Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha, maskini ndio wanaongiza kwa kuijaza dunia aisee.Suluhisho dhidi ya umaskini ni moja tu, Masikini asiruhusiwe kuzaa!
Kumbuka ili uendelee kuwa tajiri inabidi ufanye kazi mkuu, kwahiyo wa kutumwa watakuepo tuu.Kama wote wangekuwa matajiri, Dunia hiyo ingekuwaje?
Nani amtume nani?
Nani amsikilize nani?
Utegemeano ktk mazingira ungekuwepo?
Kabla hujatuuliza nani ataenda mererani kusimamia mgodi, jiulize hao watu watapata utajiri kwa njia gani.Tutarudi Pale Pale Hizo Machine Ataziendesha Nani? Bakhresa Anaweza Kusimamia Mashine (Lift) Ya Kubebea Makontena?
Wazungu Hujitahidi Kutengeneza Robots Mpaka Za Ngono Lakini Mwishowake Wote Zinahitaji Muendeshaji Kwani Robot Ni Sawa Na Computer Haiwezi Kufanya Kazi Mpaka ipate Binadamu Wa Kumsimamia.
Kabla Ya Kusimamia Machine nani Atazitengeneza Hizo Mashine? Koz Tutahitani Raw Materials Zakutengenezea Mashine Amabazo Ni Chuma! Kama Sote Ni Mabilionea Nani Angelienda Mererani au Geita Kuzama Mgodini Kutafuta Chuma?
MKUU UMASIKINI NI LAZIMA UWEPO ILI DUNIA IENDE, VENGINEVYO MATAJIRI WATUPU HAWAWEZI KUISHI! ASILI YA KILA KITU HAPA DUNIANI NI MASIKINI NDIYO WANAFUATA.
MKUU MAISHA HAYAWEZI KUWA BILA YA KUWEPO NA FOOD CHAIN! In Biological System Producers Ni Plants! Lakini Katika Life System Producers Ni MASKINI.
Ingia you tube uangalie documetary za wa Israeli uone kama kuna mfanya kazi hata mmoja. Mtu analima ekari mia kila kitu ana operate mwenyewe kwa mashine zakeMkuu Usijidanganye! Ni Kweli Matajiri Ndiyo Wanaolima Kwa Njia Za Kisasa!
Lakini Tupe Ufafanuzi Atalimaje Kuanza Kutayarisha Shamba Mpaka Kuvuna Bila Ya Kupata Wafanyakazi? Hao Wafanyakazi Ni Kina Nani Na Atawapata Wapi Wakati Tajiri Hakubali Kuwa Chini Ya Mwenziwe? Au Unataka Kuniaminisha Atapata Marobots Ya Kusimamia Shamba?
Sasa Hizo Robots Ataziendesha Nani? Najua Utasema Ni Remote Control Lakini Still Zitahitani Kucontroliwa Je atafanya Nani?
Mkuu Maskini Lazima Awepo Duniani?
Ukiniambia Ufukara Unaweza Kuondoka Basi Hapo Tutaelewana Lakini sio Umaskini.
Mfano Mdogo itazame Nchi Ya DUBAI ambao Asilimia Kubwa Raia Wake Ni Matajiri! Hivi Sasa Wanatafuta WAHINDI Na WAAFRIKA (Hata Watanzania Wako) ili Kuwatuma.
mkuu ufafanuzi kidogo hapa muhimu wake ni upiPlus working smart, networking and a little bit of luck.
Jiibu la Mtu Kuzaliwa Maskini Na Akafa Maskini Ni Kwa Sababu Ya NATURAL SELECTION .
Nature ikikuchagua uwe wewe basi Hata Ufight Vipi Unakuwa Huna Ujanja (Zari) Wa Kutoboa Lengo likiwa Ni Kubalance Maisha ili Tutengeze Ecosystem.
JE TUNGELIISHI WAPI?
