muhula wa utawala wa Magufuli ndiyo mwisho wa awamu ya tano na mwanzo wa awamu ya sita ya Mama Samia.
... kama unachukulia hii nchi ni mali ya CCM hapo sawa; otherwise you're wrong! Halafu hii kitu inayoitwa "awamu" ni msamiati wa ki-CCM yafaa wabaki nao huko huko. Focus iwe Rais wa 1, 2, 3, ... etc. Hii kitu inayoitwa awamu inatuchanganya bila sababu; let's not waste time for useless things!
 
Marehemu hajafariki katika awamu hii bali awamu iliyopita.

Au unamaanisha nini?
Ipo hivi,kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano Rais aliyepo akifariki chini ya miaka mitatu kabla ya kumaliza awamu yake Makamu wa Rais anamalizia awamu hiyo..
 
Ingewezakua awamu ya tano kama Marehemu alopita angefariki ikiwa ni chini ya miaka mitatu kabla ya awamu hii kuisha
Hata kama angetawala mwezi mmoja hiyo ni awamu tosha. Samia akifariki leo tutasema awamu ya sita imedumu mwezi mmoja na tutaanza na awamu nyingine. Itoshe kusema neno awamu limesimikwa na CCM kwa maana ya kuhesabu viongozi wao!
 
Siyo kweli,kama angefariki 2023 isingekua awamu ya sita bali ya tano.
 
Kuna moja ya thread jukwaa hili, imeandikwa humu ikiwa na hoja ya kwamba awamu ya Sasa serikali ya Mama Samia ni ya awamu ya tano yaani muendelezo wa mtangulizi wake.

Yafuatayo ni maelezo mafupi juu yakijibu hoja hiyo.

Ni vyema kutofautisha kati ya awamu na muhula ili usipate mkanganyiko;

1. Kuingia kwa serikali na Rais mpya madarakani ni awamu nyingine.

2. Awamu moja ina mihula miwili.

3. Ukomo wa awamu ya utawala unaenda sambamba na ukomo wa muhula.

Kwa mantiki hiyo, Rais anaweza akatawala kwa muhula mmoja awamu fulani ama mihula miwili, akishindwa kuendelea na muhula mwingine kwa sababu za kikatiba na serikali mpya ikaingia madarakani, basi itahesabika awamu nyingine.

Awamu ni ile ile tu kama Rais ni yule yule.

Ukomo wa muhula/mihula wa utawala ni mwisho wa awamu ya utawala na mwanzo wa awamu nyingine.

Yatosha kusema, ukomo wa muhula wa utawala wa Magufuli ndiyo mwisho wa awamu ya tano na mwanzo wa awamu ya sita ya Mama Samia.
Safi sana, umeelezea vizuri. Cha kutiliwa maanani ni ile maana kwamba awamu inamuwakilisha rais mmoja.

Tunashindwa kutenganisha kati ya Muhula na Awamu.
 
Back
Top Bottom