Kwanini tunazaliwa masikini na kufa masikini?

Kwanini tunazaliwa masikini na kufa masikini?

Mkuu, mambo ya umasikini na masikini ninayaongea kwa umakini mkubwa sana. Maisha ya wanadamu wote yana vikwazo vikubwa. Wengi wa watu waliofanikiwa ni wale waliopambana na vikwazo vingi na kuvishinda. Siyo sahihi hata kidogo kudhani watu wenye vikwazo vingi hawataweza kuvishinda na kuondokana na umasikini. Siyo sahihi kabisa kukata tamaa au kuwakatisha tamaa watu walio kwenye mapambano ya kimaisha. Ni sehemu ya maisha ya mwanadamu kupambambana na changamoto, pale changamoto zinapotushinda sawa tunajipanga tena na kuanza upya pale tunapozishinda tunasema hewala na kuendelea. Maisha ni mapambano hakuna asiye na nafasi ya kutoka.

Nimeshalielezea hilo tuna limitations, na inategemea limitations zako, binadamu wote siyo sawa, na ndo maana kuna mtu anakaa sehemu yenye mbu hapati Malaria mwingine anapata, sasa ni kwa nini wakati wote wameumwa na mbu yule yule? Ni kwa sababu hawa watu wawili wako tofauti, bailojia yao iko tofauti, wamezaliwa tofauti na maisha yako hivyo kuna watu wanaweza kupigana na haijalishi ni vikwazo gani hata kama ni kuuuwa watauwa na kuondoa vikwazo ili waende mbele na kuna wengine hawawezi wamezaliwa hivyo ni baiologia yao, na huo ndioy ukweli wetu sisi kama Binadamu hata Wanyama wako hivyo ndo maana kuna Mbwa wakali watakuuma wengine hata uwafanye nini hawawezi kuuma watu, ni hivyo bailojia yao.
 
Siyo kweli, bado unarahisisha sana mambo, kama nilivyosema binadamu tuna limitations ambazo ziko nje ya uwezo wetu, wakati mwingine unazaliwa ktkt mazingira ambayo hayaruhusu wewe kwenda mbele, nitakupa mfano niliona ITV kuna mtoto huko kijijini ana miaka 15 wazazi wake wote wamefariki na ana wadogo zake 3 yeye tayari ni mzazi kwa wadogo zake, akienda Shuleni anatoroka hawezi kukaa kwa sababu ya njaa, pili watoto (wadogo) zake nyumbani hawana mtu, huyu mtoto ana nafasi gani ya kuja kuwa tajiri maishani mwake? Na kosa lake ni lipi? Amezaliwa ktk hayo mazingira na hizo ndiyo limitations za maisha hakuna kitu anaweza kufanya.

Kuna watu wengi sana Duniani wanakumbana na hali kama hizo hivyo usihukumu watu usiowajua kwamba kla anayekufa masikini ni kosa lake hapana, kumbuka tuna limitations ambzo ziko nje ya uwezo wetu!
Kwa hiyo ww unapingana na aliesema huo msemo kuwa kuzaliwa maskini sio kosa lako bali kufa masikini ndio kosa tuambie hapa yaani wewe umekuwa mtu wa kwanza kuupinga huu msemo.
 
Tutarudi Pale Pale Hizo Machine Ataziendesha Nani? Bakhresa Anaweza Kusimamia Mashine (Lift) Ya Kubebea Makontena?
Wazungu Hujitahidi Kutengeneza Robots Mpaka Za Ngono Lakini Mwishowake Wote Zinahitaji Muendeshaji Kwani Robot Ni Sawa Na Computer Haiwezi Kufanya Kazi Mpaka ipate Binadamu Wa Kumsimamia.

Kabla Ya Kusimamia Machine nani Atazitengeneza Hizo Mashine? Koz Tutahitani Raw Materials Zakutengenezea Mashine Amabazo Ni Chuma! Kama Sote Ni Mabilionea Nani Angelienda Mererani au Geita Kuzama Mgodini Kutafuta Chuma?

MKUU UMASIKINI NI LAZIMA UWEPO ILI DUNIA IENDE, VENGINEVYO MATAJIRI WATUPU HAWAWEZI KUISHI! ASILI YA KILA KITU HAPA DUNIANI NI MASIKINI NDIYO WANAFUATA.