Kwahiyo Mkuu ili SYSTEMS IBALANCE Ni Lazima NATURAL SELECTION ituchague Sisi Wengine Tuwe Maskini ili dunia iendeshwe.
mkuu ufafanuzi kidogo hapa muhimu wake ni upi
mkuu ufafanuzi kidogo hapa muhimu wake ni upi
Hii sio sahihi, huwezi kufight kuitafuta pesa, uwe na nidhamu nayo, uwe na role model, ujifunze Mara dufu, phone book yako ijae watu wenye mchango chanya ktk biashara zako au maisha yako, marafiki zako wawe ni wale waliokuzidi na ambao ukikaa nao na kuongea nao utagain kitu halafu usitoboe! Eti uniambie Hata iweje kama nimeandikiwa umasikini nitabaki hapo hapo!! Usikatishe watu tamaa! Watu wanapambana. Mfano Erick Shigongo mbona alizaliwa ktk Lindi la umaskini wa kushindwa Hata kula Milo miwili kwa siku lkn sasa ni tajiri ana kampuni hadi marekani, hotel south Africa, Dar live, Global C.E.O huyo ni mmoja tu lkn wapo wengi!Yote Uliyoyaandika Ni Miongoni Mwa Dhana Tu Na Si Reason Zinazoexist Kiuhalisia! Kiufupi Tunaita Ni Mawazo Ya Kusadikika.
Headline Ya Ulichokipost Jibu lake Ni Moja tu Whether You Want or Not.
Jiibu la Mtu Kuzaliwa Maskini Na Akafa Maskini Ni Kwa Sababu Ya NATURAL SELECTION .
Nature ikikuchagua uwe wewe basi Hata Ufight Vipi Unakuwa Huna Ujanja (Zari) Wa Kutoboa Lengo likiwa Ni Kubalance Maisha ili Tutengeze Ecosystem.
Dunia Nzima Tungelikuwa Kama Zuckerberg Nani Angelilima Viazi, Maharage, Mpunga, Nyanya, Mahindi, Salad?
Nani Angechunga Ng'ombe, Pigs, Kuku, Mbuzi, Camel Na Kondoo?
Nani Angelivua Samaki and other Marine Creatures?
Nani Angelikesha Baharini Kuendesha Cargo Ships ili Kuleta Bidhaa Hapa Kwetu?
JE TUNGELIKULA NINI?
Nani Angebeba Zege?
Nani Angelikula Unga Wa Saruji Kwa Kutengeneza Matofali?
JE TUNGELIISHI WAPI?
Kwahiyo Mkuu ili SYSTEMS IBALANCE Ni Lazima NATURAL SELECTION ituchague Sisi Wengine Tuwe Maskini ili dunia iendeshwe.
the only comment that makes sense in this topicHardworking alone ll not it, one need to smarter.
Mkulima anaweza kulima Kwa jembe kila siku masaa 12 kwa mwaka mzima, akitumia mvua na mbegu za kawaidi zisizo na ubora mkubwam lakini asifanikiwe baada ya miaka 10,
Mwingine anaweza kukodisha trekta kwa wiki chache tu kwa mwaka, anatumia, mbegu bora, irrigation system, pesticides control na njia nyingine za kisasa baada ya miaka kumi watakuwa hawalingani ingawa wote ni hard workers. Namna mbili is smarter.
Networking nyingine zinakuja natural kutokana na mazingira uliyokulia, shule, vyuo ulivyosoma, place and people you hang out with.
Kijana aliyekulia Masaki, amesoma IST na Princeton University, akiwa amesoma na watoto wa viongozi, wafanyabiashara wakubwa, serious academics, captains of industries atakuwa na opportunity nyingine za kunetwork with serious people and vice versa.
babu tunazungumzia watu wazima ambao wanaufahamu tayar uyo ni mtt kwa bahati mbya hana misingi mizuri kumfanya aweze kifa umri wa kujitambua xo nae hakishakua na kufika utu uzima nazani hii kitu hitamuusu,,,,, mtoa maana anazungumzia how unakua na maamuzi na pesa yako xo hata uyo mtt wa mtaani hakiwa mtu mzima na kushindwa kuzifanyia maamuzi mazuri pesa zake ni another case ya kukosa misingi mizuri ambayo ata mtoa mada kasema kuwa baba maskini hatamfundisha nn mtoto wake kuhusu maamuzi ya pesa hiari yeye hana pesa,Siyo rahisi kihivyo, binadamu tuna limitations, fikiria mtoto anayelala kwenye maboksi mtaani anaishi kwa kuomba omba huyu utasema ni chaguo lake kufa masikini? Ili ufanikiwe unahitaji elimu, sasa yeye elimu ataipata wapi kama hata chakula hana?
