Mkuu nafikiri tunaiga kwanu ukifatilia chimbuko ama asili ya jina lenyewe utagungua kuwa hakina double consonant....
Mara nyingi matumizi ya double consonant yanatokana na asili ya jina na mahali, mfano: Mmari, Mmole, Mmuya nk. Waganda aghalabu huwa.na double S au Z kama vile Ssemogerere, Zziwa n.k. kwa hio mie binafsi sioni shida yoyote kwa baadhi ya majina kuwa na double consonant.
Salaam Wakuu!
Uwa najiuliza, ni sababu ipi ya msingi inayofanya Wabongo kulazimisha majina yao ya Kibongo kubeba 'double consonant' kama ilivyo ktk majina ya Kizungu?
Kadri ninavyo fahamu majina mengi ya Kibongo hayana utamaduni wa kubeba 'double consonant'.
Mfano, majina kama vile:
Massawe, Muttalemwa, Mkullo, Mawalla, Lissu, Mrosso, Mollel, Marealle, Chotta, Makalla, Mgassa, Ngassa, Chollo, Ndullu, Kassanga, Mwigga, Rutta etc.
Ukichunguza utagundua kuwa ni herufi tatu hivi zinazotumika mara kwa mara (S, T & L) na mara chache herufi 'G'.
Nini hasa sababu za msingi zinazopelekea kufanya hivi? Tuelimishane tafadhali.
Uhuru wako wa kuamua chochote hauzuii watu kutaka kujua kwanini ukaamua hivyo...... Period
Kila jambo lina sababu zake na kama kwako hazina maana kunawengine wanajali
Ndio maana ukienda congo/burundi haukuti jina la francis,joseph,laurent,vicent,michael yote yanaitwa franswa,joze,loraa,vansa na misheli so jina ni wewe utavyojiita hakuna formula ndio maana kuna bizmungu na bizmana ,salim na salum na salima,kuna Musa na Moses,kuna Jimmy na Juma,kuna Fredrick na Fred,kuna Nkurunzinza na Niyonzima na Niyonzimana!!