Kwanini tunazaliwa masikini na kufa masikini?



Nimeshalielezea hilo tuna limitations, na inategemea limitations zako, binadamu wote siyo sawa, na ndo maana kuna mtu anakaa sehemu yenye mbu hapati Malaria mwingine anapata, sasa ni kwa nini wakati wote wameumwa na mbu yule yule? Ni kwa sababu hawa watu wawili wako tofauti, bailojia yao iko tofauti, wamezaliwa tofauti na maisha yako hivyo kuna watu wanaweza kupigana na haijalishi ni vikwazo gani hata kama ni kuuuwa watauwa na kuondoa vikwazo ili waende mbele na kuna wengine hawawezi wamezaliwa hivyo ni baiologia yao, na huo ndioy ukweli wetu sisi kama Binadamu hata Wanyama wako hivyo ndo maana kuna Mbwa wakali watakuuma wengine hata uwafanye nini hawawezi kuuma watu, ni hivyo bailojia yao.
 
Kwa hiyo ww unapingana na aliesema huo msemo kuwa kuzaliwa maskini sio kosa lako bali kufa masikini ndio kosa tuambie hapa yaani wewe umekuwa mtu wa kwanza kuupinga huu msemo.
 
Umeiongelea hoja yangu ya mwisho tu.

Bado hujanipa mwanga wa nature ni nini, vigezo inavyotumia ni vipi n.k.
 
Uko sahihi kabisa mkuu matatizo ni changamoto tu ktk maisha na tunaita ni fursa pia ila kwa asiefahamu kama huyo jamaa hapo akipata matatizo atakaa chini na kulia kutwa nzima hiyo haitasaidia kuondoa hilo tatizo bali ni kuyaona kama ni sehem tu ktk maisha ya mwanadam na uone kama ni fursa tu utazivuka na utasinga mbele.
 
Kwa hiyo ww unapingana na aliesema huo msemo kuwa kuzaliwa maskini sio kosa lako bali kufa masikini ndio kosa tuambie hapa yaani wewe umekuwa mtu wa kwanza kuupinga huu msemo.


Naupinga ndiyo!
 
Uko sahihi kabisa mkuu matatizo ni changamoto tu ktk maisha na tunaita ni fursa pia ila kwa asiefahamu kama huyo jamaa hapo akipata matatizo atakaa chini na kulia kutwa nzima hiyo haitasaidia kuondoa hilo tatizo bali ni kuyaona kama ni sehem tu ktk maisha ya mwanadam na uone kama ni fursa tu utazivuka na utasinga mbele..sio sahihi kukubali kuwa kuna watu wameandikiwa kuwa maskini na wengine matajiri hapama ni juhudi zako binafsi tu..tusikatishane tamaa hapa aisee.
 
Mkuu, umeelezea vizuri kabisa, kinachotofautisha mtu masikini na asiye masikini ni juhudi na maarifa. Watu wenye juhudi na wakapata maarifa wanatoka kwenye huo mtego wa umasikini. Angalia watu kama wachagga, wakinga na wapemba. Hizi ni jamii ambazo zimeukataa umasikini, bila kujali wako katika mitego gani ya ki-umasikini watu hawa wanajuhudi kubwa na wamefanikiwa kuukataa umasikini.
 
Mbali na kuwa na elimu , jamaa was a genius alitengeneza program ya kwanza akiwa na miaka 13 tu unaweza kuona alishaanza kuukata umasikini tangu utotoni. Point of correction pia Billy Gates sio tajir was kwanza dunian kwa sasa
 
Msikie mzee wa upakoView attachment VID-20180526-WA0013.mp4
 


Mkuu Usijidanganye! Ni Kweli Matajiri Ndiyo Wanaolima Kwa Njia Za Kisasa!
Lakini Tupe Ufafanuzi Atalimaje Kuanza Kutayarisha Shamba Mpaka Kuvuna Bila Ya Kupata Wafanyakazi? Hao Wafanyakazi Ni Kina Nani Na Atawapata Wapi Wakati Tajiri Hakubali Kuwa Chini Ya Mwenziwe? Au Unataka Kuniaminisha Atapata Marobots Ya Kusimamia Shamba?

Sasa Hizo Robots Ataziendesha Nani? Najua Utasema Ni Remote Control Lakini Still Zitahitani Kucontroliwa Je atafanya Nani?

