mwambaasilia
Member
- May 12, 2023
- 68
- 143
Wasalaam katika Jina la Mwenyezi Mungu....
Moja kwa moja kwenye mada...
Tupo duniani kwa Neema ya Mwenyezi Mungu (upendo wake kwetu).
Tupo duniani ili kumpendeza yeye aliyetuumba na kutii maagizo yake.... shetani (malaika aliyeasi)alikuwepo kabla ya kuumbwa sisi wanadamu, akamusi Mungu na kufukuzwa mbinguni.
Mwenyezi Mungu akatuumba na kutuweka duniani ili pawe kipimo kwetu, ndiyo maana akaweka mti wa ujuzi wa mema na mabaya katika bustani kabla ya kufukuzwa.
Kama ingetokea Adamu na mkewe kutokula matunda ya mti huo wangekuwa wamefanikiwa katika jaribu lao, kwa kuitii sauti na maagizo ya Mungu. Kwa kuwa walifeli ndiyo maana tunaendelea kuwa katika kipimo hapa duniani.
Tupo duniani ili kupimwa katika matendo na imani yetu juu ya Mwenyezi Mungu, kama tunamtii yeye au shetani na mambo yake.
Hivyo duniani ndipo kipimo chetu kilipo, kabla ya kwenda peponi (raha ya milele pamoja na Mungu) au jehanamu (matesoni pamoja na shetani)
Tuwapo hapa duniani njia ni mbili tu, ni kwamba upo upande wa Mungu au shetani... hakuna zaidi ya hapo...amua leo, ni njia gani upo.
Maisha baada ya kifo yapo... kama wachawi waendapo kuwanga huuacha mwili wa nyama na damu na kuwa katika mwili wa roho.
Itashindikana vipi kwa Mungu kwa yote tuahidiwayo baada ya maisha ya hapa duniani.
Niwatakie maamuzi mema...