Kwanini tupo hapa

Kwanini tupo hapa

Joshua Haji

Senior Member
Joined
Nov 4, 2011
Posts
108
Reaction score
20
Kwanini Ujamaa wa Azimio la Arusha 1967 umetucost,Unajua timing ya Ujamaa wa Mwalimu ilikuja baada ya Mahusiano ya Kimataifa baina yetu na Wingereza kuharibika 1965' hii ilitokana na fact kwamba Nyerere aliamini kuikomboa kwanza Afrika YOTE ndio awe na uhakika na maendeleo yetu..kwanini?jibu ni dogo tu.Mataifa makubwa bado yalikuwa yanainyonya Afrika, so presha za Ukoloni mamboleo,kupitia mamluki ambao wangeweza kuwapa silaha watu wako mwenyewe waingie msituni kukupindua, vita baridi ya Ubepari na Ujamaa wa Urusi sambamba na Ucommunisti wa Mchina,hivi vyote vilikuwa ni changamoto.

Hofu kubwa sana Nyerere aliipata sababu hakuna mtu mweusi aliekuwa amezoea kujitawala katikati ya miongo mingi ya ubabe wa Mataifa ya magharibi kwa Nchi za Afrika,Matokeo ya vita kuu mbili za Dunia zilizoleta mabadiliko ya kinguvu kwenye Dunia ya kwanza na kuzingatia kwamba hata Mipaka ya Nchi zetu ni Mkoloni aliyeichora kwahiyo kijasusi anatujua fika.

Unataka kujiuliza kwanini pengine Nyerere alikuwa tayari kupigania sana ukombozi wa nchi za Kusini mwa Africa mpaka kufikia kuitwa Frontline State?Jibu ni dogo tu,Hakuwa na Uhakika kama uhuru tuliokuwa nao ulikuwa wa kugushi au kweli.Bado una Waingereza wanaishi nchini kwako,wanamiliki mashamba na wengine ujuzi wao mnauhitaji kuendesha Nchi huku majirani zako wengine bado wanaishi na Mkoloni,unashuhudia wakipewa Uhuru wa Bendera huku Umoja wa Mataifa na OAU wapo ila hawana nguvu za kuamua basi Afrika nzima iwe huru tu tuachane na suala zima la Ukoloni.

Kufuatia Uhuru wa bendera ama Universal Declaration of Independence pale Rhodesia ,Nyerere akaona ,ebo!hawa Waingereza wanabariki nini??kupambana na kukataa ukandamizaji, Serikali ya Wingereza Kupitia Common Wealth inaamua kukata misaada kwa Tanzania €15mil ambayo iliokuwa njiani tayari,ni dhahiri kwamba TANU na wananchi wasingemuelewa Mwl.Nyerere kama kikwazo hicho cha Uchumi kingefunika Msimamo wake juu ya Zimbabwe na Afrika ya Kusini si ndio Miaka miwili baadae Azimio la Arusha lenye misingi ya Ujamaa na Siasa za Uchumi wa Kujitegemea zinazaliwa

kumbuka hapo Mahusiano ya Kimataifa baina ya Tanzania na Wingereza yalikuwa mabaya sana!!!!Huku Wingereza ana mahasimu wakubwa ambao kupitia Common Wealth angetetea makoloni yake yote aliyoyapatia Uhuru sababu vidonda vya Vita kuu mbili za Dunia bado vilikuwa vibichi,sasa Nyerere anaelekea kuchafua hali hiyo kwa washirika wake wengine ambao wangefollow Suit juu ya msimamo huo sababu Tanzania ilikuwa Taifa kaka kwa mataifa mengine machanga ya Afrika, hivyo basi sakata la Tanzania kuwa kinyume na Mkoloni wao wa zamani Wingereza juu ya Uhuru wa Rhodesia na Uuzaji wao wa silaha pale South Africa kwa kigezo kwamba kuna hofu ya Urusi kuiteka bahari ya Hindi na siasa zake za Ujamaa vilichochea hisia hasi upande wa Westminster...

Nyerere alijiamini sana,kwenye awamu yake ya kwanza katika kipindi cha 1967-75 tunaweza kukubali kwamba mambo yalikuwa safi sana sababu serikali ya TANU sasa ingeweza kutaifisha Uchumi wote, takribani Asasi za Serikali ikiwa ni Mashirika ya umma yalifikia 400;afya ilikua,elimu na ajira havikuwa tatizo kabisa hadi kufikia mnamo mwaka 1977 TANU na ASP kuungana na kuzaa CCM,basi Nyerere alijihakikishia ushawishi wa nguvu wa kudumu wa Chama hichi mkombozi.Kama zilivyokuwa serikali zote zilizoleta Uhuru,viongozi wake hawakuwa na mpango wa haraka wakuachia madaraka haswa Nchi zote washiriki wa Siasa za Ujamaa kujisahau ndio ikawa tanzi kuu kwao.

