Kwanini ukiwa na marafiki wanaopenda kusindikizwa katika mambo yao huwa wako tabia hizii ??

Kwanini ukiwa na marafiki wanaopenda kusindikizwa katika mambo yao huwa wako tabia hizii ??

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,822
kuna utafiti nimeufanya mtu ukiwa na marafiki wa aina flani wenye tabia ya kupendwa kusindikizwa katika mambo yao japo sio wote ila wengi wao sijui wako hivi

kuna wengine unakuta anakuomba umsindikize sehemu au mahala kama rafiki yako lakini ukifika kule sasa kuanzia gharama za kula na mambo mengine anakuachia iwee ni juu yako badala yake yeye .....

kuna wengine ndo kabisa unakuta anakuomba umsindikize sehemu mfano na hiyo sehemu unakuta anaenda kupiga dili zake na wewe kama rafiki anakuomba umsaidie kufanya mambo mawili matatu ila akishakamilisha dili zake mnarudi mlipotokaa cha ajabu hata kama kapiga dili hakupi hata hela ya maji ya kunywa yeye atakukushuru umesindikiza salama na mmerudi salama yaani hata kukufikiria kukupa hata kidogo hamna na kabisa akikuangalia anaona umechoka mnoo

hivi huwa najiuliza hivi hawa huwa ni aina gani ya marafiki na kwanini wanakuwaga wako hiviii ......
 
Sinaga rafiki wa matumizi. Nina rafik wa mapato
 
Na wewe kwa nini ukubali kwenda sehemu ili mradi tuu.
Kuwa na rafiki haimaanishi kuwa kila kitu lazima ufnye kwa sababu ni rafiki
Wewe pia unauwezo wa kuuliza unakotaka nikusindikize kuna nini na mimi nitanufaikaje
Kama kweli ni rafiki ako akuoe deatail zote na sio unasindikiza kisa tuu ni rafiki kakuomba.
 
siku zote ukiona umezungukwa na marafiki ambao hawajui thamani yako na maisha yako kaa ukijua umezungukwa na wachawi

ivi kweli mtu una rafiki yako anakutoa hapo ulipo anakupeleka sehemu mathalani kariakoo unazunguka nae siku nzima huku jua kaliii likikupiga baada ya mishe mishe kukamilika unarudi nyumbani umechoka mnoo una kiu kali, njaa imekushika alafu lijitu lililokupeleka huko halikupi hata elfu 5 au tatu ya maji kidogo upozeee kiuuuu.

kiukweli kama ni mimi bora matendo urafiki ufee tuu ubakie urafiki wa macho na mdomo tukikutana tunasalimiana tuu
 
Kwani maana ya urafiki ni nini? Ina maana unaweza kumtoza gharama ya kwenda mahala au jambo fulani rafiki yako? Je wewe ukiwa na shida huwa hasaidii? Huwa hamli bata pamoja siku za mapumziko? Binafsi siwezi kumlipa rafiki yangu kwa jambo alilonisaidia au nililomsaidia. Najisikia furaha kumsaidia bila kufikiria nimetumia kiasi gani au muda gani. Mara nyingi huwa tunafanya mambo bila kuhesabu how much nimetumia kwa ajili ya rafiki yangu. Hadi tumekuwa zaidi ya rafiki. Ukianza kufikiria namna ya kumtoza rafiki yako huo sio urafiki.
 
Back
Top Bottom