MKUU MAISHA HAYAWEZI KUWA BILA YA KUWEPO NA FOOD CHAIN! In Biological System Producers Ni Plants! Lakini Katika Life System Producers Ni MASKINI.
Umeiongelea hoja yangu ya mwisho tu.

Bado hujanipa mwanga wa nature ni nini, vigezo inavyotumia ni vipi n.k.
 
Mkuu, kwanza kabisa naomba uondokane na dhana ya utajiri ukiwa unapigana vita na umasikini. Umasikini umewekewa vigezo, baadhi ya vigezo ni pamoja na kukosa huduma za msingi kama vile, makazi bora, chakula bora na maji safi na salama, matibabu na kuwa na ziada kwa ajili ya kufanya shangwe mbili tatu. Hivyo basi, usiwaze utajiri, bali jitihada zifanyike ili kuhakikisha unapata hizo huduma za msingi na muhimu na hapo utakua umeondokana na umasikini, lakini haujawa tajiri. Kwa muujibu wa mfano wako, kwangu mimi naona huyo kijana bado anayo nafasi ya kuushinda umasikini, kama anao, na kuishi maisha mazuri yeye pamoja na nduguze. Kimsingi, changamoto anazopitia huyo kijana ni fursa ya kuondokana na hali yake duni ya kimaisha. Nafasi bado anayo, na akitumia vizuri akili yake atatoka tu, kila mtu anayo nafasi ya kutoka kimaisha.
Uko sahihi kabisa mkuu matatizo ni changamoto tu ktk maisha na tunaita ni fursa pia ila kwa asiefahamu kama huyo jamaa hapo akipata matatizo atakaa chini na kulia kutwa nzima hiyo haitasaidia kuondoa hilo tatizo bali ni kuyaona kama ni sehem tu ktk maisha ya mwanadam na uone kama ni fursa tu utazivuka na utasinga mbele.
 
Kwa hiyo ww unapingana na aliesema huo msemo kuwa kuzaliwa maskini sio kosa lako bali kufa masikini ndio kosa tuambie hapa yaani wewe umekuwa mtu wa kwanza kuupinga huu msemo.

Naupinga ndiyo!
 
Mkuu, mambo ya umasikini na masikini ninayaongea kwa umakini mkubwa sana. Maisha ya wanadamu wote yana vikwazo vikubwa. Wengi wa watu waliofanikiwa ni wale waliopambana na vikwazo vingi na kuvishinda. Siyo sahihi hata kidogo kudhani watu wenye vikwazo vingi hawataweza kuvishinda na kuondokana na umasikini. Siyo sahihi kabisa kukata tamaa au kuwakatisha tamaa watu walio kwenye mapambano ya kimaisha. Ni sehemu ya maisha ya mwanadamu kupambambana na changamoto, pale changamoto zinapotushinda sawa tunajipanga tena na kuanza upya pale tunapozishinda tunasema hewala na kuendelea. Maisha ni mapambano hakuna asiye na nafasi ya kutoka.
Uko sahihi kabisa mkuu matatizo ni changamoto tu ktk maisha na tunaita ni fursa pia ila kwa asiefahamu kama huyo jamaa hapo akipata matatizo atakaa chini na kulia kutwa nzima hiyo haitasaidia kuondoa hilo tatizo bali ni kuyaona kama ni sehem tu ktk maisha ya mwanadam na uone kama ni fursa tu utazivuka na utasinga mbele..sio sahihi kukubali kuwa kuna watu wameandikiwa kuwa maskini na wengine matajiri hapama ni juhudi zako binafsi tu..tusikatishane tamaa hapa aisee.
 
Mkuu, umeelezea vizuri kabisa, kinachotofautisha mtu masikini na asiye masikini ni juhudi na maarifa. Watu wenye juhudi na wakapata maarifa wanatoka kwenye huo mtego wa umasikini. Angalia watu kama wachagga, wakinga na wapemba. Hizi ni jamii ambazo zimeukataa umasikini, bila kujali wako katika mitego gani ya ki-umasikini watu hawa wanajuhudi kubwa na wamefanikiwa kuukataa umasikini.
 
