Kwanini Tunaweka 'double consonant' Katika Majina Yetu Ya Kibongo?

Kwanini Tunaweka 'double consonant' Katika Majina Yetu Ya Kibongo?

Binafsi nawaunga mkono wachangiaji waliotoa hoja kuwa, mkazo wa matamshi ni sababu kubwa inayowafanya watu watumie konsonati mbili kwenye majina yao,kwa mfano kocha wa Simba jina lake linaandikwa Phiri, wazambia wanatumia mfumo huo wa matamshi, watanzania tukilitamka kwa kufuata mazoea yetu tunalitamka Firi, ambapo ukimsikia mzambia akitamka utamsikia katamka Piri. Swali hili,ni swala muhimi sana katika lugha za kiafrika,ni muhimu kwa taasisi zinazojishughulisha na lugha za kiafrika,kuja na utaratibu maalumu wa kuandika lugha za kiafrika kwa ufasaha na ufanisi zaidi.
 
Mkuu nafikiri tunaiga kwanu ukifatilia chimbuko ama asili ya jina lenyewe utagungua kuwa hakina double consonant....

Mara nyingi matumizi ya double consonant yanatokana na asili ya jina na mahali, mfano: Mmari, Mmole, Mmuya nk. Waganda aghalabu huwa.na double S au Z kama vile Ssemogerere, Zziwa n.k. kwa hio mie binafsi sioni shida yoyote kwa baadhi ya majina kuwa na double consonant.
 
Mara nyingi matumizi ya double consonant yanatokana na asili ya jina na mahali, mfano: Mmari, Mmole, Mmuya nk. Waganda aghalabu huwa.na double S au Z kama vile Ssemogerere, Zziwa n.k. kwa hio mie binafsi sioni shida yoyote kwa baadhi ya majina kuwa na double consonant.

Sikatai kuna wanaoiga na kuna wanaotaka majina yao yatamkike ipasavyo,ukiangalia majina ya watu ya watu wanaokaa mipakani,utagundua kuna tatizo/changamoto,mfano nchi za Malawi,Zambia,Afrika ya Kusini Zimbabwe,huongeza h kwa mfano Thabo,lakini wanatamka Tabo.Kuna jamii zilizomo kwenye nchi zaidi ya moja,jina lilelile linatamkwa vile vile,lakini linaandikwa tofauti kwenye nchi tofauti,mfano Malawi wanaandika Muthari,Mutharika,ambapo Tanzania wanaandika Mutari, Mutarika.Ni muhimu kwa taasisi zetu za lugha kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika kuja na utaratibu maalumu.Sikatai,hata lugha kama kiingereza kuna cha Uingereza,Marekani na kadhalika,na huandika tofauti.Tunachopasa kufanya ni kuweka utaratibu maalumu.
 
Nimekuwa nikifuatilia huu mjadala kwa umakini kabisa nimegundua kuwa
1.wataalam wa lugha ya kiswahili hawajachangia kabisa
2.Mtoa uzi nae hajawa wazi (hajaeleweka)
Naomba nirudi kwenye mada kwa kusema yafuatayo :

unapotumia kishazi cha kiingereza "double consonant " unaweka utata kwani hata "kwanini " ni double consonant kwamjibu wa mtoa mada! kwani herufi k imefuatana na herufi w! anachotakiwa kusema ni konsonanti / kinsoni mbili zinazofanana kufuatana!
pili naomba niweke wazi kwamba ; kiswahili kinasifa pia ya kufatana kwa konsoni mbili zinazofanana lakini hazikukubaliwa katika maandishi na Mzungu mmoja ajulikanae kwa jina Bishop Steeler katika kikao chao cha kwanza cha usanifishaji wa lugha ya kiswahili! .konsoni hizo mbili zinazo fuatana zikabaki katika matamshi tu! mifano ya maneno hayo ni mmbwa, nnge, nnzi!! lakini katika maandishi tunaandika : mbwa, nge na nzi!! kwahiyo kulalamika na kudai kuwa kiswahili hakina sifa hiyo ni upungufu wa weledi katika lugha adhimu ya kiswahili .Naomba kuwasilisha!
 
Dhana kuwa majina yakiwa Na double mfano Dennis # Denis Kizungu zaidi Kiswahili zaidi Majinana ya watu hatuna uhakika Na Consonati zao ila majina yetu ni Mara chache sana yanakuwa Na double Kwa mfano jima Chakubanga au Kimario huwezi kuweka double nanii... Labda kiubishi tu.
 
wengi wameshindwa kujibu swali. Hoja ni double consonant si identification. Hizo double zifafanue kwenye matamshi. Zaidi ya hapo ni utumwa kama kuvaa nywele bandia ili uonekane mzungu
 
Salaam Wakuu!

Uwa najiuliza, ni sababu ipi ya msingi inayofanya Wabongo kulazimisha majina yao ya Kibongo kubeba 'double consonant' kama ilivyo ktk majina ya Kizungu?
Kadri ninavyo fahamu majina mengi ya Kibongo hayana utamaduni wa kubeba 'double consonant'.

Mfano, majina kama vile:
Massawe, Muttalemwa, Mkullo, Mawalla, Lissu, Mrosso, Mollel, Marealle, Chotta, Makalla, Mgassa, Ngassa, Chollo, Ndullu, Kassanga, Mwigga, Rutta etc.

Ukichunguza utagundua kuwa ni herufi tatu hivi zinazotumika mara kwa mara (S, T & L) na mara chache herufi 'G'.

Nini hasa sababu za msingi zinazopelekea kufanya hivi? Tuelimishane tafadhali.

Ubepari tamaduni ndo sababu!
 
Hata Marekani kuna wengine Michele, wengine Michelle.

Wote nawajua, na ukiandika jina la Michele "Michelle" au Michelle "Michele" kitanuka hapo.

Sasa huko nao wanataka uzungu au vipi?

Binadamu ana hulka ya kutaka kuwa tofauti, ndiyo maana hata ma fashionista nguo ikiingia sana mtaani wanaishonea pazia.
 
Uhuru wako wa kuamua chochote hauzuii watu kutaka kujua kwanini ukaamua hivyo...... Period
Kila jambo lina sababu zake na kama kwako hazina maana kunawengine wanajali

Hakuna ubaya wowote watu kuuliza kwa madhumuni ya kutaka kujua na pia hakuna ubaya wowote kwa watu kupewa au kujipa majina wayapendayo.

Kuuliza ni jambo la kawaida sana.
 
Ndio maana ukienda congo/burundi haukuti jina la francis,joseph,laurent,vicent,michael yote yanaitwa franswa,joze,loraa,vansa na misheli so jina ni wewe utavyojiita hakuna formula ndio maana kuna bizmungu na bizmana ,salim na salum na salima,kuna Musa na Moses,kuna Jimmy na Juma,kuna Fredrick na Fred,kuna Nkurunzinza na Niyonzima na Niyonzimana!!


Mkuu, ulichokiandika wewe ni kuhusu "matamshi" ambayo kimsingi yanategemea na lugha...

Mleta uzi amechokonoa kubadili jina kutoka kwenye utamaduni wako kwenda utamaduni mwingine...mf:
François/Françoise=kifaransa
Francis=kiingereza
Jean=kifaransa
John=kiingereza....

Ni tofauti na Doto, Sita, Wasira, Lusinde n.k. ambayo kwa asili ni ya kibantu lakini huandikwa kwa mtindo wa kiingereza: Dotto, Sitta, Wassira, Lussinde n.k

Tafakari...
 
Back
Top Bottom