Mkuu Maskini Lazima Awepo Duniani?
Ukiniambia Ufukara Unaweza Kuondoka Basi Hapo Tutaelewana Lakini sio Umaskini.


Mfano Mdogo itazame Nchi Ya DUBAI ambao Asilimia Kubwa Raia Wake Ni Matajiri! Hivi Sasa Wanatafuta WAHINDI Na WAAFRIKA (Hata Watanzania Wako) ili Kuwatuma.
 
Kuwa mfanyakazi wa shambani Hakuna uhusiano wowote na umasikini. Unazungumzia umasikini wa level ipi? Ya kushindwa kupata mahitaji muhumi au wa kukwama kulipa private jet? Unaweza kuwa boda boda na ukawa kundi la watu wa kipato Cha Kati, umasikini wako unategemea unalinganishwa na Nan? Lakini pia hata Kama kila mtu atakuwa na uwezo wa kukidhi mahitaj muhimu,usafiri mzuri na kipato kizuri bado kutegemeana kutaendelea kuwepo as long classes zipo tuu hata baina ya matajiri hivyo labda tujenge hoja nyingine yenye mashiko. Lakini kusema inabidi kuwepo masikin hohe hahe ili hali ta kutegemeans izidi kuwepo ni hoja nyepesi sana
 
Mbali na kuwa na elimu , jamaa was a genius alitengeneza program ya kwanza akiwa na miaka 13 tu unaweza kuona alishaanza kuukata umasikini tangu utotoni. Point of correction pia Billy Gates sio tajir was kwanza dunian kwa sasa


Hakuutakataa umaskini kwa sababu kwanza hakuwa nao, kwa maana alizaliwa kwenye familia tajiri, na siyo tu baba yake hata babu yake Bill Gates alikuwa ni tajiri pia, ingawaje sijaondoa jitihada zake binafsi lkn ukweli pia ni kwamba Bill Gates hakuwa masikini na wala hakuujua umaskini!
 
Wazazi wake hawakuwa maskini Hilo NI sawa, tunamzungumzia yeye mwenyew kuamua kuanza kutafuta za kwake at 13 bila kujal nyumbani zipo au la.
 
Kwa hiyo ww unasemaje ni bora tajir wawe wengi kuliko maskini au ni bora maskini wawe wengi kuliko matajir
 
Wazazi wake hawakuwa maskini Hilo NI sawa, tunamzungumzia yeye mwenyew kuamua kuanza kutafuta za kwake at 13 bila kujal nyumbani zipo au la.


Aliwezeshwa pia usisahau hilo, haujui Wazazi wake walichangia kwa kiasi gani yeye kuwa jinsi alivyo!
 
Kwi kabisa bi hoja nyepes sana Haina mashiko basi labda nimwambie tu kuwa kama anataka maskini wawepo ili matajir wapate wa kywaajiri na kuwatuma naomba mi nisiwe ktk oridha ya hao maskini bali ktk orodha ya matajir
 
Aliwezeshwa pia usisahau hilo, haujui Wazazi wake walichangia kwa kiasi gani yeye kuwa jinsi alivyo!
In short alibebeka, sio kila mtu anaweza kubebeka na sio kila mzazi tajiri anaweza kumbeba mwanae. Nimelielezea kiasi fulani hili kwenye reason ya kwanza kabisa. Mchango wa wazaz katika mafanikio
 
In short alibebeka, sio kila mtu anaweza kubebeka na sio kila mzazi tajiri anaweza kumbeba mwanae. Nimelielezea kiasi fulani hili kwenye reason ya kwanza kabisa. Mchango wa wazaz katika mafanikio


Na ndo maana na mimi nikasema kuna limitations na siyo kila anayeshindwa kufanikiwa ni kosa lake, sasa Bill Gates alikuwa na Wazazi, alizaliwa nchi yenye kutoa nafasi n.k. hayo yote hakuyachagua bali alizaliwa na kuyakuta sasa huwezi kumlinganisha na mtoto ambaye amezaliwa Mpwapwa, wazazi wamefariki akiwa na miaka 10, ndugu wote hakuna na inabidi aje Dar kuomba omba ili aishi, hawa ni watu wawili tofauti lkn kinachowaunganisha ni kimoja wote hawakuomba hali waliozaliwa nayo hivyo wote hawana kosa, na huwezi kuwalaumu kwa kushindwa au kufanikiwa kwao bila ya kuujua undani wa maisha yao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…