Sasa wewe unaongelea vitu 2 tofauti kabisa, kwanza kama ulimaanisha Bill Gates, Bill Gates kwanza hakuwa masikini, wazazi wake Bill Gates walikuwa ni matajiri, pili Bill Gates alichagua kutokumaliza Chuo kumbuka alikuwa anasoma Harvard aliamua kuacha baada kupata wazo la kuanzisha Kampuni lkn kama ingeshindikana angerudi kumalizia masomo huyo ni mtu ambaye alikuwa na options ktk maisha yake.

Hapa naongelea mtoto wa Kitanzania aliyezaliwa Loliondo kwenye Manyata baba mchunga ng'ombe mama ndo hivyo ana nafasi gani ya kuja kuwa tajiri leo hii? Au mtoto wa miaka 6 anayeishi Mtaani baba amefariki mama amefariki ndugu hawajulikani ana nafasi gani ya kuja kuwa tajiri?
Mbali na kuwa na elimu , jamaa was a genius alitengeneza program ya kwanza akiwa na miaka 13 tu unaweza kuona alishaanza kuukata umasikini tangu utotoni. Point of correction pia Billy Gates sio tajir was kwanza dunian kwa sasa
 
KWANINI TUNAZALIWA MASIKINI NA KUFA MASIKINI/ MAFUKARA NDIO WENYE AKILI NYINGI LAKINI BADO NI MAFUKARA.

"yuleaa ana akili Sana ni vile tu bado hajapata pakutokea". "Aah yule si anatumia tu Mali za baba yake, yani mi ningekua ndi geto yeye ningekua mbali Sana".

Hizi ni baadhi ya kauli ambazo tumekuwa tukizisikia kila siku mitaani,makazini,majumbani kwetu na sehemu zinginezo. Ni kauli ambazo zimesemwa tofauti lakini zote zikiwa na maana inayofanana, zikionyesha ni namna gani mtu mwenye hali duni kimaisha amekua akionekana mwenye akili,kujitambua,maono na mipango mizuri kwa manufaa ya maisha yake.

Lakini bahati mbaya katika jambo hili ni kwamba wengi wa masikini hawa wamekuwa wakiendelea kuishi hivyo hivyo na ndoto zao kichwani mpaka siku ya mwisho wa safari yao hapa duniani. Huku wale wanaoonekana hawana akili ya maisha wakiwa na maisha yao mazur na yakiendelea kuboreka kila kukicha.

Nini hasa tatizo,nini sababu ya watu hawa wenye akili na mawazo mazuri kushindwa kufanikiwa kimaisha? Kukosa kazi? Mshahara mdogo? Kutofahamiana na watu wenye uwezo? Au tatzo ni nini hasa? Mada hii ni pana na imezungumziwa na wahamasishaji na waandishi wengi kwa namna tofauti tofauti,ila Mimi nitajaribu kuelezea sababu chache ambazo zitakusaidia wewe unaeteseka kutaka kutoka katika ufakara huu kwa muda mrefu sasa.

1. NI JAMBO LA KIMAPOKEO

Hapa sababu hii imegawanyika Mara mbili; moja ni kutoka kwa wazazi na pili kiimani.

(i) Kutoka kwa wazazi.

Mara nyingi wazazi ndio huwafundisha na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadae. Wakati wazazi matajiri wanawaandaa watoto wao kwa kuwashirikisha katika biashara zao,kuwatambulisha katika ulimwengu wa kibiashara na kuwatengea mtaji au biashara za wao kuja kuongoza baadae. Mzazi masikini ni kipi basi anaweza kumrithisha mwanae zaidi ya elimu? Elimu inayomfanya mtoto huyu kuwa na ndoto nyingi na maono kinadharia pasi kuwa na uzoefu wowote na masuala ya fedha na kiuchumi yanavyokwenda katika dunia ya kweli. Mwandishi na mhamasishaji Robert Kiyosaki katika kitabu chake Cha Rich dady poor dady anasema "tatizo kuhusu fedha ni kwamba haifundishwi mashuleni,tunajifunza kuhusu fedha kutoka kwa wazazi wetu. Je mzazi masikini atamfunza nini mwanae kuhusu fedha?" Ni wazi kuwa mtoto huyu atakuwa akiwa hajui hili wala lile katika kutengeneza,kutunza na kufanya maamuzi ya kifedha.