Nyerere alifeli sana kwenye Ujamaa kwa upande wa Kuleta maendeleo endelevu,muitikio wa kukua kwa Uchumi kwenye awamu za mwanzo za ujamaa haikuwa na maana kwamba Ujamaa ulikuwa ndio mpango kabambe uliokidhi mahitaji ya Taifa letu la hasha,bali mabadiliko ya ghafla yalikuwa mazuri lakini baada ya muda, uchumi ulivyojiadjust ni dhahiri kwamba mahesabu hayakukaa vizuri,yaani kwa Kiswahili rahisi kwa Mtu asiejua Uchumi kabisa ,Nchi iligawa Uchumi zaidi ya ilivyoweza kukusanya.Kimsingi gawio hilo halikutokana na mali za ndani tu,bali Mikopo na Misaada kutoka Nje vilikuwa na nafasi yake.Kipindi chote cha miaka 13 ya Ujamaa,Tanzania ilikuwa imechukua fedha kutoka mataifa yaliyofikia 40.Sasa Pamba ,Karafuu na mazao mengine ndio vilikuwa vyanzo vikuu vya biashara nje ya mipaka yetu kwenye Soko la Dunia.

Sijui ni bahati mbaya,sijui ni ule msemo kwamba N'gombe wa maskini hazai,lakini Ujamaa wa Nyerere ukaja kuwa Kitanzi chake Mwalimu kwani hata kipindi anaachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe tafsiri nzuri ya msomi yoyote anaweza kusema ni dhahiri kuwa aliletwa chini kabisa na mawazo yake ambayo vijana waliyaamini mpaka wakatembea kwa mchakamchaka toka mikoa ya mbali mpaka Arusha kuunga mkono Azimio la Arusha,kama alivyokuwa nabii Franklin Roosevelt wa Marekani na "New Deal" Kufikia 1985 Ujamaa ulikuwa umetufikisha mahali pabaya na Pagumu mno,pengine wasomi wanaweza kuhoji,Je Nyerere aliamua tu Kuachia madaraka au ni kwamba ingekuwa ngumu kurudi kwa Wananchi na kuwaambia kwamba Azimio la Arusha halikuwa mkombozi wetu na kwamba nilikosea ama Utatafuta sehemu ya kulaumu kushindwa kwake ,je yote haya ungemaliza kuyaelezea na kupendekeza Azimio jingine ambalo tungelifuata?tukuamini tena kweli?

Kwanini tunasema kwamba N'gombe wa masikini hazai?tatizo la Uchumi wa dunia ya tatu ni moja tu,"Umefungwa sambamba na dunia ya Kwanza"
Sio kama namalaumu ama kumkejeli Baba wa Taifa,Azimio la Arusha lilikuwa ni wazo zuri sana. Pamoja na kufeli kwake lilituletea Umoja,vile vijiji viliondoa kabisa ukabila na uwezekano wowote wa kushindwa kwetu kuwa wazalendo,Mapenzi ya mtu na nchi yake yalikuwa makubwa sana matabaka yakawa ni hadithi za nchi jirani kiufupi Umoja wa kitaifa ndio ulikuwa wimbo wetu.

Kurudi kwenye matukio yaliyotokea hadi kupelekea kushindwa vibaya kwa Baba wa Taifa na Ujamaa,

"Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi, mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na tusipuuzwe tena " (Nyerere feb1967)

Utafikiri Dunia ilikuwa inampinga Baba wa Taifa na jitihada zake za kutujengea uchumi imara,January 1967 wakati tunatangaza kujikita na Ujamaa miezi Minne baadae Urusi inatoa taarifa tetesi za kijasusi kwa Misri na Syria juu ya kile kilichoitwa "Uvamizi wa Israel kwenye maeneo yao waliyoyatawala nje kidogo ya eneo la Mipaka ya Israel 'yaani Sinai ,Milima ya Golani na sehemu ya Mfereji wa Suez lenye makubaliano ya Umoja wa Mataifa (Armistice Agreement ) ,Vita hii ilipiganwa siku sita tu na kupelekea kushindwa vibaya kwa Egypt ya Gammal Abdel Nasser na Syria Salah Jadid na Nchi washiriki wao waliowasaidia kwa namna moja au nyingine kwa upande mwingine Israel kuchukua maeneo yao waliyohofia wangeyachukua ,Ukanda wa Gaza,Milima ya Golani,Jerusalem Mashariki na West Bank.Swala sio kujadili vita hii lakini kumbe hii vita ikawa ndio chanzo cha mgogoro mkubwa ambao masikini ya Mungu ingekuja kuua mpaka msimamo wa Uchumi wa Kidunia.Inumbukwe kuwa Uchumi wa dunia ya 3 unaathirika moja kwa moja na matukio yote yanayotokea kuathiri dunia ya Kwanza.

