Kwanini tunazaliwa masikini na kufa masikini?

Karibu kitaa huku hatukariri ili tujibu mtihani maisha hayana fomula yale uliyokaririshwa darasani huku hayafanyi kazi.. School start after living school
 
Kama wote wangekuwa matajiri, Dunia hiyo ingekuwaje?
Nani amtume nani?
Nani amsikilize nani?
Utegemeano ktk mazingira ungekuwepo?
Kumbuka ili uendelee kuwa tajiri inabidi ufanye kazi mkuu, kwahiyo wa kutumwa watakuepo tuu.
 
Kabla hujatuuliza nani ataenda mererani kusimamia mgodi, jiulize hao watu watapata utajiri kwa njia gani.

Kwamba mtu akishakua tajiri, basi hatofanya kazi tena? Atawezaje kuendelea kuwa tajiri?
 
Ingia you tube uangalie documetary za wa Israeli uone kama kuna mfanya kazi hata mmoja. Mtu analima ekari mia kila kitu ana operate mwenyewe kwa mashine zake

Tatizo watanzania tunazania mtu ukiwa tajiri, we kufanya kazi ndio basi tena. Kwamba we ukiwa tajiri unashindwa kuendesha mtambo wa kuvuna mahindi?
Unashindwa kuendesha mtambo wa kupandia na kuweka mbolea?
 

Wewe haya sio mawazo ya kusadikika.???
 
mkuu ufafanuzi kidogo hapa muhimu wake ni upi

Hardworking alone ll not do it, one need to be work smart as well.

Mkulima anaweza kulima Kwa jembe kila siku masaa 12 kwa mwaka mzima, akitumia mvua na mbegu za kawaidi zisizo na ubora mkubwam lakini asifanikiwe baada ya miaka 10,

Mwingine anaweza kukodisha trekta kwa wiki chache tu kwa mwaka, anatumia, mbegu bora, irrigation system, pesticides control na njia nyingine za kisasa baada ya miaka kumi watakuwa hawalingani ingawa wote ni hard workers. Namna mbili is smarter.

Networking nyingine zinakuja natural kutokana na mazingira uliyokulia, shule, vyuo ulivyosoma, place and people you hang out with.

Kijana aliyekulia Masaki, amesoma IST na Princeton University, akiwa amesoma na watoto wa viongozi, wafanyabiashara wakubwa, serious academics, captains of industries atakuwa na opportunity nyingine za kunetwork with serious people and vice versa.
 
mkuu ufafanuzi kidogo hapa muhimu wake ni upi

We all need certain luck to succeed, ukizaliwa na kukua na wazazi wawili una nafasi nzuri zaidi ukilelewa na Single parent au bila wazazi kabisa (yatima).

Sehemu uliyozaliwa, wakati ulipozaliwa, nchi uliyozaliwa, wazazi waliokuzaa, hivi vitu vyote vina impact kwenye maisha yetu ingawa ni bahati (sababu hatujapata hizi privileges kwa jitihada zetu)

Mfano: hata kama una akili sana lakini umezaliwa North Korea kwenye familia ya kawaida unaweza usifike mbali.

Mfano:- Wakati, vijana wa sasa hivi wana opportunities nyingi kujitangaza zaidi kwenye Mitandao na kujifunza mbinu nyingi jinsi ya kufanikiwa ukilinganisha vijana miaka 20,30, 40, iliyopita ambapo hata mobile phone hazikuwepo, never mind smartphone.

Unaweza kusema hata sera za serikali nazo zinaweza kuchangia kiasi fulani mafanikio yako.

Fair taxes, easy of doing business, lack of corruption, state of the market, size of the market, supportive government, quick, easy and efficient system, somehow ll affect your chances positively. Reverse is also true.
 
Hii sio sahihi, huwezi kufight kuitafuta pesa, uwe na nidhamu nayo, uwe na role model, ujifunze Mara dufu, phone book yako ijae watu wenye mchango chanya ktk biashara zako au maisha yako, marafiki zako wawe ni wale waliokuzidi na ambao ukikaa nao na kuongea nao utagain kitu halafu usitoboe! Eti uniambie Hata iweje kama nimeandikiwa umasikini nitabaki hapo hapo!! Usikatishe watu tamaa! Watu wanapambana. Mfano Erick Shigongo mbona alizaliwa ktk Lindi la umaskini wa kushindwa Hata kula Milo miwili kwa siku lkn sasa ni tajiri ana kampuni hadi marekani, hotel south Africa, Dar live, Global C.E.O huyo ni mmoja tu lkn wapo wengi!
 
the only comment that makes sense in this topic
 
Siyo rahisi kihivyo, binadamu tuna limitations, fikiria mtoto anayelala kwenye maboksi mtaani anaishi kwa kuomba omba huyu utasema ni chaguo lake kufa masikini? Ili ufanikiwe unahitaji elimu, sasa yeye elimu ataipata wapi kama hata chakula hana?
babu tunazungumzia watu wazima ambao wanaufahamu tayar uyo ni mtt kwa bahati mbya hana misingi mizuri kumfanya aweze kifa umri wa kujitambua xo nae hakishakua na kufika utu uzima nazani hii kitu hitamuusu,,,,, mtoa maana anazungumzia how unakua na maamuzi na pesa yako xo hata uyo mtt wa mtaani hakiwa mtu mzima na kushindwa kuzifanyia maamuzi mazuri pesa zake ni another case ya kukosa misingi mizuri ambayo ata mtoa mada kasema kuwa baba maskini hatamfundisha nn mtoto wake kuhusu maamuzi ya pesa hiari yeye hana pesa,
 


Hii ni kwasabadu hatuna maendeleo mjini. Kwa mfano : Ngombe tunazo tena bora zenye afya lakini viwanda vipo wapi!?
Ukulima twafanya lakini viwanda lazima tusaidiwe na jilani zetu. Serikali mwanzo ifanye jambo ndio wananchi tuimalike
[HASHTAG]#SantanosAli[/HASHTAG] Hades
[HASHTAG]#Abdirahman[/HASHTAG] Dadio
[HASHTAG]#AliDiVybz[/HASHTAG]
 
Kitabu cha 'Poverty is not natural' kimeelezea vizuri kuhusu jambo hili.


Kitafute hicho kitabu uongezee maujanja.


Umaskini siyo wa kuchekea hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…