Kwanini ubora wa magolikipa upimwe kwa clean sheets!?

Kijuram

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
513
Reaction score
374
Kama topic inavyojieleza. Naamini wapo baadhi ya magolikipa wanapata clean sheets nyingi si kwa ubora wao bali kutokana na mfumo mzuri wa ulinzi unaotumika na timu zao, pamoja na umahiri wa mabeki. Kwa mtazamo wangu ingekuwa bora zaidi kama magolikipa wangekuwa wanapimwa ubora wao kwa uwingi wa saves walizofanya. Tujadili.
 

Na kwanini pia unadhani ubora wa Mwanaume unapimwa kwa idadi ya Mabao / Magoli anayomfunga tu Mkewe / Demu wake 24/7?
 
Utapataje cleen shit bila ku'save.
Kuna magolikipa wanamaliza mechi hawajapigiwa shot on target hata moja, na wengine wanatoka wamefungwa 5 lakini kafanya saves 10 hapo nani anakuwa kafanya kazi.
 
Kwanini forward anapimwa ubora wake kwa kufunga magoli, ukipata jibu haoa utaweza kujijibu na hilo.
 
Kwanini forward anapimwa ubora wake kwa kufunga magoli, ukipata jibu haoa utaweza kujijibu na hilo.
Kazi ya forward ni kufunga magoli na kutengeneza nafasi za kufunga. Kazi ya golikipa ni nini kama sio kuzuia Mpira usiingie golini? Sasa kama yupo golini mpaka mechi inaisha timu yake imeshinda 5-0 huku yeye akiwa hajapigiwa shuti hata moja lililomlazimisha azuie lisiingie golini anakuwa kafanya kazi gani? Mbona tukiangalia vipindi vya summary za ligi mbalimbali kwa wiki au kwa msimu mzima tunaoneshwa best goals na best saves? Kwanini tusioneshwe best clean sheets?
 
Na ndio maana De Gea amekuwa ktk team of the year mara 5 ktk miaka 6 iliyopita epl na katika miaka yote hiyo ni mwaka huu tu ndio anaongoza kwa clean sheet
Ina maana miaka mingine yote alikuwa haongozi yeye kwa clean sheet na still alikuwa anachaguliwa kama golikipa bora
Ingawa zipo tuzo maalum kwa ajili ya clean sheet ila haidetermine kwamba ndio kipa bora
Miaka kadhaa nyuma kule la liga Valdez alikuwa anachukua zamora trophy (kipa aliyeruhusu magoli machache kwa msimu) karibia kila msimu na ukija kwenye tuzo za fifa unakuta casillas ndio kipa bora na valdez hata pua anusi
 
Kuna magolikipa wanamaliza mechi hawajapigiwa shot on target hata moja, na wengine wanatoka wamefungwa 5 lakini kafanya saves 10 hapo nani anakuwa kafanya kazi.
Anapanga ukuta vzr... Halafu hawezi kukosa shuti on target season nzima
 
Golikipa mzuri hapimwi kwa cleansheet tuu na nafikiri sio kitu cha kwanza kumdetermine kipa bora...kuna kitu kinaitwa Expected goals kuna sku nliona makala moja skysports wanaelezea hio kitu ndio hapo utajua nani kipa bora na nani anabebwa na defence yake
 
Huyo kipa aokoi faulu.. Hatoi au kudaka kona??
Unaposema best save huwa ni moja.. Best goal ni moja.. Tofautisha mchezaji bora na goli bora
 
Nadhani kipindi cha nyuma walikuwa wanaangalia sana hayo mambo ya clean sheets ila kwa miaka ya karibuni ligi nyingi wana angalia number of saves alizo fanya kipa kumchagua kuwa kipa bora. Kwa hiyo ubora wao unapimwa kwa idadi ya saves alizo fanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…