Namna ya kuepuka hili ni kujaribu kuishi katika maisha ya tofauti na uliyolelewa,jichanganye na watu waliokuzidi kipato, jifunze kutoka kwao namna wanavyofanya mambo yanayohusu fedha,wanawekeza vipi na kwenye kitu gani hasa. Wanaweka vipi akiba na mahitaji yao ya kila siku wanayamudu vipi kuweza kubaki na akiba ya kufanya Mambo ya maendeleo.

(ii) Kiimani

Kutoka katika vitabu vya dini inaandikwa kwamba alienacho ataongezewa na asiye nacho atapokonywa kabisa. Hivyo hali hii ya ufukara na utajiri imekua ikijiendeleza kutoka kizazi hadi kizazi. Namna pekee ya kuepukana hili ni kupambana na kukikuza kidogo ulicho nacho. Ota ndoto Kubwa ila anza taratibu itakusaidia kustahimili matarajio yao. Usikae kusubiri siku upate hela nyingi au dili Kubwa,hapo hapo ulipo ipo ngazi ya kupandia kuelekea juu itumie kabla hajapewa mwingine.

2.SAIKOLOJIA NA IMANI KUHUSU UTAJIRI.

Kuna misemo mingi sana mitaani kuhusu fedha misemo ambayo tumekuwa tukiisikia au kuiishi wakati mwingine tangu utotoni mpaka sasa. Baadhi ya misemo hii ni Kama vile

(i) matajiri ni walafi

(ii) pesa ni uovu

(iii) huwezi kuwa tajiri kifedha na kiroho kwa pamoja

(iv) huwezi kuwa tajiri na ukawa na furaha

(v) hatuwezi nunua kile au hali yetu hairuhusu hiki.

Maneno huumba na kutufanya tuishi katika kile tunachoamini. Kama umekua ukiamini siku zote kuwa pesa ni uovu hata siku moja huwezi kufanikiwa kuwa na fedha nyingi kama usipoiondoa hiyo imani iliyojijenga ndani yako. Unaweza pata ajira nzuri ukalipwa vizuri lakini kila ukipata mshahara haukai,siku mbili umeisha,madeni yanakuzunguka majanga ni mengi unajiuliza kwanini hupati jibu,tatzo haliko mbali tatizo ni kile unachokiamini. Kwa sababu unaaamini utajiri ni uovu na wewe hutaki kuwa muovu, kila upatapo fedha nyingi ni lazima zipate matumizi ya haraka kusudi zipungue na kukuepusha na uovu Kama unavyoamini.

Hivyo nimeshakufungua macho sasa jaribu kutathimini upya imani yako kuhusu fedha,ifanyie kazi upya badili mfumo wako wa kuamini na kufanya kazi utayaona matokeo.

3.DHAMIRA YA KUYATAKA MADANIKIO NI NINI?

Mwandishi T Harvey anasema watu wengi wanaokuwa katika mazingira ya umasikini hugeuka waasi wa hali hiyo hivyo dhamira yao kuu huwa katika kufanikiwa huchochewa na uasi huu. Hali ya umasikini ni Hali inayokosesha furaha hasa pale umasikini huu unapopelekea kukosekana kwa mahitaji muhimu. Tunapozaliwa katika mazingira ya kimasikini na kubahatika kuwa na akili nyingi hukuwa tukiwa na ahadi za kupambana na kubadilisha maisha yetu na ya nyumbani. Kama ilivyo ada ukitafuta baraka huwa zinakuja siku zote. Lakini hata baada ya kupata mafanikio huwa tunajisihi bado hatuna amani,ile furaha haipo moyoni mwetu kama ambavyo tulitarajia ingekuwa. Mwisho tunayachoka maisha ya huzuni na kuona namna pekee ya kuirudisha furaha ni kujiweka mbali na utajiri. KOSA! Baada ya kuupoteza utajiri huzuni,msongo na kukosa amani huongezeka Maradufu. Kwanini? Kwa sababu tumeondoa kitu ambacho si sahihi. Tulipaswa kutafuta namna ya kuipata furaha bila kurudi kwenye umasikini. Furaha na umasikini havihusiani, Bali Ile Hali yetu ya uasi na majeraha ya umasikini mioyoni mwetu ambayo yalikua bado hayajapona ndio chimbuko la huzuni yetu.

