My county
Member
- Aug 6, 2016
- 22
- 60
KWANINI MRADI WA UZALISHAJI UMEME WA MAJI BWAWA LA NYERERE MTO RUFIJI NI MUHIMU?
Mradi huu unatarajia kuzalisha megawati 2,115 za umeme hatua ambayo inaelezwa kwamba itasaidia kupunguza tatizo la nishati hiyo muhimu kiuchumi na kijamii hapa nchini. Wasomi wanaeleza kukamilika kwa mradi huu kutakuwa ni habari njema kwa sekta nyingi ikiwemo viwanda ambavyo wawekezaji wake wamekuwa wakilalamikia gharama kubwa za bei ya nishati ya umeme na ambao sio wa uhakika hali ambayo inapelekea kuwepo kwa gharama kubwa katika uzalishaji wa bidhaa hapa Tanzania ukilinganisha na bidhaa zinazotoka nje hivyo kushindwa katika ushindani wa soko.
Kwa sasa Tanzania inalipa dola za kimarekani senti 10.7 kwa uniti moja ya umeme kiasi ambacho ni kikubwa tofauti na nchi kama Misri inayolipa dola za kimarekani senti 4.6, Korea Kusini na China dola za kimarekani senti 8, Afrika Kusini dola za kimarekani senti 7.4, India dola za kimarekani senti 6.8, Ethiopia dola za kimarekani senti 2.4, Uingereza dola za kimarekani senti 0.15 na Marekani dola za kimarekani senti 0.12.
Kukamilika kwa mradi huu kutashusha bei za umeme hapa nchini kwa kati ya asilimia 35-40 hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
Gulatone Masiga.
masigag1987@gmail.com
Sent using Jamii Forums mobile app