Kwanini Ujerumani ina idadi ndogo ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID -19? Tanzania tuna cha kujifunza

Kwanini Ujerumani ina idadi ndogo ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID -19? Tanzania tuna cha kujifunza

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Wakati ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Corona ukiendelea kusambaa na kuua watu wengi duniani, nchini Ujerumani idadi ya watu walokufa ni ndogo kulinganisha na nchi zingine barani Ulaya na duniani kwa ujumla

Kwa mujibu wa taasisi ya Robert Koch hadi kufikia Ijumaa asubuhi watu 13,957 walikuwa wameambikizwa ugonjwa huo na idadi ya vifo ilikuwa ni watu 31.

Hii inaifanya nchi hii kuwa na asilimia 0.22 tu ya idadi ya vifo zaidi ya Italia ambayo ina asilimia 8.3 na Uingereza asilimia 2.2 na hiyo ni licha ya kwamba Ujerumani ina watu 10,688 zaidi ya Uingereza.

Ujerumani nchi ambayo inaongoza baraani Ulaya kwa uchumi mkubwa wamekuja na mikakati kadhaa ya kukabiliana na ugonjwa huu hatarti wa COVID -19

Majaribio

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani majaribio ya mara akwa mara kwa kesi mpya za wagonjwa ni muhimiu kufanywa na maabara.

WHO wamekuwa wakisisitiza kwa nchi mbalimbali kufanya majaribio na nchi za Korea Kusini na Ujerumani zimekuwa mstari wa mbele kufanya majaribio kwa wananchi wake kabla ya ugonjwa kuenea hivyo kurahisisha zoezi la kuwaamuru raia kujitenga kwa kukaa majumbani.

Ujerumani walianza kufanya majaribio tokea mwezi January mwaka huu kwa kusambaza vifaa vya kufanyia majaribio hayo katika mahospitali na vituo vya afya nchi nzima.

Mtu ambae anaonyesha dalili za kawaida au ambae amekwishaambukizwa ugonjwa huo, hufanyiwa vipimo mara moja na kuanza kupata matibabu.

Pia kuna sehemu maalum za kupita na gari kisha kuacha sampuli ya mkojo wako ili ukapimwe.

A person throws a sample into a collecting container at the mobile Corona-Drive-In in Schoenebeck near Magdeburg, eastern Germany (Photo: Getty)
Mwananchi akiweka sampuli kwenye kontena maalum kwenye "Corona-Drive-In" kwenye kitongoji cha Schoenebeck karibu na Magdeburg, Ujerumani mashariki

Nchini Uingereza mtu ambae ameonyesha dalili baada ya kuambukizwa huendelea na maisha bila kupata nafasi ya kufanyiwa vipimo na hivyo kuendelea kuambukiza watu wengine na kusababisha idadi kubwa ya watu wenye dalili ya uginjwa huo.

Nchini Ujerumani zipo sehemu maalum za kukusanyia sampuli za mkojo ziitwazo Corona- Drive-In ambapo mwananchi anaacha sampuli hizo ili zende kupimwa.

Umri mdogo

Majaribio na vipimo nchi Ujerumani vimebainisha kuwepo kwa idaidi kubwa ya watu wenye umri mdogo ambao walikuwa wana dalili za ugonjwa na kuwa hawakuwa na hali mbaya kiasi cha kuhatarisha Maisha hivyo kupata nafuu haraka na kupona dalili hizo.

Watu walochukuliwa kuwa wako hatarini au High risk ambao walikuwa na magonjwa mengine na wenye umri Zaidi ya miaka 70, pia idadi yao ilikuwa ni ndogo na hawakuwa matatizo yanayotatiza afya zao.

Kesi 6,557 kati ya 8,198 zilizorekodiwa zilikuwa ni za watu wenye umri kati ya mika 15 na 59 wakati wenye umri wa kati walikuwa ni wa umri wa miaka 47

Italia nchi ambayo ni ya pili barani Ulaya kwa kuwa na idadi kubwa ya wazee, imejikuta ikikubwa na dhahama hii ya uginjwa huu wa hatari na wazee hao umri wa wastani walio nao ni miaka 79.5

Wakati huohuo rekodi zinaonyesha kuwa watu walopimwa na kukutwa na dalili za uginjwa wa COVID-19 wana wastani wa miaka 63 na wengi wa walokuwa tayari walikuwa wanasaumbuliwa na magonjwa mengine.

Hivyo basi, serikali zingine hususani serikali ya Tanzania ingechukua nafasi hii kuhakikisha ina vifaa vya kupimia vya kutosha na pia kuhakikisha hospitali zetu zimesheheni vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huu kupita wagonjwa ambao wengi wao huhitaji mashine maalum za kusaidia kupumulia.
 
Je ulitaka wafe wengi?
Kwan Tanzania tuna vifo vingi vya Covid19?
Huoni kuna haja ya wao ndio waje kujifunza kwetu hatuna record ya mtu kufa na hayo mafua .
 
Je ulitaka wafe wengi?
Kwan Tanzania tuna vifo vingi vya Covid19?
Huoni kuna haja ya wao ndio waje kujifunza kwetu hatuna record ya mtu kufa na hayo mafua .

Kuna haja ya kuhakikisha wazee wetu wanapata uangalizi zaidi kutokana na afya zao.

Zaidi ya hapo tumejitahidi sana kama nchi kuhakikisha watu wasafiri wanaoingia nchini wanajitenga kabisa kwa siku 14.

Maana raisi kasema kwenye hoituba kwa taifa kwamba kati ya wagonjwa 12 waliopoa Tanzania ni 4 ndo wanaotoka nje ya nchi.
 
Ni suala la muda tu lazima graph itasoma asilimia 9.5 mpaka 10.0 kwa mataifa yenye wazee wengi na mataifa hayo yaliyoendelea Kiuchumi na huduma za afya yapo Marekani ya Kaskazini, Ulaya, Mashariki ya Mbali.

Yaani mfano kikokotoo cha 10%, kukiwapo na maambukizi ya watu 20,000 ktk waliopimwa , kirusi cha coronavirus husababisha vifo 2000 hiyo ndiyo trend.
 
bagamoyo,
Njia nzuri ni kuzuia mikusanyiko ya watu yaani social gatherings.

Inatakiwa hata kama watu wakiambukiwa iswe zaidi ya mmoja hivyo ndani ya mwezi idadi ya waloambukizwa isizidi watu 30.
 
Back
Top Bottom