KWANINI TUNAZALIWA MASIKINI NA KUFA MASIKINI/ MAFUKARA NDIO WENYE AKILI NYINGI LAKINI BADO NI MAFUKARA.
"yuleaa ana akili Sana ni vile tu bado hajapata pakutokea". "Aah yule si anatumia tu Mali za baba yake, yani mi ningekua ndi geto yeye ningekua mbali Sana".
Hizi ni baadhi ya kauli ambazo tumekuwa tukizisikia kila siku mitaani,makazini,majumbani kwetu na sehemu zinginezo. Ni kauli ambazo zimesemwa tofauti lakini zote zikiwa na maana inayofanana, zikionyesha ni namna gani mtu mwenye hali duni kimaisha amekua akionekana mwenye akili,kujitambua,maono na mipango mizuri kwa manufaa ya maisha yake.
Lakini bahati mbaya katika jambo hili ni kwamba wengi wa masikini hawa wamekuwa wakiendelea kuishi hivyo hivyo na ndoto zao kichwani mpaka siku ya mwisho wa safari yao hapa duniani. Huku wale wanaoonekana hawana akili ya maisha wakiwa na maisha yao mazur na yakiendelea kuboreka kila kukicha.
Nini hasa tatizo,nini sababu ya watu hawa wenye akili na mawazo mazuri kushindwa kufanikiwa kimaisha? Kukosa kazi? Mshahara mdogo? Kutofahamiana na watu wenye uwezo? Au tatzo ni nini hasa? Mada hii ni pana na imezungumziwa na wahamasishaji na waandishi wengi kwa namna tofauti tofauti,ila Mimi nitajaribu kuelezea sababu chache ambazo zitakusaidia wewe unaeteseka kutaka kutoka katika ufakara huu kwa muda mrefu sasa.
1. NI JAMBO LA KIMAPOKEO
Hapa sababu hii imegawanyika Mara mbili; moja ni kutoka kwa wazazi na pili kiimani.
(i) Kutoka kwa wazazi.
Mara nyingi wazazi ndio huwafundisha na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadae. Wakati wazazi matajiri wanawaandaa watoto wao kwa kuwashirikisha katika biashara zao,kuwatambulisha katika ulimwengu wa kibiashara na kuwatengea mtaji au biashara za wao kuja kuongoza baadae. Mzazi masikini ni kipi basi anaweza kumrithisha mwanae zaidi ya elimu? Elimu inayomfanya mtoto huyu kuwa na ndoto nyingi na maono kinadharia pasi kuwa na uzoefu wowote na masuala ya fedha na kiuchumi yanavyokwenda katika dunia ya kweli. Mwandishi na mhamasishaji Robert Kiyosaki katika kitabu chake Cha Rich dady poor dady anasema "tatizo kuhusu fedha ni kwamba haifundishwi mashuleni,tunajifunza kuhusu fedha kutoka kwa wazazi wetu. Je mzazi masikini atamfunza nini mwanae kuhusu fedha?" Ni wazi kuwa mtoto huyu atakuwa akiwa hajui hili wala lile katika kutengeneza,kutunza na kufanya maamuzi ya kifedha.
Namna ya kuepuka hili ni kujaribu kuishi katika maisha ya tofauti na uliyolelewa,jichanganye na watu waliokuzidi kipato, jifunze kutoka kwao namna wanavyofanya mambo yanayohusu fedha,wanawekeza vipi na kwenye kitu gani hasa. Wanaweka vipi akiba na mahitaji yao ya kila siku wanayamudu vipi kuweza kubaki na akiba ya kufanya Mambo ya maendeleo.
