Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Inadaiwa kuwa barabara za zege ni imara na zinadumu kwa muda mrefu kuliko za lami. Japo wanasema ni gharama kujenga lakini nchi kama yetu inaweza kuzijenga kwa kutumia malighafi zote kutoka ndani ukilinganisha na zile za lami. Kwa hiyo inawezekana kwetu zikawa na bei rahisi kuliko za lami. Barabara za zege unaweza kujenga kwa nondo au hata bila nondo. Hizi zingetufaa sana kwenye barabara za mitaa kwenye miji yetu. Hata kampuni ndogo ndogo za ujenzi zingeweza kufanya ujenzi huu.
Kwa nini tusiachane na barabara za lami na kuanza kujenga za zege tu?
View attachment 2875303View attachment 2875302View attachment 2875301View attachment 2875300View attachment 2875299View attachment 2875304View attachment 2875305
Kabisa. Hizi za mitaani fupi fupi zingepewa kampuni ndogo ndogo za ndani zipige zege.Mitaani hakuna barabara ndefu huwezi linganisha na kuunga mkoa kwa mkoa kwa rami
Sio kweli barabara za zege ni nafuu sana kulinganisha na barabara ya lamiBarabara za zege ni imara na durable but very expensive. Nashauri serikali ijenge zege maeneo ya mjini yaanj katikati ya miji.
Ndio ni kweli Zinadunda dunda kutokana na Expansion JointHili swali aliwahi kuulizwa bosi wa TANROADS kuwa kama ujenzi wa barabara za zege ni nafuu, kwanini zisijengwe hizo badala ya lami! Alijibu kwamba ni kweli gharama ni nafuu ila wanazijenga zaidi sehemu korofi zenye majimaji chini.
Akasema changamoto za hizi barabara ni kukosa 'smoothness' na 'comfortability' yake ni mbaya tofauti lami iliyonyooka. Ukiendesha gari inakuwa inadundadunda.
Kuliko kudunda kwenye mashimo ni bora kudunda kwenye zege. Zingetufaa sana kwa barabara za mitaani.Hili swali aliwahi kuulizwa bosi wa TANROADS kuwa kama ujenzi wa barabara za zege ni nafuu, kwanini zisijengwe hizo badala ya lami! Alijibu kwamba ni kweli gharama ni nafuu ila wanazijenga zaidi sehemu korofi zenye majimaji chini.
Akasema changamoto za hizi barabara ni kukosa 'smoothness' na 'comfortability' yake ni mbaya tofauti lami iliyonyooka. Ukiendesha gari inakuwa inadundadunda.
Kumbe zinajengwa. Miji yote ingeiga hili.Tembelea mitaa ya tandika zinajengwa barabara za zege mitaani na hazina gharama kubwa kamaunavyodai
Kama mwanza ile barabara ya Igogo-BugandoNadhani mikoa yenye mawe, wajenge barabara za mjini kwa kutumia mawe
Mahondaw amerudi...