Lakini pia kuna baadhi yetu tuliotoka kwenye maisha haya ya dhiki,tunapopambana na kuanza kuiona njia Mara nyingi huwa tunataka kufanikiwa wenyewe. Tunataka kulipiza. Hivyo Mara nyingi tunajikuta tumebaki wenyewe hakuna my katika mzunguko wetu wa kutushika mkono wakati wa uhitaji sababu tulijitenga tangu mwanzo. Happy ndipo anguko letu wengi hufuata.

Namna Bora na nzuri ya kufanikiwa ni kwa kutokula wenyewe. Hatujui maisha yatatukutanisha wapi kesho. Ni vyema kuwa na mtaji wa wema kwa kusaidia kunyanyua ndoto za wengine pale unapokua na uwezo wa kufanya hivyo. Si tu utapata thawabu kwa Mungu lakini pia unajitengenezea ngome imara hapa duniani ambayo ni ngumu kutetereka achilia mbali kuanguka kabisa.

4.CHAGUZI NA MAAMUZI YA KIFEDHA.

Mfumo wetu wa elimu kwa bahati mbaya hata kwa masomo ya kibiashara bado umefeli kugusia suala hili nyeti,usimamizi na utumiaji wa fedha. Mashuleni na vyuoni tunafundishwa namna ya kusimamia kukagua na kuzalisha fedha za mataasisi na mashirika,ila ni namna gani tunapaswa kukuza na kutumia kipato chetu hilo limesahaulika kabisa. Kama nilivyosema awali nikimnukuu Robert Kiyosaki Mambo ya fedha tunajifunza nyumbani. Kama wazazi walikua wakitumia kipato chote kwenye chakula na malazi kiasi kwamba ikitokea dharura tunaanza kukimbia kwa ndugu kuomba msaada,haitakua ajabu kama mtoto atakua hajui na haoni umuhimu was kuweka akiba.

Tunaweza kuwa tunapata kipato kinachojitosheleza lakini namna tunafanya tunavyofanya maamuzi yetu ndio tatizo. Masikini kununua shati sababu amelipenda kwake si tatizo,ila tajiri atanunua endapo tu lilikua kwenye mipango hiyo. Kwa masikini kununua simu ya toleo jipya ilihali aliyonayo ni nzima na inafanya kazi vizur haoni shida,ila tajiri atanunua simu mpya pale anapokuwa na uhitaji wa simu mpya.

Hivyo tunaweza kuwa na akili nyingi Sana za kutengeneza hela lakini matumizi yasiyo sahihi yakatudumaza na kuturudisha nyuma kila siku. Mada hii ya utunzaji na utumiaji wa fedha ni pana na muhimu Sana,nitaiongelea zaidi katika makala za mbele.

Jambo la msingi ili kudhibiti matumizi yasiyo muhimu ni kuandaa taarifa ya mahitaji yako,yalinganishe na kipato chako. Anza na yale ya muhumu hakikisha huendi nje ya ulichojiwekea hi itakusaidia kudhibiti na upotevu was hella zako katika Mambo yasiyo ya lazima.

5. KUISHI KWA KUJIOMYESHA.
Hili sitalieleza Sana sababu lipo mtaani Sana na tunaishi nalo kila siku. Tunaona namna ambavyo watu wa kipato Cha chini wamekuwa wakitumia muda na nguvu nyingi kutaka kuonyesha dunia kuwa Hali zao ni bora. Wakiweka fedha nyingi kwenye mavazi,muonekano,simu na vitu vingne vinavyozidisha umasikini wao badala ya kuwanyanyua. Wenyewe wanasema umaridadi unaficha umasikini, lakini ukweli ni kwamba umaridadi huo huo ndio unaozidi kuwadidimiza katika dimbwi Hilo la umasikini.