(ii) Kiimani
Kutoka katika vitabu vya dini inaandikwa kwamba alienacho ataongezewa na asiye nacho atapokonywa kabisa. Hivyo hali hii ya ufukara na utajiri imekua ikijiendeleza kutoka kizazi hadi kizazi. Namna pekee ya kuepukana hili ni kupambana na kukikuza kidogo ulicho nacho. Ota ndoto Kubwa ila anza taratibu itakusaidia kustahimili matarajio yao. Usikae kusubiri siku upate hela nyingi au dili Kubwa,hapo hapo ulipo ipo ngazi ya kupandia kuelekea juu itumie kabla hajapewa mwingine.
2.SAIKOLOJIA NA IMANI KUHUSU UTAJIRI.
Kuna misemo mingi sana mitaani kuhusu fedha misemo ambayo tumekuwa tukiisikia au kuiishi wakati mwingine tangu utotoni mpaka sasa. Baadhi ya misemo hii ni Kama vile
(i) matajiri ni walafi
(ii) pesa ni uovu
(iii) huwezi kuwa tajiri kifedha na kiroho kwa pamoja
(iv) huwezi kuwa tajiri na ukawa na furaha
(v) hatuwezi nunua kile au hali yetu hairuhusu hiki.
Maneno huumba na kutufanya tuishi katika kile tunachoamini. Kama umekua ukiamini siku zote kuwa pesa ni uovu hata siku moja huwezi kufanikiwa kuwa na fedha nyingi kama usipoiondoa hiyo imani iliyojijenga ndani yako. Unaweza pata ajira nzuri ukalipwa vizuri lakini kila ukipata mshahara haukai,siku mbili umeisha,madeni yanakuzunguka majanga ni mengi unajiuliza kwanini hupati jibu,tatzo haliko mbali tatizo ni kile unachokiamini. Kwa sababu unaaamini utajiri ni uovu na wewe hutaki kuwa muovu, kila upatapo fedha nyingi ni lazima zipate matumizi ya haraka kusudi zipungue na kukuepusha na uovu Kama unavyoamini.
Hivyo nimeshakufungua macho sasa jaribu kutathimini upya imani yako kuhusu fedha,ifanyie kazi upya badili mfumo wako wa kuamini na kufanya kazi utayaona matokeo.
3.DHAMIRA YA KUYATAKA MADANIKIO NI NINI?
Mwandishi T Harvey anasema watu wengi wanaokuwa katika mazingira ya umasikini hugeuka waasi wa hali hiyo hivyo dhamira yao kuu huwa katika kufanikiwa huchochewa na uasi huu. Hali ya umasikini ni Hali inayokosesha furaha hasa pale umasikini huu unapopelekea kukosekana kwa mahitaji muhimu. Tunapozaliwa katika mazingira ya kimasikini na kubahatika kuwa na akili nyingi hukuwa tukiwa na ahadi za kupambana na kubadilisha maisha yetu na ya nyumbani. Kama ilivyo ada ukitafuta baraka huwa zinakuja siku zote. Lakini hata baada ya kupata mafanikio huwa tunajisihi bado hatuna amani,ile furaha haipo moyoni mwetu kama ambavyo tulitarajia ingekuwa. Mwisho tunayachoka maisha ya huzuni na kuona namna pekee ya kuirudisha furaha ni kujiweka mbali na utajiri. KOSA! Baada ya kuupoteza utajiri huzuni,msongo na kukosa amani huongezeka Maradufu. Kwanini? Kwa sababu tumeondoa kitu ambacho si sahihi. Tulipaswa kutafuta namna ya kuipata furaha bila kurudi kwenye umasikini. Furaha na umasikini havihusiani, Bali Ile Hali yetu ya uasi na majeraha ya umasikini mioyoni mwetu ambayo yalikua bado hayajapona ndio chimbuko la huzuni yetu.
Lakini pia kuna baadhi yetu tuliotoka kwenye maisha haya ya dhiki,tunapopambana na kuanza kuiona njia Mara nyingi huwa tunataka kufanikiwa wenyewe. Tunataka kulipiza. Hivyo Mara nyingi tunajikuta tumebaki wenyewe hakuna my katika mzunguko wetu wa kutushika mkono wakati wa uhitaji sababu tulijitenga tangu mwanzo. Happy ndipo anguko letu wengi hufuata.
