Kwanini Ufugaji wa Nguruwe Unaweza Kuwa Utajiri Mkubwa?

Anayetajirika haraka ni yule anaechukua - chinja na ondoa kichwa, miguu na mapupu kisha kuviuza kwa bei tofauti na makubaliano ya awali na mfugaji

Ka huamini tembelea machinjio ya k-moto ndo utaona mnyororo wa thamani ulipo
Uko sahihi,hawa jamaa wanapiga hela na ndo wanaokuamulia faida au hasara
 
Mimi nafuga nguruwe kibiashara.
Hawa wanaotangaza biashara wanaongeza namba na kutaja faida kubwa tu hawakuambii changamoto.
Uzoefu wangu:
Nguruwe hubeba mimba miezi 3 majuma(week) 3 na siku 3.
Huzaa watoto wastani 8 mpaka 12. Uzao wa kwanza wanaweza kuzaa hadi 4, mzoefu anaweza kuzaa wengi zaidi 16 kutegemea na mambo mengi tu.
Kweli nguruwe wanauzwa bei kubwa na wanahitajika Sana.
Changamoto kulisha nguruwe gharama kubwa hasa ukiwa mjini hauna chakula Cha ziada ulicholima mwenyewe.
Pia magonjwa ya mlipuko ya nguruwe tatizo kubwa. Mfano homa ya nguruwe kizungu African Swine Fever (ASF).
Mwisho wafanyakazi wa kuhudumia nguruwe wanaweza kusumbua hawakai muda mrefu unajikuta unatafuta na kufundisha kazi wapya mara kwa mara.
 
Mimi ninajirani yangu anaitwa Mohamed.Aliacha kunisalimia kisa nafuga nguruwe.Siku Moja nikaamua kuchinja na kuipika vizuri na yeye nikampelekea.Toka siku hiyo akawa ananisalimia na kuomba nyama nyingine.
Na mimi nina rafiki yangu msabato tulikuwa chuo, tukaenda kuoiga kitimoto yeye akasema atakula ya mbuzi. Walipoleta kitimoto imewekwa na ka mchicha kidogo, weeee, tangu Siku hiyo humwambii kitu mbele ya kitimoto!
 
Unasahau kuwa mtu mmoja anaweza kukaa ng'ombe 50 walewale kwa miaka mitano au zaidi, ila mtu hawezi kukaa na nguruwe mmoja kwa mwaka mzima.
Nguruwe wanna mzunguko wa haraka zaidi.
 
Nguruwe wanatengeneza faida haraka sana japo wanakula Sana.
Yaani kufuga nguruwe unahitaji kuandaa badger kubwa ya chakula chao
 
Kwasababu nguruwe wana kazi sana kuwafuga...kwanza wanakula sana...na wakianza kuumwa ni shida.,.pili watu wanafanyiwa figisu na wale wanayoiona ni haramu
 
Wengine wenye uzoefu na ufugaji waje watoe elimu ili na wengine tuanze
 
Mkuu kwa mtu anayeanza kufuga nguruwe kibiashara unamshauri aanze na nguruwe wangapi? Je mtu ukishaanza kufuga baadae wanaweza kujiendesha wenyewe? Kama unaweza tunaomba mchanganyiko kwa anayeanza kufuga ikiwa ana eneo la kuanzia
 
Mkuu kwa mtu anayeanza kufuga nguruwe kibiashara unamshauri aanze na nguruwe wangapi? Je mtu ukishaanza kufuga baadae wanaweza kujiendesha wenyewe? Kama unaweza tunaomba mchanganyiko kwa anayeanza kufuga ikiwa ana eneo la kuanzia
Idadi ya kuanzia inategemea na msuli wako yaani mtaji wako.
Gharama za kulisha nguruwe zinafikia 75% ya gharama zote za mradi hadi kuanza kupata faida.
Ningeshauri watu waanze na nguruwe wachache kama hauzalishi chakula mwenyewe.
Nenda kafugie mahali ambapo utapata chakula mbadala unacholima mwenyewe.
Wengi wanashindwa mradi wa nguruwe sababu ya kushindwa gharama za kulisha mifugo.
Kama una Tsh 1 - 3M baada ya kujenga mabanda anza na nguruwe 3 - 4.
Nazungumzia nguruwe ambao siyo pure breed, Hawa wa michanganyiko ya holela wa bei rahisi laki 2 hadi 3 kwa piglet wa miezi 2 hadi 3.
Kisha wakizaa unauza baadhi unanunua pure breed 1M na zaidi kwa piglet. Vizuri ukinunua dume pure breed unapandisha mbegu ya hao wa zamani.
Hawa breed ya hovyo unatafutia mtaji na uzoefu wa kufunga.
Huwezi nunua piglet 1.5M alafu anakufa sababu ya kukosa uzoefu inakuwa hasara kubwa au itakukatisha tamaa.
NASHAURI WAONE WATAALAM KAMA HAWA RUBABA.
 
Homa ya nguruwe na wafanyakazi hapo ni kasheshe.

Hayo mengine ya msosi hasa mahindi ni rahisi kulima japo hao Jamaa Wanahitaji lishe Bora.
 
Mt anakaa na ng'ombe adi miaka mitano uku ana zaa wakat nguruwe akimaliza mwaka1 tu iyo ni bahat kwaiyo lazima nguruwe waonekane wachache kuliko ng'ombe
 
Jambo jema!!
Kazi ni kipimo cha utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…