Natumaini makala hii fupi imekuwa msaada kwako kwa namna moja au nyingine. Pengine na wewe NI mmoja Kati ya wanaopambana kutaka kujinasua na umasikini huu Kama ilivyo wengi wetu na Leo umejifunza kitu au kuongeza kitu kwa mtazamo mwingine. Karibu kwa ushauri,nyongeza, usahihisho na pongezi pia.

Na
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SHULE YA BIASHARA.
EMAIL ; bensonflexon@gmail.com
FB ; Benson Flexon Shirima
Instagram @benitto_tz
Twitter Benittotz.
Msikie mzee wa upakoView attachment VID-20180526-WA0013.mp4
 
Kama hujui mambo unaweza taka kukubaliana na huyo jamaa lakini mi nakuunga mkono kama ukivosema kuwa siamini wala hatutakiwi kuamini kwamba kuna ambao walizaliwa ili wawe maskini bali tupambane mpaka kieleweke hizo kazi ngumu na uvuvi na kulima na zege zitafanywa na mashine au marobot si ndo kazi yao kuhusu kilima nyanya au kuvua samaki hata mayajiri wanalima kibiashara kwani anelima ni maskini tu kilimo kinataka uwe na mtaji hivo ukiwa tajiri unalima kisasa na kwa uhakika zaidi na chakula kitakuwepo hata cha kulisha duania nzima kabisa..hera ndio kila kitu buana.

Mkuu Usijidanganye! Ni Kweli Matajiri Ndiyo Wanaolima Kwa Njia Za Kisasa!
Lakini Tupe Ufafanuzi Atalimaje Kuanza Kutayarisha Shamba Mpaka Kuvuna Bila Ya Kupata Wafanyakazi? Hao Wafanyakazi Ni Kina Nani Na Atawapata Wapi Wakati Tajiri Hakubali Kuwa Chini Ya Mwenziwe? Au Unataka Kuniaminisha Atapata Marobots Ya Kusimamia Shamba?

Sasa Hizo Robots Ataziendesha Nani? Najua Utasema Ni Remote Control Lakini Still Zitahitani Kucontroliwa Je atafanya Nani?

Mkuu Maskini Lazima Awepo Duniani?
Ukiniambia Ufukara Unaweza Kuondoka Basi Hapo Tutaelewana Lakini sio Umaskini.

Mfano Mdogo itazame Nchi Ya DUBAI ambao Asilimia Kubwa Raia Wake Ni Matajiri! Hivi Sasa Wanatafuta WAHINDI Na WAAFRIKA (Hata Watanzania Wako) ili Kuwatuma.
 
Kuwa mfanyakazi wa shambani Hakuna uhusiano wowote na umasikini. Unazungumzia umasikini wa level ipi? Ya kushindwa kupata mahitaji muhumi au wa kukwama kulipa private jet? Unaweza kuwa boda boda na ukawa kundi la watu wa kipato Cha Kati, umasikini wako unategemea unalinganishwa na Nan? Lakini pia hata Kama kila mtu atakuwa na uwezo wa kukidhi mahitaj muhimu,usafiri mzuri na kipato kizuri bado kutegemeana kutaendelea kuwepo as long classes zipo tuu hata baina ya matajiri hivyo labda tujenge hoja nyingine yenye mashiko. Lakini kusema inabidi kuwepo masikin hohe hahe ili hali ta kutegemeans izidi kuwepo ni hoja nyepesi sana
 
Mbali na kuwa na elimu , jamaa was a genius alitengeneza program ya kwanza akiwa na miaka 13 tu unaweza kuona alishaanza kuukata umasikini tangu utotoni. Point of correction pia Billy Gates sio tajir was kwanza dunian kwa sasa

Hakuutakataa umaskini kwa sababu kwanza hakuwa nao, kwa maana alizaliwa kwenye familia tajiri, na siyo tu baba yake hata babu yake Bill Gates alikuwa ni tajiri pia, ingawaje sijaondoa jitihada zake binafsi lkn ukweli pia ni kwamba Bill Gates hakuwa masikini na wala hakuujua umaskini!
 
Wazazi wake hawakuwa maskini Hilo NI sawa, tunamzungumzia yeye mwenyew kuamua kuanza kutafuta za kwake at 13 bila kujal nyumbani zipo au la.
 