Namna Bora na nzuri ya kufanikiwa ni kwa kutokula wenyewe. Hatujui maisha yatatukutanisha wapi kesho. Ni vyema kuwa na mtaji wa wema kwa kusaidia kunyanyua ndoto za wengine pale unapokua na uwezo wa kufanya hivyo. Si tu utapata thawabu kwa Mungu lakini pia unajitengenezea ngome imara hapa duniani ambayo ni ngumu kutetereka achilia mbali kuanguka kabisa.
4.CHAGUZI NA MAAMUZI YA KIFEDHA.
Mfumo wetu wa elimu kwa bahati mbaya hata kwa masomo ya kibiashara bado umefeli kugusia suala hili nyeti,usimamizi na utumiaji wa fedha. Mashuleni na vyuoni tunafundishwa namna ya kusimamia kukagua na kuzalisha fedha za mataasisi na mashirika,ila ni namna gani tunapaswa kukuza na kutumia kipato chetu hilo limesahaulika kabisa. Kama nilivyosema awali nikimnukuu Robert Kiyosaki Mambo ya fedha tunajifunza nyumbani. Kama wazazi walikua wakitumia kipato chote kwenye chakula na malazi kiasi kwamba ikitokea dharura tunaanza kukimbia kwa ndugu kuomba msaada,haitakua ajabu kama mtoto atakua hajui na haoni umuhimu was kuweka akiba.
Tunaweza kuwa tunapata kipato kinachojitosheleza lakini namna tunafanya tunavyofanya maamuzi yetu ndio tatizo. Masikini kununua shati sababu amelipenda kwake si tatizo,ila tajiri atanunua endapo tu lilikua kwenye mipango hiyo. Kwa masikini kununua simu ya toleo jipya ilihali aliyonayo ni nzima na inafanya kazi vizur haoni shida,ila tajiri atanunua simu mpya pale anapokuwa na uhitaji wa simu mpya.
Hivyo tunaweza kuwa na akili nyingi Sana za kutengeneza hela lakini matumizi yasiyo sahihi yakatudumaza na kuturudisha nyuma kila siku. Mada hii ya utunzaji na utumiaji wa fedha ni pana na muhimu Sana,nitaiongelea zaidi katika makala za mbele.
Jambo la msingi ili kudhibiti matumizi yasiyo muhimu ni kuandaa taarifa ya mahitaji yako,yalinganishe na kipato chako. Anza na yale ya muhumu hakikisha huendi nje ya ulichojiwekea hi itakusaidia kudhibiti na upotevu was hella zako katika Mambo yasiyo ya lazima.
5. KUISHI KWA KUJIOMYESHA.
Hili sitalieleza Sana sababu lipo mtaani Sana na tunaishi nalo kila siku. Tunaona namna ambavyo watu wa kipato Cha chini wamekuwa wakitumia muda na nguvu nyingi kutaka kuonyesha dunia kuwa Hali zao ni bora. Wakiweka fedha nyingi kwenye mavazi,muonekano,simu na vitu vingne vinavyozidisha umasikini wao badala ya kuwanyanyua. Wenyewe wanasema umaridadi unaficha umasikini, lakini ukweli ni kwamba umaridadi huo huo ndio unaozidi kuwadidimiza katika dimbwi Hilo la umasikini.
Natumaini makala hii fupi imekuwa msaada kwako kwa namna moja au nyingine. Pengine na wewe NI mmoja Kati ya wanaopambana kutaka kujinasua na umasikini huu Kama ilivyo wengi wetu na Leo umejifunza kitu au kuongeza kitu kwa mtazamo mwingine. Karibu kwa ushauri,nyongeza, usahihisho na pongezi pia.
Na
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SHULE YA BIASHARA.
EMAIL ; bensonflexon@gmail.com
FB ; Benson Flexon Shirima
Instagram @benitto_tz
Twitter Benittotz.