Miaka sita baadae kupelekea kuingia madarakani kwa Anwar Sadat Misri baada ya Nasser kufariki 1970 kwa ugonjwa wa Moyo ,huku Historia ikisema pengine ni kutokana na kuaibishwa na Muisraeli kwenye vita,huku Syria Salah Jadid nae akionja kupinduliwa na Wanachama wenzake wa Ba'ath Party mpaka kupelekea Baba yake Bashir Al Assad kuingia madarakani.

Vita ya "Yom Kippur" 1973 ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kutibu vidonda vya miaka 6 iliyopita,kama kisasi kwa Israeli na nia ya kurejesha mali Nasser na Jadid walipoteza katika mikono ya Waisraeli,bila kujua Hafidh Al Assad ambae alikuwa waziri wa ulinzi wa Syria aliempindua Jadid na aliedundwa 1967 na Muisrael huku mwenzake Anwar Sadat akiwa kipenzi cha Marehemu Nasser kwa Pamoja walikuwa wanaenda kutengeneza tatizo kubwa la Kiuchumi ambalo pengine ingechukua muda kwa Dunia ya kwanza kupona na kwa Upande wa Pili nchi za Dunia ya tatu hususani Afrika ndio zisingeweza tena kusimama vizuri.

Israeli kwa hisani ya Marekani inawapiga tena Misri na Syria pamoja na Washiriki wao yaani Nchi Falme za Kiarabu,Urusi ,Venezuela na Cuba kwa Upande mwingine.

Waarabu wakaona aibu ya kupigwa mara mbili na kutumia kigezo cha Mafuta kuipigisha magoti dunia.OAPEC ikiwa ni Umoja wa Nchi za Kiarabu zenye mafuta wakatangaza Embargo.Ikumbukwe kuwa Mafuta ndio yalikuwa Uti wa mgongo pekee wa Uchumi katika dunia ya kwanza ,na Siasa za Mafuta ndio siasa mbaya ambazo mpaka leo zinahofiwa duniani kote hata na Nchi Tajiri.Gaddafi wa Libya alikuwa ndio Rais wa kwanza kuchukua hatua hii ili kuishinikiza Dunia kuwaambia Israeli waachie maeneo yale walioshikiria kwa Hiari yao wenyewe maana jitihada za kivita zilishaprove kushindikana kabisa,Saudi Arabia ikafuata,kipindi hicho "Wahhabi" hao ndo walikuwa na mafuta mengi kuliko mtu yoyote duniani,uamuzi huo ukafuatiwa na Kuwait,Iran,UAE,Morocco,Iraq na Nchi nyingine kwa Sauti Moja pasi kujua maafa ya uamuzi huu wa kuzuia kuuza mafuta yao haswa Marekani na Ulaya , ujumbe waliotaka kuufikisha ulifika lakini je ni nini kingetokea baada ya hapo na kuibadilisha kabisa dunia ya 3......(itaendelea)
 
Nani kakwambia UJAMAA umekucost?

Misingi yake imebadilika kutokana na Siasa za Magharibi!
 
Nani kakwambia UJAMAA umekucost?

Misingi yake imebadilika kutokana na Siasa za Magharibi!

Nitafika huko..usiwe na haraka 'na hata ujamaa wetu ulikuwa ni matokeo ya siasa hizohizo za Magharibi
 
Ungemalizia bandiko lako ndo tukaanza changia coz twaweza changia kwa muono wa mbele zaidi ukasema hujafka huko

Bandiko n zuri malizia au summarize ili tuwe huru kuchangia
 
Ungemalizia bandiko lako ndo tukaanza changia coz twaweza changia kwa muono wa mbele zaidi ukasema hujafka huko

Bandiko n zuri malizia au summarize ili tuwe huru kuchangia

nivumilie kdg au Endelea kufuatilia tu ninaandika taratibu sabbu najua watanzania huwaga hawapendi kusoma vitu virefu
 
nafikiri ungesamaraizi

Ni muhimu kunivumilia kwa manufaa ya wengi lkn mwisho wa article hii ni ushahidi wa kihistoria unaolenga kuonyesha dhahiri ni nani Anaebeba sera ya kuleta maendeleo kwenye hii nchi bila chembe ya Mashaka..kwanini naamini hivyo..picha kamili mtakuwa mmeiona...
 
nivumilie kdg au Endelea kufuatilia tu ninaandika taratibu sabbu najua watanzania huwaga hawapendi kusoma vitu virefu

Mkuu tusiende kwa fikra hzo hili n jukwaa la historia so wewe mwaga data tusome ili tuchangie kwa mantiki ya uzi mzima
 
Back
Top Bottom