Mkuu Usijidanganye! Ni Kweli Matajiri Ndiyo Wanaolima Kwa Njia Za Kisasa!
Lakini Tupe Ufafanuzi Atalimaje Kuanza Kutayarisha Shamba Mpaka Kuvuna Bila Ya Kupata Wafanyakazi? Hao Wafanyakazi Ni Kina Nani Na Atawapata Wapi Wakati Tajiri Hakubali Kuwa Chini Ya Mwenziwe? Au Unataka Kuniaminisha Atapata Marobots Ya Kusimamia Shamba?

Sasa Hizo Robots Ataziendesha Nani? Najua Utasema Ni Remote Control Lakini Still Zitahitani Kucontroliwa Je atafanya Nani?

Mkuu Maskini Lazima Awepo Duniani?
Ukiniambia Ufukara Unaweza Kuondoka Basi Hapo Tutaelewana Lakini sio Umaskini.

Mfano Mdogo itazame Nchi Ya DUBAI ambao Asilimia Kubwa Raia Wake Ni Matajiri! Hivi Sasa Wanatafuta WAHINDI Na WAAFRIKA (Hata Watanzania Wako) ili Kuwatuma.
Kwa hiyo ww unasemaje ni bora tajir wawe wengi kuliko maskini au ni bora maskini wawe wengi kuliko matajir
 
Wazazi wake hawakuwa maskini Hilo NI sawa, tunamzungumzia yeye mwenyew kuamua kuanza kutafuta za kwake at 13 bila kujal nyumbani zipo au la.

Aliwezeshwa pia usisahau hilo, haujui Wazazi wake walichangia kwa kiasi gani yeye kuwa jinsi alivyo!
 
Kuwa mfanyakazi wa shambani Hakuna uhusiano wowote na umasikini. Unazungumzia umasikini wa level ipi? Ya kushindwa kupata mahitaji muhumi au wa kukwama kulipa private jet? Unaweza kuwa boda boda na ukawa kundi la watu wa kipato Cha Kati, umasikini wako unategemea unalinganishwa na Nan? Lakini pia hata Kama kila mtu atakuwa na uwezo wa kukidhi mahitaj muhimu,usafiri mzuri na kipato kizuri bado kutegemeana kutaendelea kuwepo as long classes zipo tuu hata baina ya matajiri hivyo labda tujenge hoja nyingine yenye mashiko. Lakini kusema inabidi kuwepo masikin hohe hahe ili hali ta kutegemeans izidi kuwepo ni hoja nyepesi sana
Kwi kabisa bi hoja nyepes sana Haina mashiko basi labda nimwambie tu kuwa kama anataka maskini wawepo ili matajir wapate wa kywaajiri na kuwatuma naomba mi nisiwe ktk oridha ya hao maskini bali ktk orodha ya matajir
 
Aliwezeshwa pia usisahau hilo, haujui Wazazi wake walichangia kwa kiasi gani yeye kuwa jinsi alivyo!
In short alibebeka, sio kila mtu anaweza kubebeka na sio kila mzazi tajiri anaweza kumbeba mwanae. Nimelielezea kiasi fulani hili kwenye reason ya kwanza kabisa. Mchango wa wazaz katika mafanikio
 
In short alibebeka, sio kila mtu anaweza kubebeka na sio kila mzazi tajiri anaweza kumbeba mwanae. Nimelielezea kiasi fulani hili kwenye reason ya kwanza kabisa. Mchango wa wazaz katika mafanikio

Na ndo maana na mimi nikasema kuna limitations na siyo kila anayeshindwa kufanikiwa ni kosa lake, sasa Bill Gates alikuwa na Wazazi, alizaliwa nchi yenye kutoa nafasi n.k. hayo yote hakuyachagua bali alizaliwa na kuyakuta sasa huwezi kumlinganisha na mtoto ambaye amezaliwa Mpwapwa, wazazi wamefariki akiwa na miaka 10, ndugu wote hakuna na inabidi aje Dar kuomba omba ili aishi, hawa ni watu wawili tofauti lkn kinachowaunganisha ni kimoja wote hawakuomba hali waliozaliwa nayo hivyo wote hawana kosa, na huwezi kuwalaumu kwa kushindwa au kufanikiwa kwao bila ya kuujua undani wa maisha yao!
 
Back
Top Bottom